katuni
Senior Member
- Dec 8, 2012
- 151
- 77
Ndugu zangu habari zenu.
Naomba niwaombe ushauri juu ya kilichonitokea........
Nilimaliza chuo miaka minne iliyopita. Kama unavyojua maisha yanavyokuwa magumu mtaani baada ya maisha ya chuo. Nilituma maombi sehemu mbalimbali ila kote niliambulia patupu. Hata hivyo sikukata tamaa. Nikaendelea kulanda huku na kule na mwishowe nikapata kazi kwenye kampuni fulani ya magazeti nikiwa kama mchora katuni ( Cartoonist).
Kwenye kampuni ndo nilipokutana na huyu mwanamke ninayeishi naye. Tulifunga ndoa mwaka jana mwanzoni kabisa. Huyu dada alikuwa mpole mno tena mwenye heshima na hekima kima. Kubwa zaidi ni mzuri mno kiasi kwamba kuna kipindi hadi nilikuwa naona kama nimebahatisha kumpata.
Mke wangu huyu kwao maisha ni mazuri tu tofauti na mimi Katuni. Kielimu simpati na hata, kifedha simpati. Nilichoshukuru ni kwamba alikuwa ananipenda mno na niliamini hivyo siku zote. Kwa upande wangu pia nilimpenda sana na nitaendelea kufanya hivyo.Tuliishi kwa upendo furaha na amani.
Lakini, baadaye taratiibu nikaanza kuona anabadilika. Alizidisha sana wivu kwangu kiasi kwamba hadi nikaanza kero. Cha ajabu sasa, akawa hataki tushiriki tendo la ndoa. Sasa ikawa tunaenda wote kazini mguu kwa mguu na tunarudi wote. Tukiwa nyumbani alipenda sana kukaa na simu yangu ila yake nikikaa nayo kwa dakika tu huja kuichukua. Kazini akiona naongea na mfanyakazi wa kike basi lazima atakuja na kujipitisha.
Ana wivu sana ila tendo kufanya hataki. Nikajiuliza ana nini huyu mwanamke. Baadaye nikasema aaah! ndo wanawake walivyo bhana nikaamua kutulia tu. Lakini akazidi kubadilika. Sasa hata heshima yake kwangu ikaanza kushuka. Nikaja humu jf kwa fake ID na nikaanzisha thread kuomba ushauri na wengi mkanishauri hadi PM.
Katika kipindi hicho simu ya mke wangu nikawa siigusi kabisa. Yaani qlikuwa hataki kabisa. Hii iliniumiza sana kichwa. Nilijiuliza ina nini kwani ile simu?.
Nilikuja humu jf nikaomba kuambiwa au kupatiwa program ya kuweza kuona sms zinazoingia kwenye simu nyingine pasipo mwenye simu kujua. Watu waliniponda sana nakumbuka. Wengine wakasema sijui eti najitafutia kufa kwa presha.
Mengi sana yalisemwa ya kunivunja moyo hata hivyo sikufa moyo. Kuna humu jf ni mtaalamu sana wa maswala mbalimbali ya technolojia akaniambia program za kumspy mtu zipo ila upatikanaji wake ni mgumu mno maana app nyingi ni FAKE au PRANK na ni bora nitafute za kulipia.
Kabla sijaanza mchakato nikaona tangazo kwenye group moja la wana IT lililohusu Whatsapp spy. Nikaichukua ile namba na kuisevu kisha nilipopata muda nikawasiliana nao wakaniambia kwanza niwatumie pesa elfu ishirini ndipo wanipe hiyo program. Niliona hapa kuna harufu ya kutapeliwa lakini nikasema potelea mbali. Nikatuma pesa.
Wakanitumia link nikaidownload hiyo program. Wakanipa maelekezo jinsi ya kuiset. Sasa shida iliyotokea ni kwamba, hiyo program ili ifanye kazi natakiwa niichukue simu ya mke wangu kisha niifanyie kitu fulani hivi. Ukizingatia hapo simu yenyewe ya mke huwa hataki niiguse ningefanyaje na pesa tayari jamaa nishawatumia kwenye namba yao.
Daaah! ilikuwa ngumu sana kuipata simu yake ila sikufa moyo niliamua kutumia kila mbinu. Mwishowe nilifanikiwa. Niliamka usiku wa kama saa nane hivi. Yeye alikuwa kalala. Nikaichukua simu yake nikafanya kama nilivyoelekezwa. Kisha nikairudisha ilipokuwa.
Asubuhi kama kawaida tukaenda zetu kazini. Nilipotulia baada ya kupata chakula cha mchana nikaamua kuifungua ile program. Nilichokikuta kwakweli sikuamini. Nilikuta sms zake zote. Alikuwa ana magroup kadhaa ya ajabu ajabu ( ya kikubwa ).
Mbaya zaidi kumbe alikuwa akitembea na mwanamke mwenzake. Yaani zile sms zilionyesha kabisa kwamba hawa ni wapenzi na wote ni wanawake. Ukizingatia huyo mwanamke anayetembea nae ninamfahamu hadi anapoishi. Ni rishangingi la mjini hilo li mama.
Linaniharibia ndoa yangu. Muda mwingi wanachat na kutumiana picha na video za ajabu ajabu. Yote wanayoyaongea ni ushetani mtupu. Wakipigiana simu kwa whatsapp kama nikiwa online nawasikia kila wanachoongea.
Wakuu nishamjua anayeniharibia ndoa yangu. Je nini nifanye ili niokoe jahazi.
( Kwa kweli ndugu zangu nimeamini kama una presha hizi program za kuona sms za mtu mwingine usiziguse kabisa)
UPDATES : Ndugu zangu, kuna watu mnakuja pm eti niwatumie link. SASA LINK MIMI NAIPATA WAPI. Mimi mwenyewe nilitumiwa nikadownload then nikafuta link maana jamaa walioniuzia waliniambia link ikikaa kwenye simu kwa zaidi ya saa 24 huaribu simu kwamba itachange na kuwa virus. SO SINA LINK WAKUU