Hatimaye Lugumi atoswa

kamati ya ufundi

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
416
439
  • Ni katika Kashfa ya Bilioni 34 za polisi.
  • Mkakati wa Kumuangushia ‘jumba bovu wakamilika.
  • Waziri Kitwanga na Infosys wajitoa Kiaina.
  • Polisi, Wizara katika wakati Mgumu.

Ni dhahiri sasa kwamba kashfa iliyoibuka hivi karibuni na kuchukua umaarufu mkubwa ya kulitia hasara jeshi la polisi katika zabuni ya kufunga vifaa vya kisasa vya kutambua alama za mikono inaelekea kumuangukia mfanyabiashara Abdallah Lugumi wa Lugumi Enterprises peke yake japo taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa biashara hiyo imekwamishwa na wabia kadhaa ikiwemo kampuni inayohusishwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Gazeti hili limeripoti hapo awali kuwa Rais Magufuli atakutana na mtihani mkubwa wa kutakiwa kufanya maamuzi kama hayo dhidi ya WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ametajwa kushiriki na kukwamisha kwa uchunguzi unaendelea wa mkataba tata baina ya mfanyabiashara Lugumi Enterprises na Jeshi la polisi mkataba ulioipelekea serikali kupitia jeshi hilo kupata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 34 kutokana na kushindwa kukamilika kwa mradi uliohitajika kufanyika.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinasema, kutokukamilika kwa mkataba huo wa kufunga vifaa maalum vya kutambua alama za mikono kunatokana na kushindwa kukamilika kwa uunganishaji wa kimtandao wa mawasiliano (internet) kama makubaliano ya mkataba yanavyosema.

Katika makubaliano ya mkataba huo ambayo gazeti hili limeuona, kampuni ya lugumi ilitakiwa kufunga vifaa hivyo katika vituo mbalimbali vya polisi vilivyo nchi nzima ili viweze kutambua alama za watuhumiwa na kuimalisha ulinzi.

Katika kufanikisha zoezi hilo, kampuni ya Lugumi inadaiwa kuwa iliipa mkata shirikishi (Sub-contract) kampuni ya INfosis limited ili iweze kukamilisha kipengele cha uunganishaji wa mtandao yaani intanet.

lugumi.jpg

Taarifa za uhakika zaidi zinasema kampuni hiyo yenye ofisi zake maeneo ya kinondoni Ada estate kwa kipindi kirefu imekuwa ikimilikiwa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi bwana Charles Kitwanga pamoja na mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa Dk. Modestus Francis Kipilimba na kwamba wawili hao wameanza kuwa wabia wa kampuni hiyo tangu wakiwa wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT) .

Taarifa hizo zinaeleza kuwa mara baada ya kampuni ya lugumi kukamilisha kukabidhi vifaa hivyo kama ilivyokubaliwa na kuhitajika, kampuni ya Infosis ilipaswa kuviunganisha vifaa hivyo na mtandao ili vianze kazi jambo ambalo kampuni hiyo inayomilikiwa na waziri huyo wa mambo ya ndani ya nchi haikuweza kukamilisha lakini ilipokea malipo yote waliyopaswa kulipwa na serikali kupitia jeshi la polisi bila wasiwasi wowote.

Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anayehusika kupitia kampuni yake hiyo ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo amefanya jitihada kadhaa ikiwemo za kukutana na mfanyabiashara lugumi ili kuyamaliza mambo hayo huku akihaha kulihamisha suala hilo kutoka kamati ya PAC kwenda katika kamati inayohusika na masuala ya ulinzi na usalama ili lisijadiliwe kwa mapana.

Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa vilivyokamilika.

Pamoja na Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona kuonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilipewa kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa ,jambo la kushangaza ni kwamba mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.

Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.

Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika.

Kujihushisha kwa kampuni hiyo inayodaiwa kumilikiwa na waziri huyo na swahiba yake aliyemteua kuwa mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho NIDA kufanya biashara na serikali ikiwemo hiyo ya kufunga vifaa hivyo, kunamuondolea waziri huyo sifa za kuwa kiongozi wa umma kwa kuwa ameweza kufanya biashara na serikali ambayo tangu awamu ya nne amekuwa sehemu ya serikali hiyo.

Sambamba na hapo, kitwanga anaanza kwa mara ya kwanza kumuweka Rais magufuli katika wakati mgumu wa ama kumuondoa ama kubakl naye kutokana na ukweli kwamba wawili hao kwa kipindi kirefu sasa wamekuwa na urafiki karibu sana kupita hata ule wa Lowassa na Kikwete.

Taarifa za uhakika zinasema, kama Magufuli ataamua kuchukua hatua kuthibitisha msimamo wake wa kutokumuangalia mtu usoni, basi kitwanga hapaswi tu kuenguliwa uwaziri, bali pia anatakiwa kufikishwa mahakani kwa ubadhirifu na udanganyifu huo alioufanya.

Wadau mbali mbali wa masuala ya kimaendeleo, wamehoji kama kweli Rais Magufuli alifanya utafiti wa kina juu ya makando kando ya watendaji wake hasa mawaziri na kujiridhisha na usafi wao kabla ili kuepukana na hajawateua ili kuepukana na tuhuma za namna hii.

Kampuni hiyo ya Infosys inayotajwa kumilikiwa na waziri kitwanga na mkurugenzi mtendaji wa NIDA inatajwa kuwa ni miongoni mwa makampuni yaliyoshiriki kuomba zabuni za utengenezaji wa vitambulisho vya uraia zabuni ambayo hata hivyo hawakuipata.

Mpaka sasa wamiliki wawili wa kampuni hiyo mmoja ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mwengine ni mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho NIDA.

Juzi mmoja wa viongozi waandamizi wa kampuni hiyo ya Infosys alizungumza na wanahabari na kukana kumtambua waziri kitwanga kama mbia huku akisema kuwa alishiriki tu kuiasisi kampuni hiyo na kujitoa kuendesha tangu mwaka 2010.

Chanzo: Jamvi la Habari
 
Kupelekwa TAKUKURU ni kumsaidia ashinde tuhuma, maana TAKUKURU haijawahi shinda kesi dhidi ya mtuhumiwa. Atakuwa huru baada ya kufikishwa mahakamani.
 
Majumba mazuri, magari ya bei kubwa na ya kifahari utafikiri wanafanya biashara ya akili kumbe majizi tu
 
AoPFblCdhxfLeQRh1gQbkW7cjrG1fcwBd6iRDOHVNHc7.jpg

Ni katika Kashfa ya Bilioni 34 za polisi.

Mkakati wa Kumuangushia ‘jumba bovu wakamilika.

Waziri Kitwanga na Infosys wajitoa Kiaina.

Polisi, Wizara katika wakati Mgumu.

Na Mwandishi Wa JAMVI LA HABARI.

Ni dhahiri sasa kwamba kashfa iliyoibuka hivi karibuni na kuchukua umaarufu mkubwa ya kulitia hasara jeshi la polisi katika zabuni ya kufunga vifaa vya kisasa vya kutambua alama za mikono inaelekea kumuangukia mfanyabiashara Abdallah Lugumi wa Lugumi Enterprises peke yake japo taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinaonyesha kuwa biashara hiyo imekwamishwa na wabia kadhaa ikiwemo kampuni inayohusishwa na waziri wa mambo ya ndani ya nchi.

Gazeti hili limeripoti hapo awali kuwa Rais Magufuli atakutana na mtihani mkubwa wa kutakiwa kufanya maamuzi kama hayo dhidi ya WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ambaye ametajwa kushiriki na kukwamisha kwa uchunguzi unaendelea wa mkataba tata baina ya mfanyabiashara Lugumi Enterprises na Jeshi la polisi mkataba ulioipelekea serikali kupitia jeshi hilo kupata hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 34 kutokana na kushindwa kukamilika kwa mradi uliohitajika kufanyika.

Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili linazo zinasema, kutokukamilika kwa mkataba huo wa kufunga vifaa maalum vya kutambua alama za mikono kunatokana na kushindwa kukamilika kwa uunganishaji wa kimtandao wa mawasiliano (internet) kama makubaliano ya mkataba yanavyosema.

Katika makubaliano ya mkataba huo ambayo gazeti hili limeuona, kampuni ya lugumi ilitakiwa kufunga vifaa hivyo katika vituo mbalimbali vya polisi vilivyo nchi nzima ili viweze kutambua alama za watuhumiwa na kuimalisha ulinzi.

Katika kufanikisha zoezi hilo, kampuni ya Lugumi inadaiwa kuwa iliipa mkata shirikishi (Sub-contract) kampuni ya INfosis limited ili iweze kukamilisha kipengele cha uunganishaji wa mtandao yaani intanet.

lugumi.jpg

Taarifa za uhakika zaidi zinasema kampuni hiyo yenye ofisi zake maeneo ya kinondoni Ada estate kwa kipindi kirefu imekuwa ikimilikiwa na Waziri wa mambo ya ndani ya nchi bwana Charles Kitwanga pamoja na mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho vya taifa Dk. Modestus Francis Kipilimba na kwamba wawili hao wameanza kuwa wabia wa kampuni hiyo tangu wakiwa wafanyakazi wa benki kuu ya Tanzania (BOT) .
Taarifa hizo zinaeleza kuwa mara baada ya kampuni ya lugumi kukamilisha kukabidhi vifaa hivyo kama ilivyokubaliwa na kuhitajika, kampuni ya Infosis ilipaswa kuviunganisha vifaa hivyo na mtandao ili vianze kazi jambo ambalo kampuni hiyo inayomilikiwa na waziri huyo wa mambo ya ndani ya nchi haikuweza kukamilisha lakini ilipokea malipo yote waliyopaswa kulipwa na serikali kupitia jeshi la polisi bila wasiwasi wowote.

Taarifa za kuaminika ilizozipata gazeti hili, zimeeleza kuwa Waziri Kitwanga anayehusika kupitia kampuni yake hiyo ya Infosys anayomiliki pamoja na Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), iliyo chini ya Wizara hiyo hiyo amefanya jitihada kadhaa ikiwemo za kukutana na mfanyabiashara lugumi ili kuyamaliza mambo hayo huku akihaha kulihamisha suala hilo kutoka kamati ya PAC kwenda katika kamati inayohusika na masuala ya ulinzi na usalama ili lisijadiliwe kwa mapana.

Kampuni hiyo ililipwa sh. bilioni 34 na jeshi la polisi ili kusambaza vifaa hivyo nchi nzima katika vituo 138 vya polisi lakini ni vituo 14 vilivyopata vifaa vilivyokamilika.

pamoja na Nyaraka za uchunguzi ikiwemo mkataba kati ya kampuni ya Lugumi na Infosys ambazo gazeti hili imeziona kuonyesha kuwa Kampuni hiyo ya Waziri Kitwanga ilipewa kazi ya kuunganisha internet kati ya vituo vya polisi na mkonga wa taifa ,jambo la kushangaza ni kwamba mpaka sasa ni vituo 14 tu vya polisi viliunganishwa, ambapo baadhi ya taarifa ilizozipata gazeti hili zilionyesha kuwa moja ya taarifa ya ukaguzi inaonekana Marijani Saleh alisaini kufikisha vifaa vya Infosys.

Vifaa hivyo, vinaelezwa vilifikishwa Machi 2, 2012. Katika Nyaraka hiyo upande wa Jeshi la Polisi alisaini ofisa mmoja wa Polisi aliyejulikana kwa jina la Nestory Tagaya na mdau mwingine kutoka kampuni ya BioLink alikuwa Pierson J.

Taarifa iliyotolewa na PAC hivi karibuni ilionyesha kuwa kampuni ya Lugumi ilingia mkataba na Jeshi la Polisi mwaka 2011, kwa kazi hiyo ya kufunga mitambo hiyo kwenye vituo vya Polisi vya wilaya nchi nzima na kulipwa fedha zote huku kazi ikiwa haijafanyika.

Kujihushisha kwa kampuni hiyo inayodaiwa kumilikiwa na waziri huyo na swahiba yake aliyemteua kuwa mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho NIDA kufanya biashara na serikali ikiwemo hiyo ya kufunga vifaa hivyo, kunamuondolea waziri huyo sifa za kuwa kiongozi wa umma kwa kuwa ameweza kufanya biashara na serikali ambayo tangu awamu ya nne amekuwa sehemu ya serikali hiyo.

Sambamba na hapo, kitwanga anaanza kwa mara ya kwanza kumuweka Rais magufuli katika wakati mgumu wa ama kumuondoa ama kubakl naye kutokana na ukweli kwamba wawili hao kwa kipindi kirefu sasa wamekuwa na urafiki karibu sana kupita hata ule wa Lowassa na Kikwete.

Taarifa za uhakika zinasema, kama Magufuli ataamua kuchukua hatua kuthibitisha msimamo wake wa kutokumuangalia mtu usoni, basi kitwanga hapaswi tu kuenguliwa uwaziri, bali pia anatakiwa kufikishwa mahakani kwa ubadhirifu na udanganyifu huo alioufanya.

Wadau mbali mbali wa masuala ya kimaendeleo, wamehoji kama kweli Rais Magufuli alifanya utafiti wa kina juu ya makando kando ya watendaji wake hasa mawaziri na kujiridhisha na usafi wao kabla ili kuepukana na hajawateua ili kuepukana na tuhuma za namna hii.

Kampuni hiyo ya Infosys inayotajwa kumilikiwa na waziri kitwanga na mkurugenzi mtendaji wa NIDA inatajwa kuwa ni miongoni mwa makampuni yaliyoshiriki kuomba zabuni za utengenezaji wa vitambulisho vya uraia zabuni ambayo hata hivyo hawakuipata.

Mpaka sasa wamiliki wawili wa kampuni hiyo mmoja ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi na mwengine ni mkurugenzi wa mamlaka ya vitambulisho NIDA.

Juzi mmoja wa viongozi waandamizi wa kampuni hiyo ya Infosys alizungumza na wanahabari na kukana kumtambua waziri kitwanga kama mbia huku akisema kuwa alishiriki tu kuiasisi kampuni hiyo na kujitoa kuendesha tangu mwaka 2010.
January Makamba amekula Tenda ya kuleta Wachakachuaji wa mikataba na kamati za Ufundi toka Gambia , hivyo kilichofanyika hapo ni mbinu za kumsafisha Kitwanga ili akimbie kutumbuliwa JIPU .
 
Majipu kila kona.... kama kweli mkurugenzi wa sasa wa NIDA ni katika wamiliki wa Infosys na kama kweli Infosys iliomba tenda kutengeneza vitambulisho vya NIDA wakakosa.... na kwa sbb Kitwanga ndo waziri wa wambo ya ndani na mmoja wa wamiliki wa infosys..... ina maana Infosys imeingia NIDA kwa mgongo wa nyuma na hii ina leta maswali mengi zaidi ya majibu......
 
Mikataba umechakachuliwa yote wamejitoa kijanja ili kumwachia Lugumi aungue peke yake, lakini Ukweli ni kwamba Lugumi na kitwanga Lao ni moja isipokuwa kwenye shida ndipo kaamua kumsukumia Lugumi peke yake , wameiga Style ya Mwakyembe juu ya mabehewa chakavu ambapo alipiga dili kisha akawabebesha zigo wengine.
 
Naona kuko na personal attacks apa na kuna ajenda nyingi nyuma ya Pazia.
Kama infoys walishakana kuwa hawajawai kuwa na mkataba na Lugumi na hii habari inasema Lugumi wamekwamishwa na hao.
Anyway time will tell ukweli ukija wekwa wazi
 
Miruzi imekuwa mingi mnoooo

Kweli kabisa, hii habari haioneshi Lugumi na Infosys wanakutana wapi japo inadai imeuona mkataba. Upuuzi mtupu. Kama mkataba ni baina ya Lugumi na polisi iweje BioLink wakabidhiane vifaa na polisi wakati katika habari hakuna sehemu yeyote inayoonesha bioLink imekuwa subbed. Sasa kama Lugumi ime i sub infosys nani anahusika na mkataba na polisi, lugumi au infosys?
 
Nina kila sababu ya kuamini kuwa; kuchelewa kutolewa kwa mkataba huo na kutoroka kwa Lugumi kuna mkono wa waziri KITWANGA.
 
Naona kuko na personal attacks apa na kuna ajenda nyingi nyuma ya Pazia.
Kama infoys walishakana kuwa hawajawai kuwa na mkataba na Lugumi na hii habari inasema Lugumi wamekwamishwa na hao.
Anyway time will tell ukweli ukija wekwa wazi
Usitegemee ukweli ndugu, utasubiri hadi uzeeke na ukweli hutopata.. Usanii umejaa hii nchi.. Wanaochukuliwa hatua nchi hii ni watu wadogo sana.. Tuendelee kuchekelea majipu uchwara wakati yale sugu yakila maisha
 
Kweli kabisa, hii habari haioneshi Lugumi na Infosys wanakutana wapi japo inadai imeuona mkataba. Upuuzi mtupu. Kama mkataba ni baina ya Lugumi na polisi iweje BioLink wakabidhiane vifaa na polisi wakati katika habari hakuna sehemu yeyote inayoonesha bioLink imekuwa subbed. Sasa kama Lugumi ime i sub infosys nani anahusika na mkataba na polisi, lugumi au infosys?
Umetumwa ulete hoja flani lkn inaonekana hawakukuandikia umekuja kuandika mwenyewe! Ona sasa umeandika PUMBA!
 
Kama umezoea kutumwa ukafikiri kila mtu anatumwa haujafanikiwa kifikra. Kama umeshindwa kimantiki kujibu ukaona nimeandika pumba na wewe umejibu hizo pumba basi wewe ni pumba mara mbili.
 
HIVI UNAMPAJE MTU KAZI YA BILLION 34 BILA YA YEYE KUKUPA SECURITY CHEQUE YA SAME AMOUNT???..Na ilikuwaje akalipwa full amount?? hivi hakuna mambo ya 50% advance kwenye serikali yetu??? Kazi kweli kweli, yani hapo wangempa siku kadhaa ameshindwa timiza kazi wana deposit cheque wanabeba pesa zao. cheque ikibaunce anakuwa na kesi 2 za kujibu, SASA KAMA HATA POLISI WANAIBIWA WANAKAA KIMYA SISI RAIA ITAKUWAJE??
 
Computer pc 100 kwa billion 36 nilidhani ni vitu vya maana sana kwamba vinaweza lingana na hela aisee Mungu atusaidie haya majambazi ni hatari sana..
 
Ni vita kati ya watetea mafisadi waliotumwa na wale wanaomtaka Rais aonyeshe kweli kama anaubavu juu ya majipu yaliyogeuka kansa mgongoni mwa Rais mwenyewe.
 
Back
Top Bottom