Hatimaye WANAWAKE walalamikia MBINU ZA UZAZ WA MPANGO

not good at all,though sijawahi kutumia ila naona wanavyohangaika watumiaji,ni heri kutumia njia za jadi kama kuhesabu kalenda n.k

hamasiha wenzio wasitumie,jana nimskiza bbc nimehuzunika sana,,,,wanawake wanaumia sana kwakweli
 
Hii Serikali huwa haisikii kama kenge, kumbuka hata SP ililalamikiwa sana, watu walibabuka ngozi na wengine kupoteza maisha wao wakakomaa tu, mpaka kelele zilivyozidi ndo wakazinduka usingizini! hatuna serikali ya kutumikia watu bali ni kinyume chake!
 
Wengi wetu hapa tunatoa ushuhuda wa ATHARI ZA HII KITU,KWANINI SERIKALI INAHAMSISHA KUTUMIA,?NA KWANINI BADO WATU WANATUMIA????@WADAU

Mkuu hapo kwenye red ni kama unavyoona sigara,pamoja na tahadhari iliyopo ya kufukuza mteja,(Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya yako) lakini bado watu wanakwenda kununua,jiulize kwenye hizo dawa ambazo zina ujumbe wa kumvuta mteja.Kuhusu serikali yetu naomba nisiongee maana vituko vilivyopo katika nchi yetu mtu unaweza kufa kabla ya siku yako.
 
Hapo red sikubaliani na wewe manake huwa zinatolewa bure!

Ni bure kwa maana ipi? Hivi unajua kwamba hakuna kitu duniani cha bure? Hizo dawa inakuwa tayari zimelipiwa na serikali na watumiaji ndiyo wanapewa bila kununua. Na kwa taarifa yako. Vitu hivyo unavyoita vya bure ndivyo vinavyoifilisi nchi kwa sana kwani ufisadi mkubwa unafanyika wakati serikali inaponunua kutoka nje.
 
Katika kipindi cha dira ya dunia cha BBC nimewasikia baadhi ya wanawake wa Dar es salaam wakilalamikia mbinu za uzaz wa mpango kuwa zina madhara kwao,,,,wengi wameonesha kusikitika na kujutia madhara wanayoyapata na wanailaum serikali kwanin inahamasisha????
Mmoja nimemsikia akisema alikosa kuona siku zake(kupata hedhi)na akawa anapata maumivu ya KIUNO,yupo aliyesema ingawa ameacha kutumia hadi sasa hajapata mtoto tena na haish kuhisi kichefichefu,
Swali kwa wataalam(madaktar)naomba sana mtuambie JE NJIA ZA UZAZ WA MPANGO KWA WANAWAKE KIAFYA ZIKOJE????

Mimi si mtaalamu wa hizo njia, ila kwa upeo wangu mdogo naona njia za kizamani kama kutumia kalenda au njia za sasa kwa kutumia familia condoms zinaweza kuwa salama zaidi na hazina madhara yeyote yaliyoripotiwa mpaka sasa.
 
Rafiki yangu mmoja aliwekewa vile vipandikizi, kilikuwa ni cha kumzuia kupata ujauzito kwa miaka mitano, hakupata period kwa mwaka na kama miez nane hv since aanze tumia hiyo njia, ila siku moja alikuja akaanza kubleed ghafla tu, haikuwa ya kawaida kwani damu ilikuwa ni nyingi mno, alikuwa anaumwa sana na kichwa, na alibleed mfululizo kwa mwez mzima mapaka akaanza kubadilika rangi coz aliishiwa na dam, ikabid wamtolee huo mjiti aanze kutumia vidinge vya majira ambavyo ndio vilimsaidia kukata hyo dam but vilikuwa vinamuumisha kichwa mno................

watu wengi sana wanalalamikia hizi njia za uzaz wa mpango, hapo bado hujaota kitambi na kunenepa ovyo ovyo...............
 
Ni bure kwa maana ipi? Hivi unajua kwamba hakuna kitu duniani cha bure? Hizo dawa inakuwa tayari zimelipiwa na serikali na watumiaji ndiyo wanapewa bila kununua. Na kwa taarifa yako. Vitu hivyo unavyoita vya bure ndivyo vinavyoifilisi nchi kwa sana kwani ufisadi mkubwa unafanyika wakati serikali inaponunua kutoka nje.

Na kwa taarifa yako kama serikali inakuwa imezilipia huko mie sijui ila kwenye clinic za kina mama huwa wanatoa bure kwa anaehitaji.......mie pia najua hakuna kitu cha bure duniani.
 
Kusema kweli madhara ni makubwa tu, mpango wa uzazi umetufanya tuhangaike hospitali kibao mpaka muhimbili kupima sperms na mifumo ya uzazi kuona kama tuko sawa kwa miaka 3 tukitafuta mtoto hatimaye tukafanikiwa.

Kiukweli hizi nyia zina madhara sana, zaidi ya hapo wife ameota kitambi ambacho kukitoa imekuwa kazi kwelikweli

Kimox! LOL. Mimi mwenyewe nimeona kitambi kimeota hapa nahaha kufanya situps. Nilitumia njit for 5 years, kupata mimba haikuwa tatizo kwangu hata kidogo zaidi ya kitambi na ku-gain weight. Nafikiri miili inatofauti. Sijawahi kuhaha kupata mimba.
 
Na kwa taarifa yako kama serikali inakuwa imezilipia huko mie sijui ila kwenye clinic za kina mama huwa wanatoa bure kwa anaehitaji.......mie pia najua hakuna kitu cha bure duniani.

kuweka njiti ni shilingi 1000, nazungumzia miaka ya 2000, sijui sasa hivi imefika ngapi. Nimeamua kukomaa kwenye kuhesabu.
 
kuweka njiti ni shilingi 1000, nazungumzia miaka ya 2000, sijui sasa hivi imefika ngapi. Nimeamua kukomaa kwenye kuhesabu.

Hahaha huku kwetu ni bure ila kuna siku wanakuambia dawa hamna hivyo changia kidogo ndio unatoa hiyo 1000.....komaa tu mpendwa manake hizi dawa sio mpango kabisa.....madhara yake ni makubwa mno.....kama sio sasa huko mbeleni....

Nje ya mada: habari za masiku tele?......umejificha wapi na mie nikuje?
 
njia za jadi (kalenda) ndio nzuri asikudanganye mtu ukaanza kutumia vidonge
angalizo kalenda nayo inahitaji uelewa wa kutosha kwani menstruation cycle (mzunguko wa mwezi) sio costant (sawa) kwa kila mwezi na kwa kila mwanamke kwa sababu mbali mbali kama kutumia dawa kali, msongo wa mawazo n.k mara nyingi ovulation ( yai kukomaa na kushushwa) hutokea siku ya 14au15 (hii ina maana mara nyingi mimba hutungwa siku ya 14au15) baada ya hedhi na yai hilo huishi kwa masaa takribani 36 na sperm (mbegu za kiume) huishi takribani masaa 42.(siku mbili) hivyo kwa mahesabu haya utagundua kuwa mimba inaweza kutugwa siku ya 11-17 baada ya hedhi
kutokea
 
Hahaha huku kwetu ni bure ila kuna siku wanakuambia dawa hamna hivyo changia kidogo ndio unatoa hiyo 1000.....komaa tu mpendwa manake hizi dawa sio mpango kabisa.....madhara yake ni makubwa mno.....kama sio sasa huko mbeleni....

Nje ya mada: habari za masiku tele?......umejificha wapi na mie nikuje?

Sijambo mpendwa wangu, karibu sana labda nitachelekelea mpaka jino la mwisho. Niko bongo, baridi linaendelea kupuliza tu nyakati za asubuhi, nahisi kurudi kuweka njiti maana mimba nje nje! lol
 
Tatizo tumekuwa tukiishi kwa akili za kuazima, kila tunachoambiwa au kuletewa na wazungu tuna-copy na ku-paste, hatutumii akili na uwezo wetu kuthibitisha ubora wa vitu tunavyoletewa.

Kuna Dokta mmoja aliwahi kunieleza kuwa dawa za mpango wa uzazi zina matatizo mengi kwenye mfumo wa uzazi wa wanawake, aliniambia kuwa, dawa hizo huongeza bacteria kwenye njia za uzazi za mwanamke ambao hushambulia sana mbegu za kiume, akanihakikishia kuwa hata ongezeko la watoto wa kike tunaloliona kwenye clinic zetu linatokana na dawa hizi.
Inauma sana.
 
Sijambo mpendwa wangu, karibu sana labda nitachelekelea mpaka jino la mwisho. Niko bongo, baridi linaendelea kupuliza tu nyakati za asubuhi, nahisi kurudi kuweka njiti maana mimba nje nje! lol

Hahahaahha eti mimba nje nje lol.....haina tatizo ikitokea mie naleta nepi.....ahsante mwaya .....ngoja nikusanye nauli ikijaa tu nakufuata!
 
Si kila kitolewacho bure ni kweli ni bure...someone somewhere is paying for it.
Kuna pharmaceutical industry duniani inayogawa dawa bure???? Hata za HIV si za bure someone is paying. And paying very high price kwani hivi ni kati ya viwanda tajiri sana duniani.

Kwa hiyo matangazo ni muhimu ili watumiaji watumie na mwenye dawa aendelee kulipwa.

Hapo red sikubaliani na wewe manake huwa zinatolewa bure!
 
Back
Top Bottom