Hatimaye nimemjua niliyetaka kumjua. Je, nini nifanye?

Aiseeeee Inahitaji kiwa na roho ya chuma kadri unavyokua na amini binadamu ni eviiiil sana,usimuone mwenzio km malaika
 
Kosa lako ni kuoa mwanamke anayekuzidi elimu pamoja na kukuzidi kiuchumi
 
Ndugu zangu habari zenu.

Naomba niwaombe ushauri juu ya kilichonitokea........

Nilimaliza chuo miaka minne iliyopita. Kama unavyojua maisha yanavyokuwa magumu mtaani baada ya maisha ya chuo. Nilituma maombi sehemu mbalimbali ila kote niliambulia patupu. Hata hivyo sikukata tamaa. Nikaendelea kulanda huku na kule na mwishowe nikapata kazi kwenye kampuni fulani ya magazeti nikiwa kama mchora katuni ( Cartoonist).

Kwenye kampuni ndo nilipokutana na huyu mwanamke ninayeishi naye. Tulifunga ndoa mwaka jana mwanzoni kabisa. Huyu dada alikuwa mpole mno tena mwenye heshima na hekima kima. Kubwa zaidi ni mzuri mno kiasi kwamba kuna kipindi hadi nilikuwa naona kama nimebahatisha kumpata.

Mke wangu huyu kwao maisha ni mazuri tu tofauti na mimi Katuni. Kielimu simpati na hata, kifedha simpati. Nilichoshukuru ni kwamba alikuwa ananipenda mno na niliamini hivyo siku zote. Kwa upande wangu pia nilimpenda sana na nitaendelea kufanya hivyo.Tuliishi kwa upendo furaha na amani.

Lakini, baadaye taratiibu nikaanza kuona anabadilika. Alizidisha sana wivu kwangu kiasi kwamba hadi nikaanza kero. Cha ajabu sasa, akawa hataki tushiriki tendo la ndoa. Sasa ikawa tunaenda wote kazini mguu kwa mguu na tunarudi wote. Tukiwa nyumbani alipenda sana kukaa na simu yangu ila yake nikikaa nayo kwa dakika tu huja kuichukua. Kazini akiona naongea na mfanyakazi wa kike basi lazima atakuja na kujipitisha.

Ana wivu sana ila tendo kufanya hataki. Nikajiuliza ana nini huyu mwanamke. Baadaye nikasema aaah! ndo wanawake walivyo bhana nikaamua kutulia tu. Lakini akazidi kubadilika. Sasa hata heshima yake kwangu ikaanza kushuka. Nikaja humu jf kwa fake ID na nikaanzisha thread kuomba ushauri na wengi mkanishauri hadi PM.

Katika kipindi hicho simu ya mke wangu nikawa siigusi kabisa. Yaani qlikuwa hataki kabisa. Hii iliniumiza sana kichwa. Nilijiuliza ina nini kwani ile simu?.

Nilikuja humu jf nikaomba kuambiwa au kupatiwa program ya kuweza kuona sms zinazoingia kwenye simu nyingine pasipo mwenye simu kujua. Watu waliniponda sana nakumbuka. Wengine wakasema sijui eti najitafutia kufa kwa presha. Mengi sana yalisemwa ya kunivunja moyo hata hivyo sikufa moyo. Kuna humu jf ni mtaalamu sana wa maswala mbalimbali ya technolojia akaniambia program za kumSPY mtu zipo ila upatikanaji wake ni mgumu mno maana app nyingi ni FAKE au PRANK na ni bora nitafute za kulipia.

Kabla sijaanza mchakato nikaona tangazo kwenye group moja la wana IT lililohusu WhatsappSPY. Nikaichukua ile namba na kuisevu kisha nilipopata muda nikawasiliana nao wakaniambia kwanza niwatumie pesa elfu ishirini ndipo wanipe hiyo program. Niliona hapa kuna harufu ya kutapeliwa lakini nikasema potelea mbali. Nikatuma pesa. Wakanitumia link nikaidownload hiyo program. Wakanipa maelekezo jinsi ya kuiset. Sasa shida iliyotokea ni kwamba, hiyo program ili ifanye kazi natakiwa niichukue simu ya mke wangu kisha niifanyie kitu fulani hivi. Ukizingatia hapo simu yenyewe ya mke huwa hataki niiguse ningefanyaje na pesa tayari jamaa nishawatumia kwenye namba yao. Daaah! ilikuwa ngumu sana kuipata simu yake ila sikufa moyo niliamua kutumia kila mbinu. Mwishowe nilifanikiwa. Niliamka usiku wa kama saa nane hivi. Yeye alikuwa kalala. Nikaichukua simu yake nikafanya kama nilivyoelekezwa. Kisha nikairudisha ilipokuwa.

Asubuhi kama kawaida tukaenda zetu kazini. Nilipotulia baada ya kupata chakula cha mchana nikaamua kuifungua ile program. Nilichokikuta kwakweli sikuamini. Nilikuta sms zake zote. Alikuwa ana magroup kadhaa ya ajabu ajabu ( ya kikubwa ). Mbaya zaidi kumbe alikuwa akitembea na mwanamke mwenzake. Yaani zile sms zilionyesha kabisa kwamba hawa ni wapenzi na wote ni wanawake. Ukizingatia huyo mwanamke anayetembea nae ninamfahamu hadi anapoishi. Ni rishangingi la mjini hilo li mama. Linaniharibia ndoa yangu. Muda mwingi wanachat na kutumiana picha na video za ajabu ajabu. Yote wanayoyaongea ni ushetani mtupu. Wakipigiana simu kwa whatsapp kama nikiwa online nawasikia kila wanachoongea.

Wakuu nishamjua anayeniharibia ndoa yangu. Je nini nifanye ili niokoe jahazi.

( Kwa kweli ndugu zangu nimeamini kama una presha hizi program za kuona sms za mtu mwingine usiziguse kabisa)

UPDATES : Ndugu zangu, kuna watu mnakuja pm eti niwatumie link. SASA LINK MIMI NAIPATA WAPI. Mimi mwenyewe nilitumiwa nikadownload then nikafuta link maana jamaa walioniuzia waliniambia link ikikaa kwenye simu kwa zaidi ya saa 24 huaribu simu kwamba itachange na kuwa virus. SO SINA LINK WAKUU

CHUKUA MKEO MPELEKE KWA WAZAZI WAKE NA UMWAMBIE UNASIKIA KUWA NI MSAGAJI KWA HIYO UNAMUOMBA AACHE HIYO TABIA AKIKUBISHIA NA KUJIFANYA UMEMUONEA VUNJA BUYU WEKA KILA KITU HADHARANI KWA MANUFAA YA NDOA YAKO TOFAUTI NA HVYO UFICHE USIFICHE NDOA IKO MASHAKANI BORA LAWAMA KULIKO FEDHEHA NA KAMA NOMA NA IWE NOMA. BADO MMOJA NAFUTIKA.
 
We mwambie umelala umeota kuwa anafanya hiyo shughuli ya usagaji sasa muulize je ni kweli
 
Nakumbuka thread ya kuuliza hili la ku spy.

Pole na yaliyokukumba. Kama anasoma humu basi atakuwa kashajua, labda kama umebadili mengine juu yako uliyoyaandika.
 
Kuna njia moja tu, ambayo ndio itakusaidia wewe, mkeo, ndoa na future yenu kwa ujumla.

Nayo ni Deliverance.


Your wife must be delivered from tht evil spirit.


Hakuna njia wala namna nyingine zaidi ya mkeo kufanyiwa deliverance.
 
Ushauri wangu kwanza usije mwambia information vipi umezipata.
Kwa sababu Utakuja kushindwa baadaye kufanya uspy wako.

La pili muite mkeo kaa nae faragha, Muulize huyo mtu ni nani na imekuwaje wakawa na uhusiano,mkatie live hayo maneno, halafu siku ambayo itakayo mwambia, mfanyie surprised asijue what's going on. Ili umshtue uwone atakavyo piga goti.

Jengine utakapo yajadili hayo usije ukawa weak, lazima uwe kidume, usiwe mtu rahisi kuombwa radhi ya dakika moja, hapo atakuona bwege, akikubali kosa weka bit kama week very seriously Au zaidi.

Jengine ukubali mawili aidha hio ndoa kuwa mwanzo wamabadiliko au mwisho wa ndoa. Jiandae kupokea, usiogope ndio systems ya ndoa.

Think like a man, don't be afraid
 
Kweli wajinga wengi yaani mnashindwa kuelewa lengo la thread mnaiamini hii story
 
Huyu jamaa ni dalali.
Alikuwa na mchora katuni akamtafutia Nazi huku.
Kaletewa app ya MTU,anaidalalia.
 
hapo tulia tu, jiandae kwa mazoezi na mlo wa uhakika,

halafu anza kupiga show za uhakika! hamna dawa zaidi ya show za uhakika
 
Huyu jamaa ni muongoooo tapeliii hamna kitu kama hicho Anataka kutake attention ya watu ili awatapeli kweny hiyo app wanaoipa promo


Amesema hiyo link yeye hana alishafuta coz ikikaa masaa 24 inaleta virus kutokana na maelezo yake!!
 
Jamaa mjanja sana. Si ajabu sasa PM yake imejaa watu wamepanga mistari kutoa 20,000 Tshs ili wapatiwe link ya hiyo program. Utapeli wa kiwango cha juu kabisa. Safi sana mdau na lazima kuna watu utawapiga tu kwa sababu hakuna namna. Halafu unakuta jitu bila aibu linakuja hapa tena ooh nimetapeliwa 20,000 kwa kuuziwa link feki ya program ya udukuzi wa simu. Hovyo kabisa !!!
Na siku akitokea mtu humu akalalamika katepeliwa na huyu jamaa naomba MOD watumie nafasi yao kumpiga ban alietapeliwa
 
Back
Top Bottom