Hatua tuliyofikia si ya kubezwa

kalulukalunde

JF-Expert Member
May 27, 2016
1,056
1,083
SERIKALI imetoa kibali cha kuajiri walimu 4,129 wa masomo ya sayansi na hisabati katika shule za sekondari nchini huku walimu 3,081 wakiwa tayari wameshaajiriwa na wanatakiwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kuanzia Aprili 18 hadi 25, mwaka huu.

Hii ni habari njema kwa wahitimu wetu, iliyochukua nafasi kubwa katika magazeti, redio, televisheni na mitandao mbalimbali ya kijamii jana kutokana na ukweli kwamba, Tanzania ya sasa ina vyuo vya kutosha vinavyozalisha vijana wengi kila mwaka. Kuwa na vyuo vya kutosha katika nchi ni ishara njema kwa kuwa taifa letu.

Nikumbushe tu kwamba wakati fulani enzi za ‘Mwalimu’, Watanzania tuliambiwa adui wakubwa kwetu ni watatu; ujinga, umasikini na maradhi.

Maadui hao wa enzi za mwalimu, kama taifa tumewapiga vita kweli kweli, maana ni juzi tu kwenye adui maradhi, Serikali imeanza kutoa vifaa vya hospitali nchi nzima, ikiwa ni pamoja na vitanda vya hospitali, vitanda vya kujifungulia wajawazito, magodoro na shuka.

Akizindua usambazaji huo juzi wilayani Kongwa katika Mkoa wa Dodoma, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema serikali imetekeleza ahadi iliyotoa kwa wananchi ambapo inawekeza katika afya ya wananchi hivyo kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa uchumi wa viwanda.

Akizungumza kwenye hadhara ya wananchi wa Wilaya ya Kongwa, Ummy alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa kwa baadhi ya maeneo ikiwemo ya upatikanaji wa dawa ambapo bajeti ya dawa imeongezeka kutoka Sh bilioni 31 mwaka 2015/16 hadi Sh bilioni 251 mwaka 2016/17.

Pia alisema kutokana na ahadi ya Rais John Magufuli ya kununua na kusambaza vitanda kwenye vituo vya umma, wizara yake kwa bajeti ya mwaka 2016/17 ilitenga kiasi cha Sh bilioni nne za kuwezesha kununua pamoja na kusambaza vifaa hivyo kwa halmashauri 184 nchini.

Vifaa vya hospitali vitakavyosambazwa kwenye halmashauri zote 184 nchini ni vitanda vya hospitalini 3,680; vitanda vya kujifungulia wajawazito 920; magodoro 4,600; na mashuka 9,200.

Thamani ya vifaa hivyo ikiwa ni Sh 2,933, 125,600 na kwamba kazi ya kugawa vifaa hivyo itakamilika kabla ya Juni 30, mwaka huu. Huo ni upande wa adui maradhi.

Kwa upande wa adui ujinga kama nilivyodokeza hapo juu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene alisema wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari kuwa bado kuna nafasi 1,048 ambazo wanaendelea kupokea maombi ya walimu wa masomo hayo.

Tuwaombe tu vijana wetu, kulalamika vijiweni hakufai, chukua hatua nafasi ndiyo hiyo! Adui ambaye anaendelea kutafutiwa dawa kwa nguvu zote kwa kuwa hawa wawili wanampa kiburi, ni umasikini. Nasema wanampa kiburi kwa kuwa kama hakuna ajira, maana yake, wasomi wanakosa kazi, wanakuwa masikini.

Lakini, kama taifa halina hospitali za kutosha na dawa kwa wagonjwa, maana yake watu wake watakuwa dhaifu, hawatakuwa uwezo wa kuzalisha, hivyo umasikini ni lazima uwanyemelee, ukiondoa hawa wawili, ujinga na maradhi, ni lazima umasikini utapungua na mwisho utaisha kabisa.

Watanzania wenye nia njema, ni lazima tumuunge mkono Rais wetu Dk Magufuli ambaye anaona mbali kwa kulitaka taifa hili liwe la viwanda.

Ni lazima tubadilishe fikra zetu hasi kuwa chanya, kwa kuwa viwanda vitazalisha ajira, vitatengeneza dawa za kutosha, hivyo tutaimarisha afya zetu kwa kuwa dawa za kuagiza nje ya nchi ni ghali.

Hospitali zikiwa na dawa na wataalamu wa kutosha, hakuna haja ya kupeleka wagonjwa nje ya nchi. Yote haya yanawezekana kwa Tanzania ya viwanda.

Tutakuwa tumeokoa fedha nyingi za kigeni ambazo zingetumika kugharimia watu kwenda nje. Tutaondokana na ujinga, maradhi na umasikini kwa mtindo rahisi zaidi. Mungu ibariki Tanzania, ibari Afrika na mbariki Rais wetu, Dk John Magufuli.
 
Kweli kabisa
 
Back
Top Bottom