Miaka ya nyuma tulijitahidi sana kuwa waaminifu kwenye chama chetu. Na lengo la uaminifu wetu ni kukifanya chama kiendelee kuwa madarakani, kwakuwa viongozi wetu walikuwa wazalendo sana hatukupata shida kuteua na kuwanadi walikuwa waadilifu na waaminifu 100%. Hawakuwaza uchaguzi wa miaka 10 ijayo. Waliwaza kututumikia.
Sasa hv tuna wakati mgumu, kwenye vikao vyetu vya uteuzi kila jina jina tunapoletewa lina dosari hii au ile. Au kama siyo dosari basi ni wa kambi ile. Tunapata wakati mgumu.
Kinachoumiza zaidi Sasa hivi watu wanaounga juhudi zetu kutoka upande wa pili, yaani wa upinzani, wanaotusema sana, wanaotuchambua sana, wanaotutukana sana majukwaani. Wakija tu, wanapata teuzi.
Nabaki na maswali ni lipi jema wamekifanyia chama chetu zaidi ya kutunanga, kutuharibia mahusiano yetu na wapiga kura, kutuvuruga, kuwafanya viongozi wetu waonekane hawafai mbele ya jamii.
Pia najiuliza hivi wamekitumikia chama kuliko sisi? Uanachama wenyewe wa chama chetu wameupata lini? Kadi yao ina umri gani? Kwa hiyo wafia chama tunateseka bure? Au wote hatujasoma?
Hata kwenye ndoa haiwezekani mke atafute na mmewe miaka 10, baada ya kufungua duka kubwa la Hardware halafu bi mdogo aje akae dukani atanue mbawa zake no!
Mwaka huu na miaka ijayo hatukubali akina nanihii waliounga kwa mfano kama wa Msigwa waliotutukana sana, kutunanga sana, mara CCM hivi mara vile, walambe uteuzi na ss tupo tu tunang'aa macho.
Ikitokea hivyo tutaamua jambo letu. Kama kuitwa wasaliti poa tu. Tumechoka! Wao akina nani na sisi akina nani! Tuhangaike na chama, tutukanwe, watuchore kwamba wanaohangaika na chama ubongo wetu ukapimwe halafu hao hao eti wakiunga juhudi tuanze kuwaita Mheshimiwa kwenye chama tulichopambania. Sikubali, Sikubali, Sikubali.
Imetosha!