BM X6
JF-Expert Member
- Nov 24, 2020
- 1,360
- 4,149
- Thread starter
- #901
SEASON 2 EPISODE 1
Saturday, September 3, Nimeamka late nakutana na missed calls 2 za Caryn kitu ambacho sio kawaida, Caryn akipiga simu mara moja hujapokea ndio imetoka hiyo harudii tena kama ni muhimu sana ndio atarudia kwa mara ya pili, mwenyewe anakuambia Two missed calls it is enough. This generation we don't miss calls, we ignore them
Nikam call back lakini hakupokea badala yake akanitex "15:45 Arrival time" ndio nikakumbuka kumbe leo ndio Ile siku
Hapa itabidi nizuge kwanza at least nipangilie mambo yangu ili nitakapoonana na Mzee mambo yote yawe sawa, lakini kusema eti leo ndio niende Airport ni uongo,
Wiki inaelekea kukata bado sijaonana na Mzee, Jumamosi jioni nakumbuka nilikuwa na mshkaji wangu maeneo ya 'Kitambaa Cheupe' Kinondoni tumechill tu jamaa anapata kamnyweso Mimi na Grand malt zangu, simu Iko mfukoni naskia Ina vibrate kuitoa naona namba ya Mzee, Nikapata ganzi kuipokea ila kwa kujilazimisha nikasogea pembeni kupokea Ile simu
BM: "Shikamoo Mzee"
Mzee: "Marhaba, Hujambo?"
BM: "Mimi mzima kabisa, za nyumbani"
Mzee: "Sisi tuko sawa, ni wewe ndio umetukimbia"
BM: "Hapana Mzee, ni pilikapilika tu za hapa na pale"
Mzee: "Sasa nilikuwa nakuhitaji siku ya kesho jioni nyumbani, ni muhimu sana"
BM: "Sawa Mzee, nitafika bila shaka"
Namaliza kuongea na simu nikarudi nilipokuwa nimekaa na mshkaji, jamaa ananiuliza "vipi mbona kinyonge?"
BM: "Hii simu niliyopokea unajua ni ya Mzee"
Mshkaji: "Mzee gani tena?"
BM: "Si Baba yake na Caryn"
Mshkaji: "Ooh! kumbe Mshua mwenyewe, father anasemaje?"
BM: "Anasema kesho nionane nae, ni muhimu sana"
Mshkaji: "Hivyo tu?"
BM: "Ndio"
Mshkaji: "Sasa kitu gani kinakutia hofu hapo?"
BM: "Unaniuliza tena Wakati unajua mchoro mzima"
Mshkaji: "Kama ni issue Ile uliyonielezea hakuna Cha kukutia hofu hapo, kwani umeiba Cha mtu? kwanza ni haki yako ya kimsingi, ila Ulichokosea wewe yule manzi (Caryn) umemuamini sana Yani umemuelezea mambo mengine ambayo hata hukupaswa kumueleza"
BM: "Dah! ila kweli asee, sijui ilikuaje hadi nikajiachia kiasi kile"
Mshkaji: "Unajua mtu akishajua madhaifu yako ni rahisi kukumaliza, yeye ndio amekufanya uache kazi basi alitakiwa akupe hata Ile kazi ya kuzisimamia zile nyumba za kule, yeye kaenda kumpa shavu mtu mwingine kabisa huku akijua wewe huna mishe, Sasa unataka kunambia Nia yake ilikuwa nzuri?"
Mshkaji: "Sasa acha Mimi nikushauri kwa mara nyingine tena, ukiamua kuubeba huu ushauri ni sawa ukiuacha ni sawa vile vile...kivyovyote vile huo Mzee atataka kujua kwanini umeacha kazi, Sasa ili umjibu hili swali vizuri huyu manzi wako (Caryn) Hutakiwi kumtaja, we tafuta sababu zozote ziwe za ukweli au uongo ila huyo manzi usimtaje kabisa"
Mshkaji aliendelea kunipa ushauri ambao anaona unafaa japo ni mara chache sana kufuatisha ushauri wake, mara nyingi mchizi huwa ananipa ushauri then nuacha kama ulivyo, basi tulimalizia na story za hapa na pale nikagonga msosi kabisa nikasepa nilivyofika home nikapiga Maji nikalala
Kesho yake ambayo ni Jumapili nimeamka nina njaa kama yote, nikicheki mazingira hayaeleweki, hadi nikamkumbuka Annie wangu maskini, tangu Annie aondoke hii nyumba haijapigwa deki, nilichokifanya ni kufagia tu fasta fasta na kuweka nguo kwenye Washing Mashine Nikatoka zangu nje kunywa chai, nilivyorudi nikakuta Mashine ishamaliza kazi yake nikatoa nguo na kwenda kuzianika
By saa sita nguo zote zishakauka kasoro viatu tu, ikabidi nitulie tu ndani nikivisikilizia maana sina ratiba ya kutoka hadi Alasiri, nikaingia YouTube BongoHoodz wameongeza movies nikacheki movie yao inaitwa Mchepuko, Bonge la tambara
14:06 nikaanza kujianda, by saa tisa nikaanza kutoka safari ya kuelekea kwa Mzee, hadi getini nikafunguliwa geti na security nikaulizia wenyeji mlinzi ananiambia kwamba Mzee ametoka na Binti yake ila wengine wapo ndani, basi nikachoma ndani kumbe Mzee ametoka na Caryn sababu Michelle nilimkuta ndani sitting room anacheki Movie sijui Documentary ile
Michelle: "Karibu mwaya BM"
BM: "Asante, nishakaribia"
Michelle: "Za kupotea?"
BM: "Aah jamani wiki hii iliyopita sinilikuwa hapa"
Michelle: "I know, tulikumiss tu"
BM: "Niliwamiss pia hasa Mzee, hayupo Nini? naona kimya"
Michelle: "Yeah, ameenda town na Caryn after tumetoka tu Church"
BM: "Ooh, Mom yeye ako?"
Michelle: "Yap but amelala"
BM: "Okay, acha nimngoje, maana Mzee aliniambia nisikose kuja leo ni muhimu"
Michelle: "Atakuwa tu anataka feedback ya Kazi aliyokupa...vipi lakini si umefikia pazuri?"
BM: "Pazuri wapi Dada yangu, mambo ni mengi ila acha tuone vile itakuwa"
Iko hivi, Japokuwa Michelle pia nimeanza kuzoeana naye lakini hajui vitu vingi kuhusu mimi kama Caryn.... Caryn ndio anajua vitu vingi pamoja na vile ambavyo hata hapaswi kujua, so saa hiyo namsubiria Mzee kichwani nilikuwa nawaza tu Caryn asije akawa kamchana Mzee kila kitu kuhusu mimi maana yule mtoto ana visirani vyake
Ikabidi nianze kumchimba Dada Michelle kwanini yeye na Caryn haziivi sana
BM: "Dada Michelle sijui kama nishawahi kukuuliza hili swali, ivi ni kwanini wewe na Caryn hampatani sana, I mean sio watu wa kukaa pamoja na kupiga story, hizo moments zishawahi kutokea kweli kati yenu?"
Michelle: "Mimi na Caryn mbona ni marafiki sana"
Nikaona huyu ni kama ananificha kitu, marafiki gani kila mkiwa pamoja ni lazima mtupiane maneno
BM: "Dada Michelle bhana, haya bhana"
Michelle: "Ni kweli Mimi na Caryn ni marafiki sana ila kwa bahati mbaya nilikuja kumkosea ndio ameniwekea kinyongo hadi leo"
BM: "Duh! kosa gani hilo lisilosameheka?"
Michelle: "Hata halina maana, ukitaka kuishi vizuri na yule mtu itakubidi ujitahidi usimkanyage, maana ukimkosea tu huwa inamchukua muda kusahau na kusamehe"
Nilivyosikia hivyo kwanza nikaanza ku recall matukio kuona kama hakuna sehemu nimekwaza yule mtu, maana kama ipo basi kazi ninayo, maana pia Michelle alishawahi kunambia kuwa Mzee huwa anamsikiliza sana Caryn kiasi kwamba Kuna maamuzi mengine Mzee huwa anayafanya lakini ushauri unakuwa umetoka kwa Caryn. so ukiweza kwenda sawa na Caryn basi pia utakuwa upande salama wa Mzee
Sasa ilibaki tu kujua ni kitu gani hicho Michelle alimfanyia mwenzake hadi Caryn amekunja kiasi hicho, nikaja kujua ni issue ya Pesa lakini issue sio Pesa issue ni kwamba Kuna uongo na ujanja ujanja ulikatiza ndio Caryn akamaindi
Mchongo ulikuwa hivi, Michelle aliomba kiasi flani cha pesa kwa Caryn, Kama milion 11 ivi, Caryn bila wasi akatoa Cash, hiyo Pesa Michelle aliomba kwaajili ya Biashara baada ya kuona Mzee kamkazia Kila sehemu
Sasa kosa alilolifanya Michelle alivyochukua Pesa kwa Caryn mzigo wote akaenda kumpa bwana ake (Opportunist) Mtiti ndio ukaanzia hapo, na kama unavyojua mtu yeyote akikupa pesa kwa lengo la kufanya Biashara atataka aone matokea yawe hasi au chasa anachotaka kuona ni ulifanyia kazi sahihi pesa ulioomba
Caryn Kila akiulizia Michelle anapiga chenga, anaingilia huku anatokea kule, Caryn alivyoona chenga nyingi siku moja akaamua kumbana zaidi, Ndio Michelle akafunguka kwamba Pesa kampa mtu mwingine afanyie Biashara ambaye ni Mpenzi wake,
Caryn akasema sawa twende tukaione hiyo Biashara yenyewe, Unaambiwa jamaa nae akaanza chenga, Caryn akaona hii miyeyusho ndio ugomvi ukaanzia hapo
Wakati anaendelea kunielezea huo mkasa, Mama akaja pale Sitting room kutoka chumbani kwake, tukasalimiana akamuuliza Michelle "Kwani Baba yako Bado hajafika tu" Michelle akajibu "bado"
Mama: "Ni saa nyingi sana nimewasiliana nao wameniambia wapo Morocco"
Michelle: "Labda Kuna sehemu wamepitia"
Mama akaenda jikoni kuandaa Supper, Sasa zile story zetu Mimi na Michelle ilibidi tuzi sweep under the Carpet, tukaanza story nyingine haujapita hata muda mrefu nikasikia Geti kubwa linafunguliwa, Michelle akasema "ndio hao wanaingia" kweli Caryn ndio alianza kuingia ndani, kuangalia vizuri nyuma Kuna mtu ameongozana nae, huyo aliyeongozana nae Sasa, hata sikuamini....Ni Mama yake Accountant aisee
Sasa najiuliza Mama yake Accountant saa hizi tena huku kwa Mzee kunani? Kabla sijapata jibu wakawa wameshafika eneo letu, saa hiyo Mzee Bado hajaingia hapo, tukasalimiana na Mama pale pamoja na Caryn,
Wakati nasalimiana na Mama yake Accountant namuona anatabasamu tu na kuniuliza Habari za masiku, saa hiyo Caryn kala wambuzi, Michelle nae yupo zake kimya mara Mzee akaingia huku anaongea na simu, Mzee akatoa ishara kama anarudi then akapata juu chumbani kwake,
Bi Mkubwa akaja Sitting room kutoka kule jikoni alikokuwa wakasalimiana na Mama yake Accountant, ongea yao ni kama watu wanaojuana, wakawa wanapiga story zao za Biashara na Kazi sie wengine tupo kimya macho kwenye Tv
Mzee akarudi akamuambia Caryn amuandalie Kahawa, Wakati Kahawa inaandaliwa tukaanza maongezi ya kawaida, lakini maongezi yalibase kwa Mzee, Mama Michelle na Mama yake Accountant, Kahawa ikaletwa, Mzee akamwambia Michelle azime Tv
Mzee: "Hiki kikao kinawahusu watu wa3 lakini si mbaya Michelle na Mama yake wakiwepo huwenda wakashauri jambo"
Baada ya Mzee kusema hivyo moja kwa moja nikajua kikao kinanihusu Mimi, Caryn pamoja na Mama yake Accountant, mapigo ya moyo yakaongezeka kidogo nikimuangalia Caryn ka relax, Mama yake Accountant nae pia ka relax,
Ghafla nikajihisi sipo Comfortable lakini hapo bado sijajua hilo jambo la sisi watu 3 litakuwa linahusu nini, ila nikahisi kwamba kama Mama yake Accountant yupo hapa na hiki kikao kinamuhusu basi agenda ya kikao itakuwa inahusu kazi pengine Accountant alifunguka Kila Kitu kwa Mama yake ila Bado nikajiuliza kwanini huyo Accountant mwenyewe hayupo sasa?
Mzee: "Kabla sijafanya maamuzi, nataka kujua sababu zilizokufanya BM uache kazi"
Ghafla nilihisi joto wakati ndani full AC watu wote kimya mimi ndio natakiwa kuongea kwa wakati huo halafu Caryn akanipiga jicho flani hivi akakunja na mikono kifuani yani Ile kwamba "TUNAKUSIKILIZA"
Itaendelea....
Hii story ni mara ya pili sasa naiandika, mara ya kwanza niliiandika yote ilibaki tu kupaste hapa lakini ikafutika, now itabidi nitakapoishia kuandika naitupia hivyo hivyo makosa yasije yakajirudia.