Hatimaye madaktari Dodoma waanza kazi

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
Mgomo wa madaktari katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma umemalizika jana asubuhi baada ya madaktari hao kulipwa madai yao juzi jioni.
Mgomo huo uliosababisha kudorora kwa utoaji wa huduma kwa wagonjwa ulianza Jumanne ambapo uliwashirikisha madaktari 33 ambao wapo chini ya uangalizi.

Madaktari hao waligoma kwa ajili ya kuishinikiza Wizara ya Afya kuwalipa fedha zao za miezi miwili wanazodai.
Madai hayo yalikuwa ya Novemba na Desemba, mwaka jana ambapo fedha za mwezi Novemba, zilitolewa na mfuko wa hospitali hiyo na kuwalipa madaktari hao.

Kutokana na mgomo huo, hospitali hiyo ililazimika kuazima madaktari
kutoka hospitali ya Manispaa ya Makole, Udom na hospitali ya Ifakara iliyopo mkoani Morogoro ili kuweza kuongeza nguvu katika utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

Hata hivyo, kulikuwa na msongamano wa wagonjwa wanaosubiri kupata huduma za afya hospitalini hapo kutokana na hospitali hiyo kuhudumia wananchi wengi wa mkoa huu.

Katibu wa hospitali hiyo, Isaack Kaneno alisema jana kuwa, tayari
madaktari hao wamelipwa madai yao juzi jioni na wameingia kazini kuendelea na kazi zao kama kawaida.

Alisema mgomo huo uliitikisa sana hospitali hiyo kwani wagonjwa walirundikana wodini wakisubiri kuhudumiwa lakini hawakupata huduma kwa muda muafaka.

“Walikuwa wakidai fedha za mwezi moja tu na si miwili kama walivyodai hapo awali na tayari wamelipwa, na wako kazini sasa,” alisema
Alisema baada ya madaktari hao kulipwa, kwa sasa hali ni shwari na ana uhakika hali ya msongamano wa wagonjwa itapungua kwa kiasi kikubwa.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI


 
mgonjwa ankufa mapokezi dr anakunywa valuu,
wazazi wanakufa leba wengine icu.source Roma
 
Vijana hawana source ingine ya mapato viongozi wako viyoyozi wanatoa maamuzi ya kisiasa!!!!!shame on them!
 
Back
Top Bottom