Hatimaye mapenzi yameniumiza kwa mara nyingine tena!!

Hatimaye mapenzi yameniumiza kwa mara nyingine tena!!

tindikalikali

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Posts
4,854
Reaction score
1,146
Habari wana JF.
Kwa muda mrefu sasa nimekuwa nikitamani kuwa na mahusiano serious ambayo yatapelekea. Kama bahati au mkosi mwezi february mwaka huu kuna binti nilionana naye kituo cha basi na kuvutiwa naye, nilifanikiwa kubadilishana naye namba ya simu baada ya kuongea naye kwa kifupi...baada ya mawasiliano ya karibu takribani mwezi mmoja tulijikuta tumekuwa wapenzi, muda huo mimi nilikuwa Mby na yeye alikuwa Moshi. Tuliendelea kuwasiliana huku akionesha kuwa mtu mwenye mtazamo chanya katika maisha na mimi nilizidi kujiridhisha kwamba atanifaa...

Tatizo lipo hapa...
Mwezi huu tulipanga tuonane either yeye aje au mimi niende, wakati tukiendelea kupanga namna ya kuonana alipata safari ya Dsm, na mimi nikaona vyema nije tu huku na yeye alikubali. Sasa cha ajabu leo nimefika, nimemtafuta ile kukutana akawa anaongea na mimi juujuu akionesha kuwa na haraka, cha ajabu ameniacha njiani kama tapeli fulani hivi, kiukweli imeniuma..niko disappointed sana na ukizingatia safari ilikuwa kwa ajiri yake! Eti yupo na rafiki yake wanaenda kibaha, namuuliza kwanini hakusema mapema hasemi kitu!! Najua mapenzi ni kujitoa kwa kila namna, nilikuwa tayari kwa lolote ili maisha yaendelee ila kwa hii hadi akili imesimama!!

Sijui nifanyeje, nisaidieni wadau maana sijui ni utoto ama kitu gani kinamsumbua (nina 28 na yeye 22)
 
al in al mke mwema anatoka kwa mungu ndo atakupangia c bnadam so uckond
 
al in al mke mwema anatoka kwa mungu ndo atakupangia c bnadam so uckond

Sawa mkuu nimekuelewa..ila inakatisha tamaa sana!! Kwa kinywa chake alikiri kwamba ananipenda!!
 
Poleh bana,rudi tu mbeya jibidishe na kazi,utamsahau aftr a while japo ni ngumu,kama kweli ni wako atakuwa tu,u did ur best mengine achana nayo
 
mke mwema huwa anatoka kwa mungu. embu shukuru kwanza usikute umeepushwa na jambo. siku ya kupata mke ikifika utashangaa mambo yatakavyokuwa yanaenda yenyewe fresh. sali na umuombe mungu akuletee mke mwema.

nakuelewa mkuu!!
 
Poleh bana,rudi tu mbeya jibidishe na kazi,utamsahau aftr a while japo ni ngumu,kama kweli ni wako atakuwa tu,u did ur best mengine achana nayo

sawa ila niliwekeza muda mwingi kwake!!
 
Pole mpendwa ndio shida ukimpenda mtu asiyekupenda anakuwa hajari kabisa kuumia kwako,pole usijari utampata aliye serious kama wewe!
 
Back
Top Bottom