Hatuna haki ya kujibu ila Mungu wa Mbinguni anaona yote.

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,670
22,261
Rais amesema (kama ni kweli) kuwa wapinzani wakifanya mikutano huvunja magari ya watu kwa mawe! Rais akisema basi ndivyo ilivyo, jambo la kujiuliza ni magari yote ni ya wanaccm tu au wanavunja na magari yao? Pili wapinzani kwani wanaishi kwenye kambi tofauti na wanaccm? Mbona mitaani huwa kuko shwari hakuna malalamiko ya uharibifu wowote, au tunarudia ile kauli ya Mkapa (mwendazake) baada ya uchaguzi mdogo Temeke kuwa maduka yalichomwa moto na mwisho wa siku akadai hakurekodiwa vizuri! Rais anapojitenga na wananchi ambao ni wa vyama vingingine inakuwa si vyema kwa taifa, pia mgongano wa kisiasa uliopo kati ya viongozi wa vyama si vyema wakageuziwa wafuasi wa upinzani kuwa ni wakorofi, siwezi kuamini kuwa mashehe, mapadri, mababa na wamama wa upinzani wanatembea na mawe kushambulia magari ya wanaccm, haiwezekani, wapinzani si watu wa hovyo kiasi hicho na kushabikia upinzani si utovu wa nidhamu ila ni hulka ya binaadamu kama ilivyo kwenye dini. Watanzania wote tunaishi pamoja pamoja na kuzijua tofauti zetu na hata tukitoka kwenye mikutano yetu inayotofautiana tunaingia nyumba moja bila kutoana ngeu.
 
Back
Top Bottom