Hatulali njaa. Tunachelewa tu kula.

Mkuu story yako imenikumbusha mbali sana zama za udogo wangu ila bado kumbukumbu ile ingalimo kichwani mwangu.
Nakumbuka jinsi baba yangu alivyokuwa anaenda resi ili maisha yaende nyumbani.
Nakumbuka mara nyingi tu giza limeshaingia na jiko limenuna tupo tumetulia mimi na MAMA tunamsubiria mzee arudi ili mkono uende kinywani.
Lakini mzee yule hakuna siku aliyotuangusha,kama ulivyosema hapo juu "tulichelewa kula tu ila hakuna siku tuliyolala njaa"...
MUNGU akurehemu BABA yangu mpendwa.Ni miezi kumi na tano sasa imepita tangu ulivyoondoka kwenye maisha yetu ilabado unasimama kama shujaa wetu mimi na Mama yangu.
Kama ntahitaji kuwa na Baba kwenye maisha mengine baada ya haya hakika ntakuomba tena wewe ukubali kuwa BABA yangu.
NAJIFAHARISHA SANA NA WEWE.
Pumzika kwa amani MPENDWA.
 
Huyo mama angekuwa ni hawa wanawake wa kidoticom...wanawake wa social network... Sjui ingekuwaje tu....I can imagine
 
Hata sisi hatukuwahi lala na njaa ila tunachelewa kula, baba hayupo mama yupo hana kazi yeyote anategemea wapangaji kodi ya elfu tatu kwa mwezi na wapangaji hawana hela hata miezi miwili,
 
Dah mkuu unanikumbusha mbali sana mama nakumbuka kipindi hicho kijijini hali ngumu akawa anachuma majani ya vitunguu anaweka chumvi tunakula ugali lakini kuna kipindi pesa hakuna linachukuliwa limao maji yake inachanganywa na maji na ugali maisha yanaenda atimae tumekua maisha yanaendelea
 
Ukikumbuka ulipotoka, utakuwa na heshima huendako.
 
Pigania future.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…