Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 427
- 666
Mahakama Kuu ya Tanzania leo inatarajiwa kuanza kusikiliza kesi ya kupinga kuenguliwa kwa mgombea urais wa ACT-Wazalendo, Luhaga Mpina, hatua ambayo inaweza kubadili mwelekeo wa uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Kwa mujibu wa mawakili wa chama hicho, mahakama leo itasikiliza hoja za awali zenye lengo la kuamua kama zuio hilo lilikuwa la kisheria, ama ni uamuzi wa kiutendaji uliopita mipaka ya kikatiba.
Source: BBC
======================
Chama cha ACT Wazalendo leo kimewasilisha kesi rasmi Mahakamani kupinga uamuzi wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) wa kumzuia mgombea wao Luhaga Mpina, kurejesha fomu za uteuzi wake kwa mujibu wa sheria.
Kesi hiyo imefunguliwa Mahakama Kuu (Masijala Kuu Dodoma) na Bodi ya Wadhamini wa Chama na Luhaga Joelson Mpina mwenyewe dhidi ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu imepewa nambari 21692 ya Mwaka 2025, ambapo imepangwa kusikilizwa kesho mbele ya Majaji watatu ambao ni Longopa J, Kahyoza J na Kagomba J kwa kuanza kusikilizwa kwa amri muhimu za awali kwa njia ya mtandao.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ACT Wazalendo wanaona uamuzi wa INEC ni kinyume na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Sheria za Uchaguzi na misingi ya haki za msingi za kiraia na kisiasa. Kwani Haki ya kugombea na kuchagua viongozi ni haki ya kikatiba isiyopaswa kunyimwa kwa visingizio visivyo na msingi.
Hivyo imewafanya kuwasilisha ombi la amri ya dharura (interim orders) ili Mahakama isimamishe hatua hiyo waliyoita ni ya ''udhalimu'' na kuhakikisha haki za mgombea wao Mpina na wananchi wote wa wapiga kura wanaomuunga mkono zinalindwa.