Hatimaye Rais Kabila akubali kuachia madaraka.

Hatimaye Rais Kabila akubali kuachia madaraka.

Freed Freed

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2017
Posts
6,851
Reaction score
7,764
Habari wadau.

Rais Joseph kabila wa Congo DRC amekubali kuachia madaraka Mara tu baada ya uchaguzi kufanywa 23/12/2018. Amesema uchaguzi utafanyika kama ulivyopangwa na hautasogezwa tena.

Hayo yamesemwa na waziri wa habari wa Congo Lambert Mende Omulanga. Waziri kusema saivi tume ya uchanguzi inamalizia zoezi la mwisho la usajili wa wapiga kura.

Pia emedai kabila atataja mwenyewe nani ktk chama chake agombee ambaye ndiye atakuwa mrithi wake wa Urais akishinda uchaguzi.

Hili la kusema atataja mwenyewe limenishutua kuwa demokrasia ya kumpata ipo nchini ya kabila na sio wana chama.

Source: VOA
 
Hawa dawa yao ni kuwakimbiza kwa mtutu tu, ukiwabembeleza wanazidi ota mapembe.
 
Atamtaja yeye.? Inatakiwa uwe na akili mbovu kuelewa hili kuwa bado atai control yeye serikali
 
Ningeshangaa kuona analishinda nguvu Kanisa Katoliki...!
 
'Ataje mwenyewe mgombea ili awe mrithi wake' na sio chaguo la wananchi.

Ndio kuachia madaraka huko?!

Africa, we still have a long way to go..
 
Mi nilidhani kasema anaachia in "45 days" kama alivyoonywa na former general. December mbali mno na bila shaka anaweza kuibuka na single nyingine
 
Kwanini ataje mwisho wa mwaka? Anazani disemba haitafika.. Ikifika atasema mwakani
 
Yale yale tu kama atachagua mwenyewe mrithi wake
 
Back
Top Bottom