Hatimaye wameamua kumkamata

Ila kijani, hawajui kwamba kwa kufanya hibi wanamuongezea nguvu zaidi na ndio atazidi kupata attention kutoka kwa wananchi. Kweli kule kijani kumejaa mapopoma na hata walio na akili nao wamejitoa ufahamu, mitego kidogo tu wanajaa
 
Alafu mnasema mnataka kuandamana na kukinukisha mtaweza kweli?
 
Kazi ya Jamii Forum nikufanya je, ni wananchi kuja na kuandika ujumbe, kero na ukweli THEN WHAT? ALFU NINI KINAFANYIKA? kama wannchi zaidi ya Elfu1 Wanaweza kuona nakuandika kilichotekea kwa Lissu sio sawa na sio haki Lakini haisaidi kueka mdhamana wakumtoa kituoni wala vyote tunavyoviongeaa huku vinatenda kazi Gan... wananchi tumekuwa waoga wakutekeleza vitendo ndio sababu wengi tuko hapa Tunaandika maneno TUUU..... JE LISSU ATAWEZA KUTOKA KITUONI KWA MSAADA YA WANANCHI NA CCM AMETUZOEA KIASI KWAMBA ANAKUNYA MBELE YETU, NATUNAMSAIDIA KUZOA
 
Mitandao ya kijamii ina nguvu na ni nyenzo mojawapo ya kupaza sauti na kufikisha ujumbe sehemu husika
 
Somo linaeleweka kabisa kuna watu apo Lumumba na kule msoga wataanza kukimbiana uko mbeleni Kuna makaburi yatafukuliwa kulipa na kujibu tuhuma,
Na hapo ndipo unabii wa mwalimu Nyerere ulipo karibu kutimia hivi karibuni.
 
Mitandao ya kijamii ina nguvu na ni nyenzo mojawapo ya kupaza sauti na kufikisha ujumbe sehemu husika

Mitandao ya kijamii ina nguvu na ni nyenzo mojawapo ya kupaza sauti na kufikisha ujumbe sehemu husika
inapofika inatekelezwa na lini inafika hapo sehemu husika na kama vilio vilivyopo huku ni vingi sana, na bado vinaongezeka, Nadhani inaitajika nguvu zaidi tufikie wahusika pengine Lissu angeweza kuachiliwa Mapema Kama hizi sauti zinafika sehemu husika
 
#HABARI: Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu amepandishwa Katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa kesi mbili ambapo awali alisomewa kesi ya uhaini na ya pili ina mashitaka matatu ya kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Katika kesi ya uhaini ambayo alishtakiwa awali majira ya saa 10:15, kesi hiyo iliahirishwa huku ikipangwa kuendelea Aprili 24, 2025.

Upande wa utetezi unaongozwa na Wakili Dk. Rugemeleza Nshalla, Hekima Mwasipu, Jebra Kambole, Dickson Matata, Gastoni Garubindi na Michael Lugina.

Mhe. Lissu alikamatwa jana Aprili 9, 2025 wilayani Mbinga mkoani Ruvuma kwenye Mkutano wa hadhara Wa Operesheni Kabambe ya #NoReformsNoElection na muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano huo (Ambao ulitawanywa Kwa Mabomu ya Machozi) Mwenyekiti Lissu alisafirishwa hadi Dar es Salaam.

Kabla ya kufikishwa mahakamani, Lissu alihojiwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Central jijini Dar es Salaam.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…