Hatuna haja ya kuleta wataalamu kutoka Misri kujifunza umwagiliaji

unauhakika na hiki ulichogandamizia RED?

Vipi lower moshi irrigation scheme?
Vipi dakawa irrigation scheme?

Kapunga?
Kilosa?
name them.........................
Mara ya mwisho umefika lini lower Moshi. Halafu kwa taarifa yako Lower Moshi ilikuwa ni msaada wa Japan ndio maana walimaliza. Lakini sasa ukifika lower Moshi ni jalala

Sent using Jamii Forums mobile app
 
True, tunaota mchana kweupe
 
Mkuu, tatizo letu kuwa ni kuwa hakuna government initiatives na lack of vision!!

Hivi kweli kati ya viwanda na kilimo kipi kilitakiwa kiwe kipaumbele chetu kwanza!!? Nchi ya 70 % wakulima, over 80 % elimu ya msingi ........... Seriously!!?
Tulishafanya kilimo kwanza kwa miaka 10,ni wakati sasa wa kuchakata mazao ya kilimo viwanda
 
Tatizo sio pesa wala utaalamu, tatizo ni uvivu, hao wamisri unafikiri kila kitu wanafanyiwa na serikali, huko lazima ujitume lasivyo utakufa njaa, hakuna biashara ya kupigana mizinga mchana kutwa. Watu wao wanajituma. Chukua mfano mwanza, unakuta mtu anaishi pembeni ya ziwa halafu anakwambia ana njaa. hata akitumia kopo kumwagilia anaweza kupata chakula lakini unamkuta anashinda chini ya mti kula miwa tu.
 
Mkuu, tatizo letu kuwa ni kuwa hakuna government initiatives na lack of vision!!

Hivi kweli kati ya viwanda na kilimo kipi kilitakiwa kiwe kipaumbele chetu kwanza!!? Nchi ya 70 % wakulima, over 80 % elimu ya msingi ........... Seriously!!?
70% wakulima ilikua enzi za nyerere, sasa 70% wamekua solar panel, mchana kutwa wamekaa vijiweni wanaota jua.
 
Mbowe amejaribu wameharibu miundombinu.Kama kujifunza wangeenda hata kwenye Mashamba ya Mbowe badala ya kuyaharibu
nitumie namba ya mbowe niwasiliane nae sie huku tunahitaji kweli huo mradi tutampa shamba bure na vijana wakumsaidia wapo tele,
 
unauhakika na hiki ulichogandamizia RED?

Vipi lower moshi irrigation scheme?
Vipi dakawa irrigation scheme?

Kapunga?
Kilosa?
name them.........................
Najua ninachosema:
Lower Moshi - 1930 (British - wakoloni) mpk leo haujakamilika
Dakawa -1981 (North Korea) mpk leo haujakamilika
Kapunga - initiated 1983, started 1988 mpk leo haujakamilika
Kilosa hata usiongelee, naijua nje ndani hakuna mradi wa maana, sio mvumi irrigation scheme, wala Idodi or mention whatever!
Hakuna mradi ambao serikali imejenga ukaisha, full stop
 
Eti wataalam wetu wanasema hawapewi pesa.Kukusanya vijana 100 wakachimba mtaro,wakafanya kazi kwenye shamba husika la mpunga wakalipwa kutokana na mavuno nako kunahitaji pesa gani?halafu mtu anajiita msomi

Tatizo linaanzia juu mpaka chini. Viongozi wa kisiasa Hawajui nchi ina nini na watu wenye ujuzi au uwezo gani na vinaweza kutumika vipi.
Vivyo hivyo wasomi H awajui watumie vipi usomi wao, na mara nyingi wanafikiri kazi yao ni kuratibu miradi inayobuniwa na kufanywa na wageni.
 
Sasa sijui tunahitaji nini, maana kila Juhudi ifanywayo inabezwa.
Heri kenda shika kuliko kumi nenda rudi.
Tujiongeze.
 
70% wakulima ilikua enzi za nyerere, sasa 70% wamekua solar panel, mchana kutwa wamekaa vijiweni wanaota jua.
weacha tu vijana wote wanendesha bodaboda na vibanda vya kunyoa nywele, huu mradi wa rea umeme unatumiaka kuchaji simu na kuchoma nyimbo kwenye memory card, wanaolima ni vibibi tu huko vijijini,
 
Serikali inapiga porojo, wanasiasa wanapiga porojo za umwagiliaji wakati hawaujui!Wao ndio waende China, Japana, Israel na Egypt wakajifunze namna wenzao wanavyowekeza pesa za kutosha kwenye miundombinu ya umwagiliaji
 
Sasa sijui tunahitaji nini, maana kila Juhudi ifanywayo inabezwa.
Heri kenda shika kuliko kumi nenda rudi.
Tujiongeze.
Utakuwa hujaelewa nilichoandika, sual la kubeza halipo hapo hili ni suala la maslahi mapana ya wananchi maskini
 
kwahiyo SUA wameshindwa kuzalisha wataalamu hadi tuagize misri?
 
Hayo unayosemankuhusu Kilosa, yote kweli tupu. Hamna kitu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
weacha tu vijana wote wanendesha bodaboda na vibanda vya kunyoa nywele, huu mradi wa rea umeme unatumiaka kuchaji simu na kuchoma nyimbo kwenye memory card, wanaolima ni vibibi tu huko vijijini,
Ipo siku hao watakosa chakula cha kununua ndipo tutakapoona mchele wa plastiki una maana
 
Eti wataalam wetu wanasema hawapewi pesa.Kukusanya vijana 100 wakachimba mtaro,wakafanya kazi kwenye shamba husika la mpunga wakalipwa kutokana na mavuno nako kunahitaji pesa gani?halafu mtu anajiita msomi

mkuu huyo mleta mada ni mtaalamu koko asiye na mbinu mbadala.Kila siku ni kupiga yowe pewsa serikali itoe pesa!!!! Huyu mleta mada na wenzie waliosoma ambao elimu zao haziwezi buni mbinu mbadala za kutatua changamoto za kilimo cha umwagiliaji AANGALIE huyu mwenzie wa India AMBAYE mjadala wake tuliweka humu ambaye kafanya maajabu wakati hajawahi soma kilimo na anasifika dunia nzima

Habari nzima hii ya huyo mhindi ilivyojadiliwa Jamii forums hii hapa chini
Rais Magufuli akatembelea kijiji cha Hiware Bazar kilichoko India
 
Eti wataalam wetu wanasema hawapewi pesa.Kukusanya vijana 100 wakachimba mtaro,wakafanya kazi kwenye shamba husika la mpunga wakalipwa kutokana na mavuno nako kunahitaji pesa gani?halafu mtu anajiita msomi
Umwagiliaji ungekuwa kuchimba hiyo mitaro kama ya barabara, basi kuna haja gani ya kwenda Egypt??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…