Hatutaki Dom iwe kama Dar

Hatutaki Dom iwe kama Dar

Binafsi naona tayari makosa yameshafanyika na yanaendelea kufanyika, sioni projects zozote zinazoendeshwa na watu wa real estates business zaidi kama unavyosema wanajenga watanzania wasio na vipato na wanaishia kuunga unga tu, sioni ujenzi wowote wa highways za kuingia kutoka na hata ndani ya mji, city centre imeachwa vilevile na mbanano labda ibaki old city na kujengwe mji mwingine uliopangiliwa na kila kitu, sioni ujenzi wowote wa gardens za kupumzikia, maeneo ya michezo nk, sioni ujenzi wowote wa malls za kisasa zaidi ya ujenzi wa frames za kukodisha, kifupi taabu tu na ni kama tunaendeleza yaleyale ya Dar na Mwanza..

well said mkuu
 
Dar ilitakiwa iwe somo kwa wenye mamlaka lakini utaona bado hakuna tulipojifunza na kuendelea kurudia makosa yaleyale..

90% ya wakazi wa dar tunaishi kwenye vibanda umiza, kifupi Dar hata uwe na nyumba nzuri vipi bado unaishi kwenye skwata area tu, huna pakutupa taka, huna barabara nzuri za kupita, kiwanja unachoishi ni 20mx20m, Ona Sinza, Msasani, Mikocheni, Kijitonyama kulivyobanana na watu wanavyosifia na kurank hayo maeneo lakini uhalisia maeneo hayo ni hatari kwa Afya kwasababu ya mbanano uliofunga mpaka njia za maji na mzunguko wa hewa..hapo bado eneo kubwa la Manzese, Tandale, Magomeni, Ubungo, Buguruni, Tandika, Vingunguti, Kiwalani, Mtoni, Tandika, Mbagala, Kariakoo, Kigogo nk.. Hivyo utaona sehemu kubwa ya jiji lilivyo chafu na ukiwa angani ndio utaelewa haya.. Makosa yaleyale yanarudiwa kwenye maeneo mapya kama, Mbezi, Goba, Bunju, Kijichi, Chamazi, Kibaha, kibamba, Kiluvya, Tegeta, Bunju, Boko nk..

Watanzania tujifunze sasa, kujenga kuachiwe makampuni yajenge apartments zilizopangiliwa kwa ramani za miji, watu wauziwe apartments kwa bei rafiki iwe cash au mikopo, Serikali isimamie hili kwa kutoa unafuu mkubwa wa kodi kwenye vifaa vya ujenzi na viwanda vyote vinavyozarisha humu ndani vipewe punguzo kubwa ili bei ya bidhaa za ujenzi iwe nafuu na watanzania wakae kwenye nyumba bora, Biashara ya kupangisha nyumba waachiwe estates agency na si kila mtu ili pia nyumba hizo ziwe bora na nafuu..
 
Dodoma mji wa manzi, trachoma, ukoma , vichaa na maombaomba, sifa ambazo The City of Paradise DSM hamna hayo makorokocho.
Dodoma ni jiji la CCM, na DSM ni jiji la CHADEMA ndio maana kwenye uchaguzi halali wa 2015 majimbo mengi ya DSM yalichukuliwa na CHADEMA huku CCM ikilamba majimbo yote ya Dodoma
 
Tuambie hapo ulipo ni eneo gani unaweza fanannisha na Mbagala?.au Tandale?.Dar kila kitu ndugu.Jiji la kukufikirisha jinsi ya kupata pesa,huku mikoani majitu ni mepesi kuridhika,vichwa butu.Ukikuta kachangamka jua huyo katoka Dar au Arusha,
Ndio maana viongozi wote nikutoka mikoani "vichwa butu" hata mkuu wenu hapo wa mikoani. Lini Dar au Tz iliongozwa na wajanja wa Dar au Arusha kama kauli yako?
 
Binafsi naona tayari makosa yameshafanyika na yanaendelea kufanyika, sioni projects zozote zinazoendeshwa na watu wa real estates business zaidi kama unavyosema wanajenga watanzania wasio na vipato na wanaishia kuunga unga tu, sioni ujenzi wowote wa highways za kuingia kutoka na hata ndani ya mji, city centre imeachwa vilevile na mbanano labda ibaki old city na kujengwe mji mwingine uliopangiliwa na kila kitu, sioni ujenzi wowote wa gardens za kupumzikia, maeneo ya michezo nk, sioni ujenzi wowote wa malls za kisasa zaidi ya ujenzi wa frames za kukodisha, kifupi taabu tu na ni kama tunaendeleza yaleyale ya Dar na Mwanza..
Uko sahihi kabisa huku mji wa govt Mtumba hadi Chamwino Ikulu wangeanza project ya new Dodoma as New Cairo (samahani kwa mifano mingi ya Misri ndio nchi naijua sana tofauti na Tz? ) halafu kule kubaki old Dodoma ila wameshaanza mambo ya Dar kuvunja majengo ya zamani (Mliokuwa mnaijua Paradise Cinema) sasa ishavunjwa sijui wataenda kuvunja na NK?
 
Kwako mtukufu rais wizara na taasisi husika pamoja na wadau wa Real estate naomba mjenge majengo ya kisasa ya kuishi, namaanisha magorofa (apartments) msiwaachie wananchi wajenge peke yao kwani wengi wao wanachafua mazingira hawajengi mfano ni eneo mkabala na mji wa govt, kuna nyumba zinajengwa kwa kasi na hazina viwango hvyo mji wa govt ukikamilika utakuwa mzuri huku pembeni yake kuna mji wa hovyo, igeni hata Misri ukitoka Giza kurudi city centre kupitia Citadel najua mshawahi fika mmeona mji ulivyojengwa .Nawasilisha

Sidhani kamma maghorofa makubwa ni muafaka kwa Dodoma kutokana na suala la matetemeko ya ardhi kwa mji huo
 
Back
Top Bottom