Hatma ya amani tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatma ya amani tanzania

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by CITYBOY, Nov 4, 2010.

 1. C

  CITYBOY Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 42
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zangu watanzania uchaguzi umekwisha tunachongoja ni matokeo ya jumla ya urais.Nifuraha yangu kuona upinzani umeongezeka bungeni,kwani hii itasaidia kupunguza makubaliano ya miswada ambayo haina maslahi kwa taifa letu.Basi ndugu zangu tupunguze ushabiki wa kidini,kikabila,rangi na kikanda.Kwani hakika utengano ni udhaifu na umoja ni nguvu,basi na tuwe wamoja tujenge taifa letu hili changa.Siasa za mwaka huu zina harufu ya udini,hivyo kuifanya amani ya taifa kua mashakani.Watakao taka kuandamana na kuleta machafuko ni hiyari yao,ila kumbuka unaweza pata kilema au kupoteza maisha,aliyekuhamasisha tawari amekwisha kuwakimbia akiacha nchi inawaka moto.Dr.Slaa anapinga matokeo ni vema kwenda mahakamani kuliko kuingia barabarani hii ni hatari!
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hatma ya TZ ni Watanzania kudai nchi yao inayokaliwa na wakoloni weusi tangu 2000.
   
 3. U

  Uyole12 JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: Oct 3, 2010
  Messages: 586
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Uoga sometimes ndo unaofanya tanzania 2we masikini kila kukicha na 2zidi kudharauliana kila kukicha natamani m2 wadai haki yao hata kwa upinde.
   
 4. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 357
  Trophy Points: 180
  1. Udini na ukabila vimebuniwa na kutumiwa kisiasa kuchafua baadhi ya wagombea. Sijawahi kusikia mfano makanisani waumini wakihubiriwa wamchague kiongozi fulani. Natolea mfano Kanisa Katoliki kwa vile nasali huko. Kanisa hili lina wanachama kutoka vyama vyote hapa nchini. Kwa hiyo, haiwezekani askofu, padre au katekesta mwenye akili timamu kuwahubiria watu wamchague kiongozi fulani wa chama (kimojawapo) bila kuzua mtarafuku ndani ya Kanisa lenye waumini wa itikadi tofauti za vyama. Hali kadhalika kuhusu ukabila.

  Jambo ambalo lilikuwa linahusishwa na udini ni kule Dr Slaa kuwa padre wa Kanisa Katoliki na baadhi ya wanasiasa kutumia hiyo kama nyenzo ya kuzusha kila aina ya uongo eti bado anapokea maagizo kutoka kwa maaskofu na mapadre ili akiwa kiongozi atetee maslahi ya Kanisa Katoliki. Naomba kama mtu yeyote ana mfano wa askofu, padre na katekesta wa kanisa hili, ambaye alikuwa anawahubiria waumini wake wamchague Dr Slaa ajitokeze na aseme ni nani, ilikuwa wapi na lini na kwa nini haikuripotiwa polisi au mamlaka husika ili ashughulikiwe kisheria kuliko kusababisha mtafaruku katika mahusiano ya Watanzania kuhusu imani zao za dini.

  2. Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitumika kupandikiza udini na ukabila vikidhani vinakisaidia chama fulani kutawala na bila kukemewa na serikali lakini yakitokea matatizo vyombo hivyo pia vitatuhumiwa pamoja na wale wote watakaotuhumiwa kwa kusababisha machafuko nchini - yawe ya kidini, kikabila au kisiasa. Mfano, ni Rwanda: vyombo vya habari vilivyochochea vita, wahariri wao na waandishi wa habari hizo za uchochezi walipata kesi ya kujibu.

  Kwa hapa Tanzania, kuna vyombo vinachochea hali kama hii vikidhani vinaishi kwenye sayari tofauti na hii ya kwetu au vinaishi nchi ambazo mkono wa sheria hauwezi kufika.

  3. Baadhi ya wanasiasa na hata vyombo vya dola vimesaidia kuwajengea wananchi hofu ya kuzuka vita au umwagaji damu. Wapiga kura wamekuwa wakiambiwa kuwa kuchagua vyama shindani nje ya chama tawala ni kutoitakia nchi mema. Walidhani kufanya hivi ni namna ya kuwafanya wananchi wapige kura kwa uhuru na utashi wao bila kujua kuwa waliwafanya wachague kwa hofu na hivyo kupiga kura bila hiari bali shinikizo. Hiyo ilikuwa 'kuwabaka' wapiga kura kiakili.

  4. Siasa za namna hii ni hatari sana. Yaani, ili kupata kura mpaka mtu aseme uongo au aibe kura. Tanzania, tumefikia hapa na mazoea kama haya yanawafanya baadhi ya wananchi waone wale wanaojitahidi kutenda haki kama watu wabaya na wale waongo na wezi wa kura kama watu wazuri. Baadhi ya mijadala hapa JF inaonesha ukweli huu - kwamba mtu akihoji mchakato wa uchaguzi anaonekana mtu mbaya na yule anayekubali au kuhalalisha wizi wa kura kuendelea (kupoteza haki ya kuhoji pale mtu anapohisi kuna ukiukwaji wa haki) anaonekana si mpenda makuu na amekomaa kisiasa. This is rubbish!
   
 5. M

  Mbalinga JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 1,382
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
  Nafikri hufahamu kuwa matokeo ya uraisi Tanzania hayapingwi mahakamani. Ndugu yangu "Where there's no justice, there's no peace", ningekuona wa maana kama ungeishauri tume ya uchaguzi kufikiria kusitisha utangazaji wa mshindi mpaka malalamiko yameshughulikiwa. Vinginevyo ni mtaani tu, sisi wengine tumeamua kujitoa kafara kwa ajili ya wanetu na wajukuu zetu hapo kesho. Tutapinga kwa njia zote, kwa heri ama kwa shari mpaka tumeikomboa nchi yetu. Ni bora kufa ukiwa umesimama kuliko kuishi ukiwa umepiga magoti.
   
 6. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  crap
   
 7. Gwaje

  Gwaje JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 271
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 45
  Naoma
   
 8. G

  Galilee Galileo Member

  #8
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Watakao haribu amani Tanzania ni CCM wenyewe kwa sababu hawako tayari kuachia madaraka hata kama wananchi hawawataki jambo litakalo sababisha wananchi kuchua nchi kwa nguvu
   
 9. JIULIZE KWANZA

  JIULIZE KWANZA JF-Expert Member

  #9
  Nov 7, 2010
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Word...
   
 10. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #10
  Nov 7, 2010
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Usidhani Amani hutoweka pale tu watu wakianza kuuana.

  Amani Tanzania imekwisha toweka tangu siku ile wanasiasa wa CCM walipoamua kuwa juu ya sheria.

  kitendo cha kuzuia maamuzi ya wananchi kupitia kura zao ni kitendo cha kuvunja Amani kwa makusudi.

  Kitendo cha kuwaenzi wezi wa fedha ya umma na kuwaacha waendelee kutembea kifua mbele kama afanyavyo Lowassa, Rostam na chenge ni kitendo cha kuvunja Amani.

  kitendo cha kuharibu mapato ya taifa kwa kuingia mikataba isiyo na tija kwa taifa ni kitendo cha kuvunja Amani.

  CCM wanajitahidi sana kuwaambia wananchi kwamba wana Amani eti kwa sababu hawafi kwa kupigwa Risasi na Mafisadi bali wanakufa kwa ufukara wa kutengenezwa na Serikali Fisadi ya CCM.

  Amani imekwisha toweshwa na mafiasadi wa CCM siku nyingi zilizo pita. Kilichobaki ni taifa kukumbana uso kwa uso na hatua ya juu zaidi ya kutoweka kwa Amani.CCM wanajua hatua hiyo itafikiwa, kwa janja yao ya nyani CCM wanatafuta mtu wa kumbebesha zigo la lawana ya kutowesha Amani ili tufikiapo hatua hiyo wananchi wawaone wao wasafi. Chaguo la CCM la kondoo wa kubeba dhambi yao si mwingine ila
  Dr Slaa.

  Hamtafanikiwa kwa sababu mmejijaza na kujilisha uongo na upepo.

  Siku ukiona watu wameanza kutoana Roho ni siku ambayo hali ya kuto kuwa na Amani kwa muda mrefu itakuwa imefikia kileleni.
   
 11. chapaa

  chapaa JF-Expert Member

  #11
  Nov 7, 2010
  Joined: Feb 19, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Kama wa TZ tutaendelea kuchezeshwa mchezo wa kitoto tufike mahali sasa TUSHIKE JEMBE TUINGIE SHAMBANI ,binafsi nimesha choka nao.
   
 12. giraffe

  giraffe JF-Expert Member

  #12
  Nov 7, 2010
  Joined: Jun 6, 2010
  Messages: 504
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Lets die,we are tired
   
Loading...