Hatimaye Startimes watoa taarifa rasmi kuhusu channel za bure

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,607
Reaction score
4,766
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU CHANELI ZA BURE (FTA)
presstz.net

INAFAHAMIKA vizuri kwamba televisheni zote za kianologia zilizimwa tangu Januari 1, 2013 nchini Tanzania. Na kwa miaka iliyofata, urushaji wa matangazo na vipindi vya ndani ukabadilika kuwa wa mifumo ya kidigitali hivyo kufanya ongezeko kubwa katika maudhui na vipindi. Star Media (Tanznaia) Limited, moja ya kampuni kubwa za kidigitali zenye vibali (MUX), inafuata maono na mpango wa kuhakikisha kila familia ya kitanzania inapata huduma ya luninga za kidigitali ambayo wanaweza kumudu kutazama. Star Media (Tanzania) Limited ndiyo kampuni iliyotengeneza na kuendesha huduma kubwa zaidi ya matangazo ya kidigitali, huku ikirusha matangazo ya zaidi ya chaneli 20 za ndani. Jitihada zote hizi zilifanya uhamiaji kwenye mifumo ya kidigitali kuwa rahisi, na vipindi vingi vya ndani vimeweza kuonyeshwa.

Hata hivyo, kutokana na mawasiliano hafifu na wateja pia kutofafanua vizuri juu ya bidhaa zetu, kumekuwa na baadhi ya mambo kuhusu luninga za kidigitali ambayo hajaeleweka vizuri. Jitihada zaidi inabidi zifanyike katika kuwaelewesha kuhusu matangaazo ya kidigitali. Hasa upande wa chanelii za Bure (FTA), inahitaji kuelezewa kama ifuatavyo:
1: Watumiaji wote wanaweza kununua dikoda za FTA kwa bei ya kuuzia ambayo ni Tsh 89,000 kwenye maduka yetu na kwa mawakala wa Star Media (Tanzania) Limited, kama zinavyoonekana kwenye picha ya kwanza. Baada ya kununua dikoda ya aina hiyo wateja wanaweza kutazama chaneli za Bure bila kulipia malipo ya kila mwezi. Watapata chaneli kuanzia 6 hadi 16 (Inategemea na sehemu ambapo kibali cha mwenye maudhui kinaruhusu). Hii pia ni hatua ambayo inayofatwa na Star Media (Tanzania) Limited kama kampuni yenye kibali (MUX).
2: Dikoda ya Kulipia inaweza kununuliwa kwenye maduka yetu na mawakala, kama inavyooneshwa kwenye kielelezo namba 2 hapo chini, dikoda hizi zina tozo ndogo ambayo watumiaji wanaweza kununua kwa gharama nafuu kisha wanalipia ada ya mwezi ili kutazama chaneli za bure za Nyumbani , na pia kutamzama chaneli nyingi zaidi za kimataifa na nyinginezo za nyumbani za kulipia. Gharama ya dikoda hii ni Shilingi 45000/=
3: Watumiaji pia wanao uwezo wa kuchagua dikoda nyingine tofauti kulingana na mahitaji yao. Pia kama mtumiaji aliyechagua dikoda ya kulipia akitaka kurudi/kubadilisha apate chaneli za bure sawasawa na mahitaji yake anaoweza kulipia tofauti ya gharama ambayo ni shilingi 44000 katika maduka yetu. Na baada ya hapo anaweza kutazama chaneli za bure.
Star Media (Tanzania) Limited itaendelea kufanya kazi kisheria, bega kwa bega na TBC pia itaendeleza uhusiano mzuri na TCRA. Star Media (Tanzania) Limited itaendelea kuwapatia wateja wake huduma nzuri za luninga pamoja na kusaidia maendeleo ya tasnia ya luninga nchini Tanzania.
 
Mbona sijaona ulichoeleza hapa. Ninavyojua ni kuwa inatakiwa chaneli zilizoainishwa na TCRA zionyeshwe bure - yaani bila kulipia.

Hayo maelezo yako ni marefu na ya kuchanganya.

Hata bila kununua kingamuzi chenu cha Star time. FTA zimekuwepo miaka nenda rudi.

kwanini ninunue king'amuzi chenu chenye picha hafifu kupata FTA?

FTA channel zilizopo zina ubora wa hali ya juu kwenye ving'amuzi vya FTA ambazo zipo tangu miaka mingi na sivyo vyenu ambavyo mnablock chaneli na mnatubadilishia kila kuchao.

Njoo upya na maelezo yaliyonyooka. TUNATAKA ZILE CHANNEL ZA FREE WALIZOSEMA TCRA ZIONEKANE .Siyo hiyo Ngojera.
 
FTA mbona zipo siku zote, hakuna jipya hapa. Tunachojua TCRA walisema local channel zote zinatakiwa zioneshwe bure. Imekuwaje mmekuja na ngonjera nyingine? Huu sio mpango mwingine wa kupiga hera.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU CHANELI ZA BURE (FTA)
presstz.net

INAFAHAMIKA vizuri kwamba televisheni zote za kianologia zilizimwa tangu Januari 1, 2013 nchini Tanzania. Na kwa miaka iliyofata, urushaji wa matangazo na vipindi vya ndani ukabadilika kuwa wa mifumo ya kidigitali hivyo kufanya ongezeko kubwa katika maudhui na vipindi. Star Media (Tanznaia) Limited, moja ya kampuni kubwa za kidigitali zenye vibali (MUX), inafuata maono na mpango wa kuhakikisha kila familia ya kitanzania inapata huduma ya luninga za kidigitali ambayo wanaweza kumudu kutazama. Star Media (Tanzania) Limited ndiyo kampuni iliyotengeneza na kuendesha huduma kubwa zaidi ya matangazo ya kidigitali, huku ikirusha matangazo ya zaidi ya chaneli 20 za ndani. Jitihada zote hizi zilifanya uhamiaji kwenye mifumo ya kidigitali kuwa rahisi, na vipindi vingi vya ndani vimeweza kuonyeshwa.

Hata hivyo, kutokana na mawasiliano hafifu na wateja pia kutofafanua vizuri juu ya bidhaa zetu, kumekuwa na baadhi ya mambo kuhusu luninga za kidigitali ambayo hajaeleweka vizuri. Jitihada zaidi inabidi zifanyike katika kuwaelewesha kuhusu matangaazo ya kidigitali. Hasa upande wa chanelii za Bure (FTA), inahitaji kuelezewa kama ifuatavyo:
1: Watumiaji wote wanaweza kununua dikoda za FTA kwa bei ya kuuzia ambayo ni Tsh 89,000 kwenye maduka yetu na kwa mawakala wa Star Media (Tanzania) Limited, kama zinavyoonekana kwenye picha ya kwanza. Baada ya kununua dikoda ya aina hiyo wateja wanaweza kutazama chaneli za Bure bila kulipia malipo ya kila mwezi. Watapata chaneli kuanzia 6 hadi 16 (Inategemea na sehemu ambapo kibali cha mwenye maudhui kinaruhusu). Hii pia ni hatua ambayo inayofatwa na Star Media (Tanzania) Limited kama kampuni yenye kibali (MUX).
2: Dikoda ya Kulipia inaweza kununuliwa kwenye maduka yetu na mawakala, kama inavyooneshwa kwenye kielelezo namba 2 hapo chini, dikoda hizi zina tozo ndogo ambayo watumiaji wanaweza kununua kwa gharama nafuu kisha wanalipia ada ya mwezi ili kutazama chaneli za bure za Nyumbani , na pia kutamzama chaneli nyingi zaidi za kimataifa na nyinginezo za nyumbani za kulipia. Gharama ya dikoda hii ni Shilingi 45000/=
3: Watumiaji pia wanao uwezo wa kuchagua dikoda nyingine tofauti kulingana na mahitaji yao. Pia kama mtumiaji aliyechagua dikoda ya kulipia akitaka kurudi/kubadilisha apate chaneli za bure sawasawa na mahitaji yake anaoweza kulipia tofauti ya gharama ambayo ni shilingi 44000 katika maduka yetu. Na baada ya hapo anaweza kutazama chaneli za bure.
Star Media (Tanzania) Limited itaendelea kufanya kazi kisheria, bega kwa bega na TBC pia itaendeleza uhusiano mzuri na TCRA. Star Media (Tanzania) Limited itaendelea kuwapatia wateja wake huduma nzuri za luninga pamoja na kusaidia maendeleo ya tasnia ya luninga nchini Tanzania.
Uongo na siasa si nzuri kwenye biashara, nyie mnatuuzia shilingi elfu zrobaini ili chaneli hizo zipatikane kwenye dekoda hizohizo mnazozikana. Sh.86,000/= kwenu nyie ni sawa na pipi lakini sisi mnaotutupia laeama ya kutotoa ushirikiano mzuri ni pesa. Ninaishauri TCRA ichukuwe hatua kali dhidi yenu kwani mnataka tuingie gharama za kijinga na tubaki na dikoda za kuchezea gemu. Startimes msiamini watanzania wrote ni wajinga hawajui elekitronikisi.
 
Wezi tu hawa wanataka tukanunue tena dekoda zingine, issue ni moja tu. Channel zote za bure ziwe bure kwa kingamuzi chao bila masharti zaidi na sio vinginevyo otherwise waliwa kama service provider wapigwe fain ya kutosha iwe fundisho
 
Walivyotaja neno TBC moja kwa moja nikajua hao ni WEZI.
nawakubali sana hawa Jamaa tatizo watanzania tunapenda vyabure kupitiliza ! we umepewa option ya kuchagua decoder bado mnalalamika km unaona ghali kanunue dish kubwa cyo kulalamika
 
Sijaelewa
Aliyeelewa naomba anieleweshe maana nikiwanukuu tcra nachanganyikiwa
Ni kwamba wana ving'amuzi vya akina mbalimbali.
Kimojawapo wamekifanyacha chaneli za Bure tu,ambacho kinauzwa bei juu
85000 ambacho ukishanunua unaangalia Chanel Burr bila kulipia kwa mwezi.
Kisha kipo cha kulipia kwa mwezi,bei ya 44000
 
Back
Top Bottom