Hatua za kufuata katika upimaji Kiwanja/shamba

Dr.

JF-Expert Member
Jan 2, 2014
217
193
1.UKAGUZI WA KIWANJA/SHAMBA

a) Kuchukua alama (Coordinates) za eneo husika kwa kutumia kifaa maalum kiitwacho GPS (Global Positioning System).

b) Alama (Coordinates) za kiwanja zikishachukuliwa hupelekwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi au Halimashauri husika katika idara ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kwa ajili ya kupatiwa Mchoro wa Mipanngo Miji wa eneo huaika.

c) Kwa kutumia mchoro wa Mipango Miji utabaini eneo unalotaka kupima limepangiwa Matumizi gani. Linaweza kua limepangwa kwa ajili ya Makazi, Viwanda, Biashara, Huduma za jamii, Hifadhi au eneo hatarishi, hivyo sasa ni muhimu kujua.

2. KIBALI CHA UPIMAJI

Mmiliki halali wa eneo husika ataandika barua Halmashauri husika akiambatanisha vithibitisho kua eneo ni lake ili apatiwe kibali cha Upimaji.

3. UPIMAJI

a) Kama eneo halina Mchoro wa Mipango Miji (TP- Drawing), Mchoro huandaliwa kwanza kwani upimaji hauwezi kufanyika bila kuwepo Mchoro wa Mipango Miji.

b) Kama eneo lina Mchoro wa Mipango Miji Upimaji huanza mara moja na Mpima (Land Surveyor) kwa kushirikiana na Mtaalam wa Mipango Miji (Town Planner) Kwa kutumia vifaa Maalum kama Total Station au RTK.

c) Baada ya uupimaji kukamilika na Mawe (Bicons) kupandwa kwenye kiwanja husika faili huandaliwa na Kupelekwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi kwa ajili ya ukaguzi na kisha kurudishwa kwa Mteja kwa ajili ya kufuatilia hati (Tittle deed)

Kwa Maswali, Maoni au Ushauri tuwasiliane kupitia

gislandsolution@gmail.com
 
Kama eneo halina mchoro unasema mchoro huandaliwa. Sentensi hii inaonyesha kuna changamoto sana kupima shamba kwa sisi ambao mashamba yetu yako vijijini ndani ndani, siyo?
 
1465570730276.jpg

Unaweza ukapitia hii
 
Back
Top Bottom