Hatuhitaji katiba mpya ya CCM! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatuhitaji katiba mpya ya CCM!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Izack Mwanahapa, Nov 18, 2011.

 1. Izack Mwanahapa

  Izack Mwanahapa JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 497
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Tanzania ya leo inahitaji katiba ya nchi iliyotokana na mapendekezo ya wananchi ili ipate uhalali (Legitimacy) ya kuheshimiwa. Mjadala wa muswada wa katiba unaoendelea sasa umekuwa ukipingwa na baadhi ya wanasiasa, Wanaharakati, Mabaraza ya katiba, Majaji na wananchi kwa ujumla. Kwa hali hii tayari katiba inayotarajiwa itakosa uhalali kutoka kwa wananchi kwani watu wanaoendelea kuujadili na wanaotarajiwa kuupitisha mswada huo ni walewale walioandika katiba zenye viraka zinazotuburuza mpaka leo yaani "watu wale wale mawazo yaleyale katika suti mpya"

  Kimsingi hatutaki mabadiliko ya rangi au kurasa za katiba tunahitaji mabadiliko chanya ya Content ya katiba.
   
Loading...