mshukuru Mama kwa kuwa alikuwa mvumilivu unless otherwise ungekuwa unaongea nao desperately mshua angekuwa kwake the same as Mama.Last week end nilipata nafasi ya kuongea na Wazazi wangu. Kama ilivyokawaida, huwa napenda kumpigia simu Mama, nikishakaliza kuongea nae basi umuomba ampe na Baba ili tuongee pia.
Kwavile huwa naongea nao mara kwa mara, safari nikaamua kutaka kujua maisha yao enzi za ujana( nilipenda kusimuliwa na Mama kuliko Baba katika ili). Wakati ananiambia mambo kadhaa ya kipindi hicho, akanigusia na jambo ambalo hawakuwahi kulizungumzia hapo kabla (sikuwa nalifahamu sababu ya umri mdogo wa kipindi hicho).
Kuna kipindi mshua uchumi uliyumba zaidi ya sana, kiasi kwamba mlo wa siku ikawa shida, maana familia ina watu 9 ( watoto tukiwa 7). Mama anasema kuna hiyo wiki ambayo hatoweza kuisahau, maana kuna siku chakula ilikuwa ugali ila mboga ni maji ya uvuguvugu yaliyowekwa chumvi. Kwake angeweza kuvumilia, ila kwa watoto wake roho ilimuuma hasa sisi wawili wa mwisho tuliokuwa wadogo. Ndani ya hiyo hiyo wiki, kuna siku ambazo tungeweza kuamshwa usiku sana ili tule ( maana muda huo ndio mzee anakuwa amerudi na chakula)
Haya kwangu yalikuwa mapya. Ikabidi nimpe pole,maana mimi na dogo kumbukumbu hiyo hatunayo,ila wao iliwaumiza na bado wanayo. Akaitikia,kisha akasema kwamba sasa imebaki kuwa historia tu..Tukamaliza kuongea, akampa simu Baba.
Baada ya salamu na mazungumzo ya hapa na pale, nikamuingizia kuhusu mazungumzo yangu na Mama, kisha nikampa pole (kama nilivyofanya kwa Mama). Hakujisumbua kuitikia, isipokuwa aliniambia "Muda huu Mama yako yupo anapika, ila sehemu nyingine kuna watu ndio wanatoka vibaruani au pengine ndio wanaenda, hapa kwetu muda wa kulala ukifika, upande mwingine kuna watu ndio wanakoka moto wapike, na pengine tukiwa usingizini, wao ndio watakuwa wanakula"
Sikumuelewa anamaanisha nini. Ila akaendelea " Hatujawahi kulala na njaa mwanangu, ila tulikuwa tunachelewa tu kula". Ukimya ukapita kidogo, baadae tukaagana.
*** *** *** *** *** ***
Wakuu napenda niwaambie kitu kimoja. Katika msoto uliopo,don't quit. Sio kwamba hautofika, ni kwamba umechelewa tu, sio kwamba umekataliwa, ni kwamba jibu lako linacheleweshwa tu (atatiki endelea kukomaa nae [emoji28][emoji28][emoji28]).
All in all ,usikubali kukwamia njiani wakati unajua fika safari yako bado inaendelea.
Learn to see positivity,even in a negative situation.
Hatulali njaa,tunachelewa tu kula.
Analyse.
Last week end nilipata nafasi ya kuongea na Wazazi wangu. Kama ilivyokawaida, huwa napenda kumpigia simu Mama, nikishakaliza kuongea nae basi umuomba ampe na Baba ili tuongee pia.