Hatutarudi nyuma – Sheikh Farid

Mie kwa kuongezea ujumbe kwa Mohamed Aboud, hivi wewe wa wapi? inabidi tujiulize - mapinduzi ya mwaka 1964 wewe ulikuwa wapi? inaonesha ulikuwa hujaja zanzibar (unguja na pemba) kweli enhe?
 
Mimi naona swali la muhimu moja tuu. Hawa mashehe wanapata wapi nguvu? Who is behind them
 
Hatutaki Muungano
Today 14:29

Junior Member
Array
Join Date : 30th May 2012
Posts : 2
Rep Power : 0
Likes Received : 0

Likes Given : 0



Duh! Leo leo!!
 
siyo kutafuta uhuru ila tu baadhi ya wazanzibari wanafanya uvunjivu wa amani jambo ambalo hatari kwa maisha ya wapenda amani:lock1:

Amani haitokuwepo kama hujaanza na vita - Hivi kweli kama mwanamke uliye muoa akikwambia kuwa sikutaki tena basi niache, utaendelea kuishi nae - labda kwa wenye vichwa vilivyozidi nyuma - sasa sisi tumesema basi hatutaki tena muungano jamani hebu tuacheni na ki-jinchi chetu, hivi mumeona wapi watu 45Milioni kufanya muungano na watu 800,000 maajabu ya Mussa haya.
 

Hata mimi kinachonshangaza na kunipa hofu ni upinzani huu kuanzia msikitini, kuna ajenda gani nyuma ya pazia?
 
Hii move ni nzuri lakini kwanini wanafanyia 'msikitini'??

Hivi makanisa yakichomwa kwa mazingira haya nani alaumiwe kama si wao??

Kwa nini wasifanyie suala hili nje ya ulingo wa 'dini'??

BTW, Hongereni wakuu tuko pamoja hadi 'kieleweke' huko Zenj!!
 
Is this Sheikh still at large?

Baada ya kuona hiyo picha, nimeingiwa na wazo kwamba initiators wa hii kitu kumbe ni masalia ya ile familia ya Al Mazrui, hebu rudini kwenu huko ghuba ya Uajemi msituletee fujo hapa....
 
Mimi naona swali la muhimu moja tuu. Hawa mashehe wanapata wapi nguvu? Who is behind them

Jibu muhimu ni moja tuu, Wazanzibari ndio walio nyuma yao na ndio wanaowapa nguvu hizo, Zanzibaris are behind them and fully committed
 
Hivi huyo Farid na Mwenzake asili yao wapi? au kukulia Zanzibar na Passport ya Oman umenakuwa Mzanzibar automatically? je walisha ukana uraia wao asilia walipofikisha miaka 18?
Maana naona kama wapo kama al Qatada
 
eti nchi yetu..nchi gani ina mikoa miwili tu...fanyeni kazi wazenji nyie acheni kutafuta umaarufu usiokua na mbele wala nyuma

Hata Kama ina kajimkoa kimoja ndo ya kwao ndugu yangu...


Sent from my iPad using Tapatalk HD
 
Ovyo kabisa huyo Sheikh, sina hakika kama yuko na akili timamu! Basi aende msituni kama kika Joseph Koni. Maana njia stahili ya kupata suluhu ya chochote ni kukaa mezani unless kama unataka kumwaga damu.
 

Hapa inahitajika busara kubwa sana ama sivyo Nchimbi & Co watakuja kuadhirika

maandamano na mikutano imepigwa marufuku lakini watu wanakutana kama kawaida bila kuogopa

hii Arab Spring imewapa sana watu moyo
 
Hata mimi kinachonshangaza na kunipa hofu ni upinzani huu kuanzia msikitini, kuna ajenda gani nyuma ya pazia?

Ndugu yangu usiwe na hofu juu ya hili, sisi Wazanzibari tuna-experience ambayo nyie wenzetu wa bongo hamna, Tukipitia chama wasema hawa wanataka kutugawa na kumwambia tendwa wafute na watatusimamisha mara moja. Ila kwenye msikiti nani ataufunga - hayupo na kama wanataka wajaribu tu, wameona Trailer ile 26th na 27th. Sasa sisi hatuna ugomvi na wakristo wala wabara waliopo hapa unguja na pemba - ikiwa hawatoingilia wala kujifanya wao wako kimbelembele kitawakuta kilichompata firauni. Maana saivi hatutanii kwa hili - hadi nchi ipatikane.
 
Jibu muhimu ni moja tuu, Wazanzibari ndio walio nyuma yao na ndio wanaowapa nguvu hizo, Zanzibaris are behind them and fully committed

Zanzibar inamilikiwa na msikiti gani? Hizi pesa za Alshabab na Boko haram zitawamaliza! By the way ninyi ni wepesi sana kwetu!
 
Hufu yangu wakijitenga kunaweza kuwa ni kituo cha al shahab na al Quida
 
Ovyo kabisa huyo Sheikh, sina hakika kama yuko na akili timamu! Basi aende msituni kama kika Joseph Koni. Maana njia stahili ya kupata suluhu ya chochote ni kukaa mezani unless kama unataka kumwaga damu.

Hivi wewe umeambiwa na nani kama unaakili wewe mwenyewe, kwasababu ukionacho kwenye sura ya mwenzako ndio ulichonacho wewe. Suluhu ya kwenye meza ni kwa wenye akili wanaoambiwa wakajiambia na kusikia - wewe unaambiwa hatutaki muungano unang'ang'ana musijadili muungano ila katiba tu, ebo! hivi hizo ndio unaona wewe ni akili - hebu muulize tena aliyekuambia kuwa unazo kweli. Lakini sishangai akili haikai miguuni ni ajabu hii........?!!!
 
eti nchi yetu..nchi gani ina mikoa miwili tu...fanyeni kazi wazenji nyie acheni kutafuta umaarufu usiokua na mbele wala nyuma

Wataalam, Ili uwe nchi inatakiwa uwe na Eneo la ukubwa gani ?
 
wazanzibar km sheria ya katiba hairuhusu kujadili muungano msitumie dini nawashauri anzisheni kampeni ya nyumba kwa nyumba kwa lengo la kuiweka kando ccm 2015,unganeni bila kujali itikadi ,wakiona hivyo wenyewe watalegeza masharti na muungano utajadiliwa vinginevyo ccm wataendelea kuwakandamiza kama ambavyo wamepeendekeza wao badala ya wananchi kwamba wanataka mfumo uliopo uendelee.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…