Hatimaye rushwa imeshindwa Same Magharibi sasa Kutimkia ACT-Wazalendo

Hatimaye rushwa imeshindwa Same Magharibi sasa Kutimkia ACT-Wazalendo

Crashwise

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Posts
22,227
Reaction score
8,760
Jina la Criss Mbajo limepitishwa kama Mgombea wa ukawa jimbo la Same Magharibi na kuenguliwa kwa Jonas Kadeghe aliyetumia rushwa kwenye chaguzi za ndani na baadae wajumbe kupeleka ushahidi kamati kuu.

Watu wote wanaoipenda Chadema hivi ni vitu vya kuwapongeza viongozi Wetu Kwa kufanya maamzi haya mazuri, Binafsi nikipongeze chama changu cha Chadema hakika kinajitofautisha na CCM kuwa ukibainika umetumia rushwa hawatasita kukung'oa, nikiombe tu kiendelee kumlika kote nchini na Ngazi zote tusije kuwa na wagombea kama akina Nape ambao jumla ya wapiga kura ni pungufu ukilinganisha na waliompigia kura ukimuuliza yeye atakwambia ni goli la mkono Chadema hatutaki magoli ya mkono tunaikata hiyo mikono.

Jonas Kadeghe Aliwasafirisha, akawalisha, akawanywesha, akawapa mlungula na kuwalaza katika guest house za Kindoroko, Kamwala na Herena na asubuhi supu na chapati katika mgahawa wa Casablanca hapohapo Same mjini pia aliwafunga kwa kiapo cha kipare maarufu kama "Mma" ili wasijemgeuka mapatano yao.

Alishirikiana na Katibu wa zamani wa Jimbo Mudy Mnandi maarufu kama Mudy Alone na Mwenyekiti wa Bawacha Jimbo Phillipina Msoffe na Katibu wake, Pia katibu mwenezi wa Jimbo Tunzo Samuel na Wajumbe wa Kamati Tendaji Mbazi Mitango ambaye pia ni Mwenyekiti wa kata ya Suji na Lukio ambaye pia ni Katibu wa Kata ya Chome..

Pia Kamanda Japhet Noah Kaimu Mwenyekiti wa Kata ya Hedaru ambaye alishiriki kiasi kikubwa kuwarubuni wajumbe kutoka kata yake, Kata ya Mabilioni na kata mpya ya Saweni ambayo hata hivyo wajumbe wake walikataliwa kwa sababu walisimikwa uongozi bila taratibu ili kulinda maslahi ya Bwana Kadeghe..

Ninavyoandika muda huu huyo Kadeghe, Mudy Alone na Filipina Msoffe wanamobilize wapambe wao eti waandamane kupinga maamuzi ya kamati kuu na wapo Mbioni kutimkia ACT, swala hili Luna Tanana kabisa na swala la Itilima Simiyu baadaya jina la Magile kupitishwa na jina la Makonda kuondolewa Kwa kununua wajumbe...

Hongera CC ya Chadema lazima tujitofautishe na magama kwamba ukibainika ndani ya Chadema kuwa ulitumia rushwa utakatwa tu...


IMG-20150819-WA0039.jpg
HUU NI UTHIBITISHO MWINGI WA UHUNI WA KADEGHE BAADA YA KUONA AMEFANYA UHUNI NA KUTUMIA RUSHWA ALIJUA ATAKATWA HIVYO KABLA YA CC HAIJAPITISHA MAJINA YEYE AKAENDA KUCHUKUA FOMU...
 
Tunaposema Chadema ni mpango wa Mungu tunaimanisha Hatulei yale mambo ya ccm hapa
 
Mwambie jamaa kuwa unamtegemea kwenye kampeni na muda huu akusaidie....umoja ndio nguvu.Lengo letu ni kuondoa ccm tukiwa wamoja
 
Ufisadi chadema ndiyo nyumbani kwake honganeni tu.
 
Itakua alitoa mpunga kidogo ndio maana mmepiga chini, Ukawa sasa hivi bila dau kubwa huendi popote
 
Mnakanyaga demokrasia mukibanwa mnasingizia rushwa, rushwa ni kosa la jinai kwa nini musiihusishe PCCB na kumfungulia mashtaka kama kweli!?
Kujuana, na upendeleo wa wazi ndio utaowangamizeni.
 
Mnakanyaga demokrasia mukibanwa mnasingizia rushwa, rushwa ni kosa la jinai kwa nini musiihusishe PCCB na kumfungulia mashtaka kama kweli!?
Kujuana, na upendeleo wa wazi ndio utaowangamizeni
Hatufanyi mambo ya Ccm huku Chadema wewe
 
CCM ipi unayoizungumzia au ile iliyowapatia Mgombea Urais!?
 
Safii,natumaini at a jumbo la Nkenge misenye watatumia busara,
 
Safii,natumaini at a jumbo la Nkenge misenye watatumia busara,

Hakuna busara inayokanyaga haki za wengine, na kama ujinga huu uliofanywa kwenye jimbo hili ni busara basi busara haifahamiki uko CHADEMA
 
Back
Top Bottom