Hatuna mbunge Chilonwa

Hatuna mbunge Chilonwa

manning

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2013
Posts
5,092
Reaction score
11,947
Wakuu wana jf
Sisi wakazi wa Vijiji vya Nzali , Mlimwa , Membe,Dabaro na vijiji vingine vya eneo hili hakika hatuna mbunge. Nadiriki kusema hivyo kwa sababu kwa miaka kibaao tangu dunia iumbwe tunakuwa kisiwani msimu wote wa mvua zinaponyesha na hata kunapokuwa hakuna mvua miezi kama hii kutokana na kukosa daraja la kupitisha maji kwa chini badala yake kuna ( flat screen tunavyoliita wenyeji)katika bonde la mto Nyasungu ambalo liko mpakani mwa vijiji vya Nzali na Mahama kata ya Chilonwa. Jambo hili limekuwa kero na kilio cha wananchi wa maeneo niliyotaja kwa mda mrefu tangu mbunge wetu akiwa Naibu Waziri wa ujenzi mpaka leo bado suluhu haijapatikana. Aidha Mbunge wetu hatukusikia anazungumza lolote kuhusu adha hii wakati bajeti ya Magufuri ilipowasilishwa. Kwa adha tunayopata sisi wananchi wa maeneo haya tunadiriki kusema hatuma Mbunge kwani hatusaidii kwa lolote wakati alipo Bungeni Dodoma mpaka sehemu husika ni kilomita 45. Wakati wa mvua kali mbunge huyo aliitwa na akaja kujionea hali halisi. Watu kwa hasira walimlazimisha avuke kwenda Nzali lakini aligoma Kabisa kwa khofia maisha yake , kwa hali hii tunadiliki kusema hatuna mbunge na tunaomba wenye kutaka ubunge wenye uchungu na wananchi wajitokeze kwa wingi mwaka 2015 nasi tutawapa kura bila kujari chama wa upinzani atapewa uzito mkubwa. manake huyu ameongoza kwa zaidi ya miaka 20 amejisahau kabisa
NAWASILISHA WANA JF NJOONI MTUSAIDIE

SAM_3344.JPG SAM_3346.JPG
 
We nawe hutabiriki utafikiri umeme wa tanesko bana mara kibao unakosoa sana wapinzani halafu leo unaleta mahaba ya ki Tanga kuwa na msimamo mpwa wangu
 
Mbunge wao wakati wa uchaguzi unamkuta anapiga pombe inautwa CHOYA na wananchi wake , baada ya hapo wanampa kura bila matatizo.
 
Mkoa mzima wa Dodoma umewahi kusikia una wabunge?Waliopo ni wabunge wa serikali kutoka mkoa wa Dodoma!Mpaka akili itakapowasogea ndipo mtakapojua umuhimu wa kuchagua wabunge wenu na sio wa serikali.Poleni lakini.

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Mkuu umenena kweli kabisa. Mkoa wa Dodoma hauna wabunge kabisa. Chukulia mfano wa Mbunge wa Dodoma mjini ndg. Malole ni hakuna kitu, Mtera kuna kichwa kinaitwa Lusinde, ukija Kondoa kuna kichwa kinaitwa Juma Nkamia, huyu ndio hewa kabisa...

My poor Dodoma!
 
Mleta mada umeandika ukichukulia hadhira yako nzima inamjua huyo mbunge na mahali lilipo hilo jimbo unalozungumzia. Weka background information iliyokamilika ili wasomaji wasipate tabu kukumbuka au kujua ni mbunge gani hasa na wa wapi anayezungumziwa. Yaani umeandika kama unaowaandikia wote ni wakazi wa huko Chilonwa mkuu.
 
Yule mzee Chibulunje hakuna kitu kabisa. Kazi yake ni kukaa tu bungeni, hakuna mchango wowote anaoutoa kwa ajili ya jimbo lake. Hata alipokuwa naibu Waziri wa ujenzi hakuna lolote alilokuwa anafanya hadi alipopigwa chini.
 
Nadhani Chibulunje sio yeye tu. Tukianza na Malecela, Lisinde Job, Kuwayawaya Steven, Lubereje George, Ndugai Job, Teu gregory, Kusila, Nkamia J. ni wote hamna kitu ns sijui watucwa Dodoma wamelogwa na nani mpaka wakawa watu rahisi kuhongeka tena hongo ya pombe ya kienyeji ya sh. 250/-. Huu mkoa nafikiri utakuwa wa mwisho katika mgeuzi na utajikuta uko peke yake ndio umebaki na CCM. Bila huruma ya Nyerere kusema Dodoma iwr makao makuu ya chama na srikalu sipati picha Dodoma ingekuwaje. Wagogo ndio kabisa hawajui kutofautisha katiya asubuhi na jioni. Kopo moja la pombe basi huyo mtu anaonekana nusu Mungu. Angalia Ndugai na Teu walipita bila kupingwa ndio utajua wagogo watabaki kuwa nyuma na CCM yao ndio inawamaliza kabisa.
 
Mleta mada umeandika ukichukulia hadhira yako nzima inamjua huyo mbunge na mahali lilipo hilo jimbo unalozungumzia. Weka background information iliyokamilika ili wasomaji wasipate tabu kukumbuka au kujua ni mbunge gani hasa na wa wapi anayezungumziwa. Yaani umeandika kama unaowaandikia wote ni wakazi wa huko Chilonwa mkuu.

CHILONWA MKUU iko katika Wilaya ya Chamwino mkoa wa Dodoma na Mbunge wake anaitwa Chiburunje mzee wa kutafakari kama Wassira.
 
Nadhani Chibulunje sio yeye tu. Tukianza na Malecela, Lisinde Job, Kuwayawaya Steven, Lubereje George, Ndugai Job, Teu gregory, Kusila, Nkamia J. ni wote hamna kitu ns sijui watucwa Dodoma wamelogwa na nani mpaka wakawa watu rahisi kuhongeka tena hongo ya pombe ya kienyeji ya sh. 250/-. Huu mkoa nafikiri utakuwa wa mwisho katika mgeuzi na utajikuta uko peke yake ndio umebaki na CCM. Bila huruma ya Nyerere kusema Dodoma iwr makao makuu ya chama na srikalu sipati picha Dodoma ingekuwaje. Wagogo ndio kabisa hawajui kutofautisha katiya asubuhi na jioni. Kopo moja la pombe basi huyo mtu anaonekana nusu Mungu. Angalia Ndugai na Teu walipita bila kupingwa ndio utajua wagogo watabaki kuwa nyuma na CCM yao ndio inawamaliza kabisa.

wametufanya kuwa masikini na wajinga ili watutawale , kumbuka mgombea aliekuwa CDM kata ya Chilonwa Julius Nyakapara kamati nzima ya CCM kata ya Chilonwa walienda kumshawishi aachane na CDM na arudi CCM . huyu bwana kwa kuwa ni mjanja aliwapa masharti ambayo bado hawajayatekeleza. Kazi yao sasa si kutekeleza ahadi zao na kutatua kero zao ila ni kuwanunua watu ili warudi CCM BILA KUFANYA UTAFITI KAMA HAO WATU WANARUDI KIMWILI AU KIROHO. wAKATI WA UCHAGUZI WANAPITISHA KHANGA , KOFIA NA TISHET na TAKRIMA YA SHILINGI ELFU TANO KILA MPIGA KURA KAMA ILIVYOKUWA 2010.
 
We nawe hutabiriki utafikiri umeme wa tanesko bana mara kibao unakosoa sana wapinzani halafu leo unaleta mahaba ya ki Tanga kuwa na msimamo mpwa wangu

Sijakuelewa mkuu , hebu fafanua
 
Nakumbuka:: Chonya of Chilonwa me!!
mkuu umenipeleka mbali sana.
ONGEZEA
i am taking this girl to hospital,if police come tell him chonya of chilonwa me.mitoto ya siku hizi haina uwezo wa kukumbuka maneno kama haya labda uwaulize beti ya wimbo wa ali kiba,diamond et al
 
We nawe hutabiriki utafikiri umeme wa tanesko bana mara kibao unakosoa sana wapinzani halafu leo unaleta mahaba ya ki Tanga kuwa na msimamo mpwa wangu

Mkuu mimi sijawahi kujiunga na chama zaidi ya CCM ila msimamo wangu siku zote ni kwenye haki. Wapinzani wakifanya vizuri nawpongeza wakiboronga nawasema. Na CCM pia ni hivyohivyo. Hii nchi ni yetu si ya vyama. Wanasisa watutendee haki nasi tutwaunga mkono, kama sivyo tunawamwaga na ndivyo tunavyotemea kufanya 2015
 
Mbunge wao wakati wa uchaguzi unamkuta anapiga pombe inautwa CHOYA na wananchi wake , baada ya hapo wanampa kura bila matatizo.

acha waonje joto ya jiwe kwanza ili 2015 vichwa vifunguke!!!
 
acha waonje joto ya jiwe kwanza ili 2015 vichwa vifunguke!!!

afadhari ingekuwa joto ya jiwe jioni ingekwisha, hii ni jehanamu. Wakati wa masika akina mama ambao wanaishi mahama wanapotaka kujifungua hapo ndo kazi, kwani Zahanati tena nzuri kabisa ipo Nzali . Hapo sasa ndo kuna kazi,labda uende Chamwino ikulu. Wa Nzali kabla ya masika lazima uwe umejiandaa na bidhaa ya kutosha masika yakianza hata mvua ndogo tu basi kazi kwako itakuwa imekula kwako.
 
Back
Top Bottom