Hatua za kuchukua unapoibiwa simu yako

Hatua za kuchukua unapoibiwa simu yako

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Kama una tabia ya kununua simu
zilizotumika kutoka kwa watu au
zile mpya barabarani na sio kwenye
maduka, unashauriwa kuacha tabia
hiyo mara moja kwa sababu
inaweza kukuleta shida siku moja .
Kumekuwa na matukio mengi ya
watu kuibiwa simu zao za mikononi
na vifaa vingine vya mawasiliano
ambavyo ni rahisi kufanyia uhalifu.
Watu wengi hawajui wafanye nini
wanapoibiwa simu, wanaamua
kusamehe na kununua simu na laini
mpya.
Kuna masuala kadhaa yanayoweza
kutokea kutokana na simu kupotea
au kuibiwa. Na mambo haya
yanaweza kumfikisha mwenye simu
au kifaa husika katika vyombo vya
sheria na hata kufungwa
ikithibitika .
Niwape mfano. Jamaa mmoja
alikuwa na tabia ya kununua simu
kutoka kwa watu na kuziuza kwa
wengine. Siku moja akaletewa simu
akainunua na kumuuzia mtu
mwingine. Mnunuzi huyu
akakamatwa kwa kukutwa na simu
ya wizi, akamleta askari kwa jamaa
mwenye tabia ya kununua simu.
Alivyopelekwa polisi akaambiwa
kuna mtu aliibiwa simu na kukatwa
mapanga. Simu iliyoibiwa
imepatikana kwa fulani ambaye
ameinunua kwako, tunakutuhumu
kwa kumkata mtu mapanga na
kuiba simu yake. Hili ni tukio moja
tu ila kuna mengine kama haya.
Mtu anaweza kuibiwa simu eneo
moja halafu simu hiyo ikatumika
kufanya mawasiliano kati ya
majambazi kwa ajili ya kufanya
tukio la uhalifu. Wakishamaliza
simu wataiacha sehemu ya tukio ili
kupoteza ushahidi.
Jeshi la polisi likianza uchunguzi
katika kutafuta ushahidi wa
mwanzo, mmiliki wa simu atakuwa
mtuhumiwa wa kwanza hata kama
hahusiki kwa ndewe wala sikio.
Hatua ya kwanza kuchukua
unapoibiwa simu au kifaa cha
mawasiliano ni kutoa taarifa kwa
mtoa huduma wako kama ni
Vodacom, Airtel, Tigo au mtandao
mwingine wa simu.
Mtoa huduma wako anaweza
kuifunga namba ya simu isitumike
mpaka utakapokamilisha taratibu
nyingine.
Wajulishe rafiki zako na jamaa zako
wengine wa karibu, ili wajue
kinachoendelea. Wengine wanapoiba
simu wanaweza kutumia dhidi ya
rafiki zako au ndugu zako wa
karibu. Ukiwafahamisha watajua cha
kufanya endapo lolote litatokea.
Katika hatua ya kwanza unatakiwa
uhakikishe kweli hiyo ni simu ni
yako na una vielelezo vyote kuhusu
simu husika na namba yake kwa
sababu mtoa huduma atauliza vyote
hivi. Kama ulinunua simu kwa mtu
na huna taarifa za kutosha inaweza
kuwa shida kwako pia.
Nenda kituo cha polisi kilicho
karibu yako kwa ajili ya kutoa
taarifa na waambie umeshatoa
taarifa hiyo kwa mtoa huduma
wako. Hapa utapewa karatasi
maalumu kwa ajili ya kupeleka kwa
mtoa huduma wako kama
uthibitisho wa kupotea kwa simu na
laini yake.
Ukienda kwa mtoa huduma wako
kuna maswali utaulizwa ukifanikiwa
kuyajibu, basi utapatiwa namba
yako iliyopotea na utafanya usajili
wa namba hiyo upya. Cha kufanya
ukiwa hapo hapo ni kuthibitisha
taarifa mbalimbali kama kulikuwa
na fedha, majina ya usajili kama ni
yale yale na mengineyo.
Mtoa huduma wako kwa
kushirikiana na jeshi la polisi wana
uwezo wa kuitafuta simu yako na
kuipata, lakini kwa ushauri wangu
achane nayo kama iliibwa nenda
ukanunue nyingine.
Gharama ya kununua simu mpya ni
ndogo kuliko gharama utakazotumia
pindi utakaposhikwa kwa kununua
simu za wizi au simu ambazo
hazina viwango vya kutosha .


Chanzo: Mwananchi
 
nashukuru kwa kutupa darasa mkuu..tumekusikia
 
ok sawa..ingawa sikuhizi ni ngumu sana kuipata simu yako iliyoibwa...hata kama iphone wadau kariakoo wapo kikazi zaidi.!!
 
Hayo yote uliyoeleza hapo juu in sawa kabisa kama watendaji watataka kuwajibika ipasavyo mambo hayo yanapotokea.Ila hapa kwetu mambo hayako hivo mkuu. Kuna danadana nyingi sana toka kwa hao unaotegemea wakusaidie. Kuna jamaa yangu aliibiwa simu na akapeleleza kwa kutumia kampuni ya simu iliyokuwa inamhudumia na IMEI namba na akaweza kujua simu ilipo na akawashirikisha na polisi ili waweze kumkamata mwizi na simu yake irudi. Lakini hadi leo mwezi wa 4 sasa hakuna cha maana kinachoendelea mpaka ameamua kununua tu simu nyingine
 
Ni ngumu kuwakamata kwa sasa suluhisho ni kwa aplication za kutrack na kufunga simu ambapo unaweza kufanikiwa kwa kuipata kutumia IMEI namba ambayo umeiweka kwa simu na laini yako,tofauti ni kusahau watu wakiiba cha kwanza ni laini wanatupa halafu wanaflash hapo detail na kila kitu ambacho kilitunzwa kinafutwa inabaki kana ilivyonunuliwa dukani na siku hizi zinarudishwa dukani inawekwa kwenye boksi tayari ni simu mpya.

Cha muhimu ni kuhimiza usajili wa hizo aplication na labda pia usajili wa IMEI za simu sababu leo laini iko kwenye simu hii kesho ile mtandao utajua ni simu ipi ya kwako?.Pia bado sheria yetu haitumiu sana ushahidi wa kielectroniki kwa vile ni rahisi kutengeneza
 
Back
Top Bottom