Hatma ya maisha yangu ipo mikononi mwa kijana wa Buguruni

BONUS EPISODE

Hello Boys & Girls, members wa Jf, Mr X6 is back with full energy, this mwezi May has been really tough for me thanks to God I’m bounced back with the Grace

After this bounce back nimejifunza kitu, When your intentions are pure, you don't loose people, people loose you, na sio hicho tu nilichojifunza, nimejifunza mambo mengi sana kupitia hii story yangu, Pengine ningekuwa sijaandika hii story nisingepata nafasi ya kujifunza haya yote, Nikikaa chini na kupitia maandishi yangu naona kabisa sehemu nilizofanya mistake na sehemu nilizopatia

So after this Bonus Episode nitakuja na Summary ya mambo niliyojifunza kupitia hii story yangu, yani kila aliyehusika kwenye hii story yangu na kila niliyemtaja amenifundisha jambo kwenye maisha

Basi bhana kama nilivyosema hapo awali, mwezi huu wa tano nilipitia kipindi kigumu sana hadi kufikia hatua ya kutaka kupoteza watu wangu wa karibu ila kwasababu dhamira yangu haikuwa mbaya basi mimi nisingewapoteza wao bali wao ndio wangenipoteza Mimi

Basi wakaamua (Caryn) kunipoteza ili kubaki na mteja, Kiukweli iliniuma sana, na kilichoniuma sio kuwekwa Benchi na Kampuni bali ni kuwekwa Benchi kwa kosa ambalo nilijitahidi kulifukia despite all my best efforts lakini nayo ilionekana kazi bure

Nikamuambia Caryn "Unajua unaweza ukawa na mapenzi ya dhati kwa mtu lakini ukavunjwa moyo kwa vitendo unavyofanyiwa na huyo mtu"

Caryn: "Mimi najua nini nafanya, sometimes inabidi ucheze na akili za watu, and If you claim to love someone you don't stop loving them even when their decision is not in your favor"

Speaking of Claim to love someone, unajua Mwanamke anayekupenda atakuonesha signs zote ili umtongoze na hilo nililiona kwa Caryn, ili nisionekane Domo zege ikabidi nisipuuzie Green light iliyokuwa inanipiga usoni, nikachapa verses zangu lakini majibu ya Caryn Sasa naweza kusema hayakuwa mabaya na wala hayakuwa mazuri

Ilikuwa hivi, mnakumbuka ile siku tulienda kwa Michelle? nakumbuka hicho kipande nilikihadithia hapa, Sasa tulivyorudi nyumbani kwangu kutokana na maongezi tuliongea kule kwa Michelle ikabidi nijaribu kutupa ndoana ili nione kama itaibuka na Samaki, sikupindisha pindisha nilienda straight to the point

BM: "Caryn, nahisi upendo nilionao kwako ni zaidi ya urafiki"

Wakati namueleza hayo tulikuwa tumekaa sitting room, yeye alikuwa amekaa chini kwenye zuria na mimi nimekaa kwenye kochi, nikanyoosha maelezo kwamba nampenda kimapenzi

Caryn: "You're joking, right?"

BM: "Nop, I'm serious, very serious"

Caryn: "Kama unamaanisha sidhani kama ni idea nzuri mimi na wewe kuwa wapenzi"

BM: "Kwanini?"

Caryn: "Okay, I used to love you, I mean i developed feelings for you lakini for Dad's sake I had to let it die"

Nilivyosikia for Dad's sake nikajua tayari Mzee kuna venye ameongea na Mwanae, nikamuuliza Caryn "Kwahiyo hapa hofu ni Mzee sio?"

Caryn: "Hofu sio Mzee, hofu ni kukupoteza wewe"

BM: "Mmh! Aje sasa? kwa hatua tuliyofikia nayo sidhani kama tunaweza kuwa separated labda uwe Mpango wa Sir God"

Caryn: "Nimemaanisha kukupoteza as a friend, unajua we lose people who are potential and important to us and in our careers sababu ya mapenzi

.....Dad aliniambia kuna watu ni muhimu sana ambao we don't deserve to date them kwasababu tunaweza kuwapoteza pindi mapenzi yatakapoisha"

Kumbuka haya maongezi yanafanyika kabla ya Mzee kuja kwangu, Sasa baada ya Mzee kuja kwangu kama mnakumbuka aliniuliza kuwa nina Mpango gani na Mwanae kabla sijamjibu ndipo akaniambia kwamba

"kwenye hii Dunia ukitambua wenye manufaa maishani mwako usiwape umuhimu, HAWATAKUUMIZA. Wenye umuhimu maishani mwako usiwafanye wenye manufaa, UTAUMIA"

Sasa hii siku jioni yake kuna kitu nilimuuliza Càryn ambacho sikukisimulia last episode

kutokana na lile swali kutoka kwa Mzee "Una Mpango gani na Caryn" nilimuuliza Caryn kama amemshirikisha Mzee kuhusiana na Mimi kumtaka kimapenzi, akaniambia hakumshirikisha"

BM: "Kuna swali ameniuliza ndio maana nataka kujua, so kama ulimshirikisha we niambie tu"

Caryn: "Swali gani kwani amekuuliza?"

BM: "Nina Mpango gani na wewe?"

Caryn: "Hapana, sijaongea na Mzee chochote kuhusu hayo mambo"

Siku zikapita, majanga yakatokea na kazi nikasimamishwa, nikawa sina budi ku move on lakini na-move on huku nikisikilizia Mpango wa Caryn huku nikitafuta Plan B ya kuni backup endapo mchongo wa Caryn uta-Bounce

Mpango wa Caryn ni gani sasa? ....ni huu hapa>>>kabla ya Mzee kumshirikisha Caryn kuhusu mimi kwenda China, Caryn nae alikuwa na Mpango wa kufungua Kampuni ya Air Cargo kama ile ya Baba yake, Sasa kabla hajanichana ndio Mzee akaja na Safari ya China na yeye ndio akaleta Proposal yake mezani

Mpango nikauona umenyooka kabisa na Caryn alikuwa serious na hilo kiasi kwamba aliachana na Mpango wake wa kununua Gari mpya kama alivyojiwekea ahadi,

Basi tulivyo sketch kila kitu kuhusu hiyo Kampuni ambayo mimi ndio nitakuwa nikiisimamia, kwasababu ya uchanga wa Kampuni tulipanga Mkurugenzi niwe Mimi na Logistic Manager niwe mimi na huku kwenye Kampuni ya Mzee pia nabaki na position yangu Ile Ile as a Logistic Manager Yani kwa kifupi nipige miguu yote yote

Hapa ndipo niliporudi kwa Mzee na kumchomolea Ile safari ya China, But guess what? Mchongo ukawa mchongoma na Deal halijakua done kama nilivyotegemea bali Dili limekuwa Dilisha, Wanasema mtaka yote hukosa yote...Yes, ila kwangu imekuwa tofauti kidogo, Mimi sikutaka yote na bado nikakosa yote

Nili think twice kwenye mchongo ambao ni wa uhakika na sikutakiwa hata kupoteza muda, I mean the deal was good and i wasn't supposed to think twice, Lakini sio mbaya Uzuri ni kwamba mtu aliye kwenda China badala yangu nammudu na tunaelewana vizuri basi naimani tutafanya makubwa zaidi

Lakini ubaya wa Binadamu huwa wanabadilika sana, so hutakiwi kuwategemea kabisa, ila sidhani kama Mchina atani disappoint kama alivyoni disappoint Kijana wa Buguruni, Kijanaa bhana alianza Ukola, nilianza kusikia makesi zake kutoka kwa sister mara "ooh huyu mtu leo hajarudi" mara "karudi lakini hakulala kabadilisha tu nguo na kuondoka"

Kabla ya kuongea nae nikaanza kumfuatilia, nilienda kule kijiweni kwake nikaambiwa ana kama wiki hivi hajaenda, lakini hiyo haikuwa kesi kwasababu jamaa kaniambia huwenda kuna kazi anafanya sehemu maana almost vifaa vyake vyote amebeba, moyoni nikajiuliza ni kazi gani hiyo inayomfanya mtu asirudi nyumbani

Nikaendelea na shughuli zangu hadi hivi unavyosoma hii story sijamtia machoni yule Kijana, nilienda tena kule anakofanyia kazi yule blaza aliniambia siku ile nilivyoenda kumuulizia baada ya siku kadhaa Kijana alienda na akachukua vifaa vyake vyote alivyoviacha huku madai yake yakiwa ni yale yale kwamba kuna kazi anaenda kuifanya,

Blanda niliyoifanya ni kutokumuambia yule blaza azuie vile vifaa vilivyobaki kama akivirudia lakini by that time sikuwaza nilichokuwa nakiwaza sasa hivi

Anyway, I have bad feelings kuhusu Kijanaa lakini mimi huwa mzito sana ku judge, nilichokifanya nilimjulisha Mzee tu, kilichobaki nikusubiria muda uniambie jambo (time will tell)

Back to BM & Caryn Nothing is working according to plan anymore, Caryn alirudi kwao lakini hakuondoka na nguo zake alienda yeye kama yeye hata Gari yake aliiacha akawa anatumia Jeep Wrangler ya Mzee, hiki kipindi Caryn alichoacha gari yake ndio kilikuwa kile kipindi kigumu, cos nilikuwa naenda misele na Gari naiacha nyumbani, si mnajua magari hayatumii Maji eeh, tena hii Engine Capacity yake si kubwa kihivyo, ni 2.5 tu

Hadi leo karibia mwezi sasa Gari bado imepark kwangu lakini siku niliyotoka nayo hazizidi 4, Hizo mara tatu ilikuwa ni misele yangu Binafsi mara moja nilitoka nayo kwenda kuonana na Càryn, tena ni juzi hapa hata week haijaisha nadhani

Hii ilikuwa Bonus Episode tu ya matukio ambayo sikuyasimulia lakini Wacha niunge na matukio yaliyotokea recently

Siku ya Jumatatu asubuhi najiandaa kwenda job kwasababu Jana yake Caryn aliniambia niende, Mimi bila hiyana nikachomoka hadi ofisini, kufika ofisini nilivyoonana na Caryn akaanza kunihoji kuhusu Ile Kampuni niliopoteza mzigo wao kama nipo sawa nao au kuna kabifu ka chini chini kanaendelea kati yetu

Nikashangaa Caryn kuniuliza vile kwasababu Mimi BM naanzaje kuwa na Bifu na likampuni linaloingiza mamilioni ya Pesa, nikamuambia Caryn hakuna Bifu na wala halitakuja litokee, labda nifungue Kampuni kama yao hapo ndio ita make sense mimi kuwa na bifu nao

Caryn: "Ooh! now I see nilichoambiwa kinaweza Kuwa na ukweli"

BM: "Umeambiwa nini na nani?"

Caryn: "Unajua nilienda kule nilikuwa na kikao nao, walikuwa na Agenda zao za kuzungumza ila na mimi nilikuwa na Agenda zangu, moja ya agenda inakuhusu wewe"

BM: "Mimi! how?"

Kwa kifupi Caryn alitaka kujua kama kuna makosa mengine nishawahi kufanya hapo nyuma au ni hili la juzi tu, maana Caryn anakuambia kwa namna Ile Kampuni ilivyoreact kuhusu upotevu wa mzigo alijua tu kuna something else, si ndipo wakamfungukia sasa

Iko hivi, kuna siku nilipeleka mizigo yao kule ofisini kwao, sasa wakati mizigo inashushwa kuna mzigo mwingine ulikuwa mzigo sana, kule Bandarini tuliupakia kwa Forklift na huku kwenye Kampuni pia tuliushusha na forklift, so you can imagine huo mzigo ni mzito kiasi gani, Sasa Mimi si nikaropota nikasema Hawa wateja ningewajua ningewaiba nikawa link moja kwa moja kwenye Kampuni yetu ningekuwa napata Commission ya kueleweka kwa aina hii mizigo (Hapo sasa ndipo nilipo halibu)

Kwasababu unajua wateja wa Ile Kampuni wao hawajui kama mizigo tunawasafirishia sisi wao wanajua ni Ile Kampuni ndio inafanya Kila kitu which is not true, Mimi nawaona ni kama mtu kati, ma broker flani ivi, ukiacha na hao pia kuna hawa watu wengine ambao wanakula pesa ya bure kabisa ambao huwa wanagiza mzigo china na kuwauzia wafanyabiashara wa mikoani, na unakuta yule mfanyabiashara wa mkoani nae anapata faida yake vizuri tu licha ya pesa yake kupita kwa mtu wa kati, sasa je kama angekuwa anaagiza yeye mwenyewe moja kwa moja kutoka china si angekuwa ana double profits,

Anyway ndio Biashara ilivyo lakini, kitendo Cha mimi kuongea Ile kauli kumbe yule jamaa aliibeba kama ilivyo akaenda kumuambia Boss wake, bwana weeh! wakawa wananisubiri niingie kwenye 18 zao na mimi si nikajaa wakanila kichwa, Aisee sikufikiria Ile kauli yangu kama ingekuja kuni cost pakubwa hivi

Unajua nilianza kumfikiria vibaya Opportunist kama wengi walivyokuwa wanadhania humu, kuna wengine humu waliniogopesha zaidi kwa kusema Hilo ni game nachezewa na Mzee kwamba hata Caryn anaweza akawa anajua kinachoendelea sema amekausha tu, Aysee nyie mliniogopesha sana

Sasa Caryn kaniambia kule kamalizana nao so nirudi mzigoni ila nikakataa, Caryn aliniruhusu niondoke badae au kesho atakuja mjengoni tuongee vizuri, nilitoka pale ofisini mida ya saa tano tano hivi asubuhi ndio nikaja humu kuandika I think we should forget a day to remember

Hamuwezi amini hii siku nilipata amani ya moyo maana siku zote nilihisi kama kuna kitu kinanikereketa, Hii siku Caryn hakuja nikabaki kuongea na Annie kwenye simu, Annie anawaza ujio wake wa kuja Dar na Bus anadai hataki kuja na ndege (Annie anakuja tarehe 4 mwezi wa 6)

Mimi nikawa namng'ang'aniza atumie ndege ili afike mapema, kwasababu akitumie Bus tutapeana heka heka za kwenda kupokeana saa sita za usiku, Mwisho wa siku nikamuambia atumie usafiri anaouona yeye unafaa

Zilipita kama siku 2 Caryn akaja home akanikuta na msimamo wangu ule ule, nikamuambia Caryn kuna ulazima gani wa mimi kurudi kufanya kazi ikiwa watu wengine wapo na wanafanya kazi vizuri tu, Caryn akaniambia Opportunist anafanya kazi vizuri lakini bado ana pwaya,

Caryn anadai Opportunist anatumia gharama kubwa kwenye kutoa mzigo, Mimi nikawa nishajua ni wapi anapokosea Opportunist, unajua kwenye haya maisha hutakiwi kuonesha mbinu zako zote za kivita, ukionesha siraha zako zote ujue wakulungwa watachukua Points 3 muhimu, inabidi ukiondoka sehemu uache pengo kwasababu siku hizi mapengo yanazibika vizuri tu

Nikamuambia Caryn amvumilie tu jamaa mwisho wa siku atajua, Mimi mwenyewe nilikuwa sijui chochote

Caryn: "BM bado una Grudge?"

BM: "Hapana! wala sina kinyongo, ila hizi nenda rudi nenda rudi kwangu hazinikalii poa"

Caryn: "Kama ni hivyo basi kulikuwa hakuna sababu za mimi kukukatalia wewe kuwa na mimi"

BM: "Unamaanisha nini?"

BM: "Daddy alinitahadharisha kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na wewe"

Dah! Mzee bhana....eniwei, According to Caryn Mzee alipenda sana urafiki pamoja na bond iliyopo kati yangu mimi na Caryn, (Hapo ni Mzee Sasa anamuambia Caryn) Mzee ananichukulia mimi (BM) kijana wa tofauti sana, kwasababu kuna mambo Caryn anaweza kuyafanya na mimi nikayachukulia poa kwasababu ya urafiki sasa kama tutaingia kwenye Mapenzi na kwa Caryn jinsi alivyo akafanya mambo au maamuzi Fulani ambayo hapo awali nilikuwa nayachukulia poa lakini huku kwenye Mapenzi nisiyachukulie poa tena (Perspectives za Mzee hizo)

So Mzee akamuambia Caryn kama ataingia kwenye mahusiano na mimi, kwanza akubali kumpoteza rafiki na workmate na hata Business Partner kwa hapo badae

Mzee alimuambia Caryn kwamba anaweza kuniona mimi muhimu kama Rafiki lakini umuhimu huo asiuone pindi atakapokuwa na mimi katika Mahusiano ya kimapenzi

BM: "Lakini watu wanaweza wakawa wapenzi na bado wakawa marafiki"

Caryn: "Hata mimi nilimuambia hivyo hivyo"

BM: "Akasemaje?"

Caryn: "Kasema ina depend na Character ya mtu"

Caryn akasema kwamba kwa mujibu wa Mzee, anadai Michelle ndio ana sifa hiyo lakini Caryn hana so kama atafanya kinyume na kuwa kimapenzi na mimi basi kuna mawili yatatokea, either Mimi nimvumilie sana Caryn na nikishindwa kumvumilia basi tutaachana na tukiacha pia kuna mawili, urafiki utakufa au utabaki na hata kama utabaki hautakuwa kama ule wa mwanzo, Mzee akadai maamuzi ya kiakili yanahitajika zaidi kuliko maamuzi ya kihisia

BM: "Wow, nimemuelewa Mzee Kwa kiasi chake"

Caryn: "Mimi nipo tayari kukuvumilia wewe BM"

BM: "Una maanisha kwamba?"

Caryn: "Kama kuna tabia zangu ambazo huzipendi niambie nipo tayari kuziacha"

MWISHO WA SEASON 2, Maybe to be continued
Hahahaa mkuu hapo Careen si ni kama kashasema yes! so kifupi swali langu still halijajibiwa na hii bonus episode nataka unijibu wewe mwenyewe 😊 😊
 
Umetisha sana mwamba, natumai onwards utazichanga karata vyema.. Hapo mpaka sasa game inakubeba wewe
 
Ila Careen nimemkubali sana aisee sio kwa confidence hiyo.. hivi hayo majibu aliyokuwa anakupa alikua na mood na aibu za kike kike au ndio alikua mkavu kama boss🤣🤣🤣.. I bet kasoma IST huyo
 
Asante sana blazee....

Kwanza nimepokea Maua yangu,

Pili Mw/Mungu akipenda labda (underline neno labda) nitakuja na SEASON 3 so utapa kujua mtihani niliuvukaje
Mimi niseme tu fata ushauri wa mzee tabia ya binadamu aibadiliki but itajificha kidogo baadae itarud ukija kushtuka you lost everything.
 
Maua yako pokea BM X6
20230505_154534.jpg
 
Mi ki ukweli hii story naifuatilia ila kuna sehemu naona as a man kuna sehemu unafeli. Sijui nature ya familia yako ila kwa ulivyojiweka ni kama umeshakuwa part ya familia ya mzee. Kuna vitu unashindwa kuvifanya kwa maendeleo yako wewe, ila unafanya kwa sababu ya nature ya watu
Noted Mkuu
 
Mkuu, kwanza hongera kwa uandishi mzuri!

Pili, nakushukuru kwa kujitolea kuleta simulizi hii! Ukiacha kuburudisha akili, mtu makini hakosi cha kujifunza hapa!

Tatu, kwa mtazamo wangu ondoa fikra za mapenzi kwa Caryn. Endelea kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, kujishusha huku ukitanguliza akili kwa kila jambo!
Kama ni upendo acha Caryn akupambanie kama ilivyokuwa kwa Anie na Accountant.

Nne, usimuonyeshe Caryn mahusiano yako mengine ( meaning of Anie na wengine kama wapo), hata kwa Anie hivyo hivyo!
Nadhani kwa sasa hauko katika wakati mzuri wa kuamua ni nani hasa anafaa.

Tano, uwe na plan B (Backup plan). Sekta binafsi hazitabiriki, kuachishwa kazi ni muda wowote mood ya mwajiri ikibadilika. Save as much as you can! Fungua kitega/vitega uchumi kwa siri kama ukiweza... (Reffer to Caryn, anafungua miradi bila Mzee kujua... hopefully anajiandaa kwa lolote mbele ya safari hasa ukizingatia kuwa familia za kiafrika hazijambo kwa kugombania urithi).

Mwisho, nakutakia kila lakheri! Usiache kumtanguliza Mungu katika upambanaji wako!
 
Mkuu, kwanza hongera kwa uandishi mzuri!

Pili, nakushukuru kwa kujitolea kuleta simulizi hii! Ukiacha kuburudisha akili, mtu makini hakosi cha kujifunza hapa!

Tatu, kwa mtazamo wangu ondoa fikra za mapenzi kwa Caryn. Endelea kufanya kazi kwa bidii, ubunifu, kujishusha huku ukitanguliza akili kwa kila jambo!
Kama ni upendo acha Caryn akupambanie kama ilivyokuwa kwa Anie na Accountant.

Nne, usimuonyeshe Caryn mahusiano yako mengine ( meaning of Anie na wengine kama wapo), hata kwa Anie hivyo hivyo!
Nadhani kwa sasa hauko katika wakati mzuri wa kuamua ni nani hasa anafaa.

Tano, uwe na plan B (Backup plan). Sekta binafsi hazitabiriki, kuachishwa kazi ni muda wowote mood ya mwajiri ikibadilika. Save as much as you can! Fungua kitega/vitega uchumi kwa siri kama ukiweza... (Reffer to Caryn, anafungua miradi bila Mzee kujua... hopefully anajiandaa kwa lolote mbele ya safari hasa ukizingatia kuwa familia za kiafrika hazijambo kwa kugombania urithi).

Mwisho, nakutakia kila lakheri! Usiache kumtanguliza Mungu katika upambanaji wako!
1: Nimeyapokea maua yangu

2: Shukrani sana, hata mimi mwenyewe najifunza kupitia mapito yangu

3: Fikra zangu hazikuwa kwa Caryn kabisa ila yeye nadhani Fikra zake zilikuwa kwangu hadi nikajikuta na mimi nazama humo humo

⁴ : Nimeamua kuandika ka nnē kadogo kwasababu nahisi kama haitawezeka, Yani Kila nikichungulia sioni tobo, sijui nitatumia mbinu gani kufanikisha hilo

5: Ni muhimu sana, huo Mpango ninao muda mrefu lakiñi nashangaa kwañini nakuwa mzito kutekeleza

Mwisho: Mungu ndio kila kitu/Mungu ni Mwema

NB: Kila namba na jibu lake
 
I
Sijajua kwakweli, labda....làkini sidhani
Ila mkuu kiupande wa mahusiano naona kama unataka kurudia makosa ya mtaka vyote.. na kuna kila dalili ya kukosa vyote, sidhani kama urafiki wako na caryn utaendelea endapo atagundua kwamba umemdanyanya umemtongoza huku ukiwa na mpenzi wako, yaani ulikua na lengo la kumchanganya hakuna mwanamke atafurahia hiyo scenario
 
Back
Top Bottom