The Consult
JF-Expert Member
- Jan 20, 2017
- 220
- 252
Wafadhili wengi (donors) hutakiwa kwa mujibu wa sheria zao ndogo ndogo (by laws) na maamuzi ya vikao vya bodi; kutoa kiasi cha fedha kila mwaka kwa ajili ya ufadhili wa miradi ya maendeleo. Hivyo basi kuwa na programu/mradi mzuri huwasaidia wafadhili katika kutimiza majukumu yao na hatimaye kufikia malengo yao. Programu au mradi mzuri na wenye ushawishi hutokana na andiko zuri, kuwa na andiko zuri ni sharti ufuate hatua stahiki ambazo ni;
- Kumfahamu mfadhili (Know about the donor), kila mfadhili ana taratibu na kanuni zake katika utoaji wa ruzuku, kuzifahamu taratibu hizi ni hatua ya msingi katika kupata ruzuku na kinyume chake hupelekea programu au mradi wako kushindwa katika hatua za mwanzo. Katika hatua ya kumfahamu mfadhili; ni vyema ukajiuliza maswali yafuatayo; Je ni vipi vipaumbele vya mfadhili? Je maslahi ya mfadhili yanaendana na shughuli ninazofanya/zinazofanywa na taasisi yangu? Maombi yanapaswa kutumwa kwa njia ipi na mwisho wa utumaji ni lini?
- Maandalizi kabla ya uandaaji wa andiko (Prepare to present your work), uombaji wa ruzuku; ni zaidi ya uwasilishaji wa andiko (proposal); hivyo kabla ya kuandaa andiko ni vyema mifumo ya kiutawala na kifedha ya taasisi yako ikawa katika mpangilio mzuri na unaofaa. Katika kuhakikisha mpangilio mzuri ndani ya taasisi, ni vyema ukajiuliza maswali yafuatayo; Je lengo, mipango na dira ya taasisi yako iko vizuri? Je una watu/wafanyakazi wenye sifa stahiki katika utekelezaji wa mradi?
- Hakikisha lengo la mradi wako linaendana na madhumuni ya taasisi yako (organization's mission), hakikisha kwamba mradi unaoenda kuutekeleza unakuwa ni sehemu katika mpango mkakati wa taasisi yako (organization strategic plan). Mara nyingi mfadhili anapofanyia tathmini andiko la mradi huangalia ni kwa namna gani mradi husika utaenda kutatua tatizo la jamii ambalo ndio lengo la taasisi husika.
- Uandikaji wa andiko la mradi (proposal write up) kuna miundo (formats) mingi katika uandaaji wa maandiko ya miradi, utofauti wa muundo hutokana na matakwa ya mfadhili, aina ya mradi n.k. Katika uandaaji wa andiko ni vyema ukajiuliza maswali yafuatayo; Je ni kipi unataka kutimiza (achieve) kupitia mradi husika? Je ni njia zipi (strategies/methodologies) zitatumika katika utekelezaji wa mradi? Je ni akina nani watahusika katika utekelezaji wa mradi na majukumu yao ni yapi? Je ni akina nani watakuwa wafaidika(beneficieries) wa mradi husika na watatambuliwaje? Je shughuli za mradi zitafanyika eneo gani, zitaanza lini na kumalizika lini? Andiko la mradi hujumuisha; Taarifa za mawasiliano ya watekelezaji wa mradi (contact information), ufupisho wa mradi (executive summary), umuhimu wa mradi (problem rationale/problem justification), maelezo ya mradi (project description), taarifa fupi ya taasisisi (organization description), bajeti (budget) na taarifa zingine.
- Uandaaji wa bajeti ya mradi, bajeti ni makisio (estimates) ya gharama katika utekelezaji wa shughuli za mradi husika. Bajeti ya mradi humsaidia mfadhili kujua ni kwa namna na kiasi gani fedha zitatumika katika mradi husika. Kuna aina mbili za bajeti katika utekelezaji wa mradi ambazo ni; bajeti ya utawala (administaration budget) ambayo hujumuisha ;mishahara, gharama za pango, umeme, usafiri n.k Pia aina ya pili ya bajeti ni bajeti ya mradi (project activities budget) hii hujumuisha gharama zote zitokanazo na utekelezaji wa shuhuli za mradi kama vile mafunzo n.k
The Consult: +255 719 518 367
Dar es Salaam
Tanzania