Hausigeli Akatwa Mdomo, aunguzwa na pasi

nyamagaro

JF-Expert Member
Feb 25, 2010
394
101
Sumiati Binti Sala Mustapa akiwa katika hospitali ya Mfalme Fahdi mjini Madina alipolazwa.
MFANYAKAZI wa ndani raia wa Indonesia, aliyekuwa akifanya kazi katika nyumba moja nchini Saudi Arabia, amelazwa hospitali katika chumba cha watu mahututi baada ya kukatwa sehemu ya mdomo wake na kuchomwa kwa pasi ya moto sehemu mbalimbali za mwili wake na bosi wake.

Mfanyakazi huyo wa ndani aitwaye Sumiati Binti Sala Mustapa amelazwa hospitalini kufuatia mateso toka kwa bosi wake wa mji wa Madina, mwanamke raia wa Saudi Arabia mwenye umri wa miaka 53.

Sumiati alishambuliwa na muajiri wake ambaye hivi sasa ametupwa rumande. Sumiati alikatwa sehemu ya mdomo wake kwa mkasi, aliunguzwa na pasi ya moto mgongoni na alipigwa sana miguuni kiasi cha miguu yake kukaribia kupooza na kumfanya atembee kwa tabu sana.

Kwa mujibu wa gazeti la Saudi Arabia la Al-Watan, kipigo alichopewa Sumiati kilisababisha kuvunjika kwa baadhi ya mifupa ya mikono na mbavu zake.

Maafisa wa Saudia na maafisa wa Indonesia walikutana juzi mjini Madina kujadili kesi ya Sumiati ambayo imesababisha mtafaruku mkubwa nchini Indonesia.

Maafisa wa serikali ya Saudi Arabia wameahidi kuifuatilia kesi hiyo kwa ukaribu zaidi.

Sumiati amelazwa kwenye hospitali ya Mfalme Fahdi mjini Madina ambapo madaktari wamelazimika kumfanyia upasuaji wa kurekebisha sura yake iliyoharibiwa vibaya.

Hii ni miongoni mwa kesi ambazo zimekuwa zikitokea katika nchi za kiarabu katika siku za hivi karibuni.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom