Hatma ya Mrema mikononi mwa Magufuli..........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,468
911,173
Hatma ya Mrema mikononi mwa Magufuli


Na John Daniel

HATMA ya Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Bw. Eprahim Mrema, sasa ipo mkononi mwa Waziri wa Ujenzi, Bw. John Magufuli huku kukiwa na matumaini
makubwa kuwa atatangaza uamuzi huo leo.

Habari za kutoka ndani ya wizara hiyo zilieleza jana kuwa tayari Bw. Magufuli amefanya maamuzi mazito juu ya mtendaji huyo na kwamba atawasilisha mapendekezo yake kwa Rais Jakaya Kikwete leo kabla ya kuwekwa hadharani.

"Juzi (Jumatatu) kulikuwa na juhudi kubwa za Bw. Mrema kutaka kuonana na Waziri Magufuli ili wazungumze zaidi lakini alikataa, akisema anachotaka kwanza ni taarifa za utendaji na majibu ya tuhuma mbalimbali.

"Baada ya kupata majibu aliyotaka amefikia maamuzi mazito sana lakini anataka kwanza kuwasiliana na ikulu kuhusu maamuzi hayo kabla ya kuwekwa hadharani," kilisema chanzo chetu.

Majira ilipomtafuta Bw. Mrema ofisini kwake ilikataliwa kufanya naye mahojiano kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utaratibu aliojiwekea wa kujibu maswali ya wana-habari kwa njia ya maandishi na si kuonana nao.

Katibu Mukhtasi wa Bw. Mrema alimtaka mwandishi wetu kuonana na Ofisa Mahusiano wa TANROADS, Bi. Aisha Malima ambaye alimwelekeza kuandika na kuacha maswali ili apelekewe Bw. Mrema.

"Wewe niandikie tu hayo maswali hapa nimpelekee bosi atayajibu ndio utaratibu wake, nakuomba sana unisamehe tu hata kama unamwona, labda akiamua yeye," alisema Bi. Malima.

Baada ya Majira kuandika maswali hayo ofisa habari huyo aliomba ufuatiliaji wa majibu kufanyika leo kwa kuwa kwa kawaida hutoa majibu si zaidi ya siku tatu.

Majira ilipomtafuta Waziri Magufuli ili kupata ufafanuzi hakupatikana kutokana na kuwa na kikao mfululizo, na baadaye kuondoka kwenda kukabidhi wizara aliyokuwa akiongoza.

Waziri Magufuli alielekeza Majira kufanya mawasiliano na Ofisi ya Habari katika jengo la Wizara ya Uchukuzi.

Hata hivyo wahusika wa ofisi hiyo walirusha mpira kwa Bw. Magufuli kwa maelezo kuwa suala hilo ni zito, hawawezi kuzungumza.
 
Ivi iyo post si ni presidential appointee?
Kama Magufuli nae atakuwa kapendekeza am sure kitakuwa kichwa tuu bse hawezi pendekeza Kanyanga
 
Back
Top Bottom