Hatimaye Kamati ya Mwakyembe yaanika ufisadi TRL

Hatimaye Kamati ya Mwakyembe yaanika ufisadi TRL

Mwongo mkubwa wewe. Hili dili la Mwakiembe mwenyewe na ndio maana aliondolewa wizara ya uchukuzi.

Alipiga dili la mabehewa na kule bandarini akapata bilioni ya kununua kiwanja kule Bahari Beach zingine alitaka ziwe za uchaguzi kule kwao Kiela ambako watu hawamtaki.

Hii ripoti alikabidhiwa tokea tarehe 01/12/2015 lakini hakuitangaza mpaka Sitta alivyokuja na kuwaambia kamati wamkabidhi yeye.

Hili ndilo lilifanya Mwakiembe aondolewe Ikulu. Kama mnabisha mwambie aipeleke mahakamani gazeti la Jamhuri lililoandika kuhusu ufisadi wake. Taarifa zote wanazo na hata alivyolipa pesa kule Yono Auction Mart kununua kiwanja kutoka kwa mzungu wa Kijerumani.

huyu bwana ameleta thread hii il kumcover mnyakyusa mwenzake....ukweli uko wazi mwekyembe ndo alikuwa nyuma ya hii kitu....
 
wizara ya uchukuzi ni miongoni mwa sekta 6 za BRN ambazo zilisemekana kupewa mfumo usiokuwa na mlolongo mwingi wa manunuzi, sasa naomba kufahamishwa haya yametokeaje????
 
Mwakyembe anaumbuka sasa ...alipiga deal la kufua umeme wa upepo akaishia kuwadanganya wananchi kuwa lowassa alihusika kwenye richmond... alimtimua chizi ATC ikafa rasmi baada ya kumteua binamu ... wameua TRL ilikuficha madhambi yao...
 
Unataka ushahidi gani? Si nenda Yono Auction Mart ukachunguze? Umekuwa toto jinga utafuniwe kila kitu?

Ukitaka taarifa zaidi kiwanja chenyewe ni plot numbers 160&161 kinatazamana na hoteli ya Bahari beach. Ikulu wanajua na ndio maana walimtoa hiyo wizara. Angelikuwa mtu mwingine angefukuzwa kabisa. Ila walijua Mwakiembe angeanza propaganda zake kwamba kaonewa. Wakamtuma rafiki yake Sitta ashuhudie ufisadi wake.

Kiwanja hicho alitaka kukifanya eneo la ku park magari kwa abiria watakaokuwa wanatumia hiyo meli kutoka Bagamoyo kwenda kule mjini. Ila wamemtoa kabla na dili imelala.

Tunajua mengi sana ya Mwakiembe. Karma ya Pasco imeanza kumrudia baada ya kumwonea Lowassa.

Jenifa naona unaugua ugojwa usioeleweka
. Umeng'ang'ana wewee Ohhh Mwakyembe kanunua kiwanja bahari beach. Tunachotaka kutoka kwako ni ushahidi wa docs na sio maneno ya Kariakoo shimoni.
Tuwekee vithibitisho. Nenda kwa huyo Yono wako akupe ushahidi. Usituletee maneno ya kwenye taarabu ya mzee Yusuf, tunataka ushahidi.
Kama huna ushahidi Nenda kwenye kazi yako ya kucheza baikoko au kanga moko, huku sio kwako hakukufai.
 
Taarifa za uwakika pasipo shaka yoyote kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa tume ya uchunguzi wa ununuzi wa mabehewa ya TRL iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa uchukuzi ambao wamekabidhi ripoti yake kwa Mhe. Sita Waziri wa sasa wa uchukuzi imeweka wazi jinsi wataalam wa TRL walivyofisadi

Nchi kwenye ununuzi wa haya mabehewa.

Mojawapo ya maajabu ya Musa kama siyo ya firahuni ni pale hawa wataalam walipobadilisha specification s na baadhi ya vipengele vya mkataba baada ya ukaguzi nchini India ili mkataba ukidhi walichokuta huko na siyo mtengenezaji atengeneze kwa mahitaji
yetu... Bila huruma wala weledi wakaweka matumbo yao Mbeleeee.

Tumwombe Mhe. Waziri awachukulie hatua stahili na wapelekwe Kmahakamani kwa kuhujumu uchumi na siyo kuwahamishaa.

Tegemea report kamili hapa .....
Serikali Ya nne imewalea Hadi hatuwawezi tena watu wanaohujumu uchumi wetu
 
Hii nchi jinsi mambo yanavyofanyika ndani ya serikari ata uelewi despite clear guidelines za sheria na tofauti zake za utendaji (utaratibu tu wa manunuzi au hata tender ungekuwa unafanywa kwa taratibu za sheria zilizopo ingepunguza huu uhujumu).

Hivi inawezekana vipi mtu kucholopoka na kiasi hiko cha fedha kwenye manunuzi tu, it does not make sense; kuna mtu anaidhinisha manunuzi huyu aliambiwa bidhaa ipi atapewa kabla ya kutoa hela, na yeye mwenyewe anajua thamani ya hiyo product ilivyo sokono. Surely hata nyumbani kwako mtu awezi kukwambia bei ya mbuzi laki mbili na ukakubali unless labda una pesa nyingi na ujali. Lakini kama mtu makini walau ungenyanyua hata simu basi kupata uhakika.

Sasa linapokuja swala la sh/b230 na watu bado wakaleta bidhaa za ovyo hivyo huku wakichekecheka mabillioni unajiuliza huyo alieidhinisha malipo ya hayo bidha alijua serikari inapata product gani kutokana na thamani ya hela.

Chain ya lawana ni ndefu sana, aishii kwa mwakymembe tu inarudi mpaka MoF this is unacceptable hakuna procurement team huko wizara ya fedha, wizara ya uchukuzi, mawaziri wote wawili wameshindwa fanya verification ya thamani ya hayo mabehewa.

Mimi ndio maana nimemuelewa January ingawa sidhani kama ni mtu sahihi (but who am I) hila hoja yake ina mashiko anapodai yaani watu hawaogopi tena kuchukua na hakuna wakuwauliza lazima mtu azuie hilo; surely huu ni uzembe kuanzia ngazi ya juu na taasisi zote husika kwenye usimamizi wa hela za umma.

Yaani mtu unashindwa kuelewa how is this possible: only in Tanzania,

Do you even need a whistle blower for this kama watu wangekuwa makini tu.
 
Mwongo mkubwa wewe. Hili dili la Mwakiembe mwenyewe na ndio maana aliondolewa wizara ya uchukuzi.

Alipiga dili la mabehewa na kule bandarini akapata bilioni ya kununua kiwanja kule Bahari Beach zingine alitaka ziwe za uchaguzi kule kwao Kiela ambako watu hawamtaki.

Hii ripoti alikabidhiwa tokea tarehe 01/12/2015 lakini hakuitangaza mpaka Sitta alivyokuja na kuwaambia kamati wamkabidhi yeye.

Hili ndilo lilifanya Mwakiembe aondolewe Ikulu. Kama mnabisha mwambie aipeleke mahakamani gazeti la Jamhuri lililoandika kuhusu ufisadi wake. Taarifa zote wanazo na hata alivyolipa pesa kule Yono Auction Mart kununua kiwanja kutoka kwa mzungu wa Kijerumani.

!!!!! Bibi Jenifa weka kumbukumbu zako vizuri...mwezi aw pili Mhe. Sita alipotembelea TRL kwa Mara ya 2 aliwaambia anaitaji hiyo report haraka. Tumia hesabu rahisi za kujumlisha na kutoa Kibibi..angekuwa na hiyo report why aulize tena. Alichofanya Mwakyembe ni kuwasimamisha wale wote waliohusika direct na issue akaunda team ikiongozwa na wahandishi wanaoheshimika kutoka nje ya TRL waje na details of what happen ili wote waliohusika direct and indirect wapelekwe kwa Pilato....Kisutu. ...Kamati ndio imeelezea hayo yote.
 
kikwete kwa nini ulimhamisha huyu jamaa Mh MWAKYEMBE ukapeleka mbemendaji 6 wanaua bandari sasa watafuata na reli ajali kila siku mkemee afanye kazi asitumie kigezo cha kukuzidi umri
 
kikwete kwa nini ulimhamisha huyu jamaa Mh MWAKYEMBE ukapeleka mbemendaji 6 wanaua bandari sasa watafuata na reli ajali kila siku mkemee afanye kazi asitumie kigezo cha kukuzidi umri

Sitta mpaka sasa sio mbaya,kamkaba koo mkurugenzi wa TPA na kumfukuza kazi kabisa.Huko TRL nako hakumungunya maneno,ametema makombora mazito na kusimamisha uongozi wa shirika la Reli.
 
Jenifa naona unaugua ugojwa usioeleweka
. Umeng'ang'ana wewee Ohhh Mwakyembe kanunua kiwanja bahari beach. Tunachotaka kutoka kwako ni ushahidi wa docs na sio maneno ya Kariakoo shimoni.
Tuwekee vithibitisho. Nenda kwa huyo Yono wako akupe ushahidi. Usituletee maneno ya kwenye taarabu ya mzee Yusuf, tunataka ushahidi.
Kama huna ushahidi Nenda kwenye kazi yako ya kucheza baikoko au kanga moko, huku sio kwako hakukufai.

Sishangazwi na maneno yako maana majungu yamekuzidi,hivi kweli wewe mwanamke mumeo huwa anakuelewa kweli?maana mtu akioa mwanamkekama weweni hasara sana
 
Soma alichoongea waziri sita wiki jana wakati anatangaza kusimamisha hao viongozi.

Ripoti iliwakilishwa kwa Mwakiembe tarehe mosi mwezi wa 12 mwaka jana. Mwakiembe aliifungia tu ndani hakuchukua hatua yoyote mpaka alipohamishwa. Mr Six akaiambia tume tena iwakilishe hiyo taarifa upya kwake. Hii ndiyo ambayo wewe unaiongelea.

Mabehewa mabovu yalijulikana tokea mwanzoni mwa mwaka jana. Mwakiembe analijua hili dili ndani na nje. Hiyo tume ilikuwa danganya toto tu lakini wenzake wakamuwahi na sasa anasoma magazeti yote ya siku kule Afrika Mashariki.
!!!!! Bibi Jenifa weka kumbukumbu zako vizuri...mwezi aw pili Mhe. Sita alipotembelea TRL kwa Mara ya 2 aliwaambia anaitaji hiyo report haraka. Tumia hesabu rahisi za kujumlisha na kutoa Kibibi..angekuwa na hiyo report why aulize tena. Alichofanya Mwakyembe ni kuwasimamisha wale wote waliohusika direct na issue akaunda team ikiongozwa na wahandishi wanaoheshimika kutoka nje ya TRL waje na details of what happen ili wote waliohusika direct and indirect wapelekwe kwa Pilato....Kisutu. ...Kamati ndio imeelezea hayo yote.
 
Mwongo mkubwa wewe. Hili dili la Mwakiembe mwenyewe na ndio maana aliondolewa wizara ya uchukuzi.

Alipiga dili la mabehewa na kule bandarini akapata bilioni ya kununua kiwanja kule Bahari Beach zingine alitaka ziwe za uchaguzi kule kwao Kiela ambako watu hawamtaki.

Hii ripoti alikabidhiwa tokea tarehe 01/12/2015 lakini hakuitangaza mpaka Sitta alivyokuja na kuwaambia kamati wamkabidhi yeye.

Hili ndilo lilifanya Mwakiembe aondolewe Ikulu. Kama mnabisha mwambie aipeleke mahakamani gazeti la Jamhuri lililoandika kuhusu ufisadi wake. Taarifa zote wanazo na hata alivyolipa pesa kule Yono Auction Mart kununua kiwanja kutoka kwa mzungu wa Kijerumani.

Hii tarehe uliyoitaja (1/12/2015) inakuonyesha tu ulivyo na majungu.
 
Jenifa naona unaugua ugojwa usioeleweka
. Umeng'ang'ana wewee Ohhh Mwakyembe kanunua kiwanja bahari beach. Tunachotaka kutoka kwako ni ushahidi wa docs na sio maneno ya Kariakoo shimoni.
Tuwekee vithibitisho. Nenda kwa huyo Yono wako akupe ushahidi. Usituletee maneno ya kwenye taarabu ya mzee Yusuf, tunataka ushahidi.
Kama huna ushahidi Nenda kwenye kazi yako ya kucheza baikoko au kanga moko, huku sio kwako hakukufai.

Umemjibu vizuri saaana nimefurahi sana ila nashanga kama kuna mtanzania ambaye anajielewa anaweza kumponda mwakyembe labda kama ni mtumwa wa wanasiasa wachafu.
 
Watu kama hawa ndo tunataka IKULU lakini sijui kwanini hatangazi nia
 
madudu yote yalitokea wakati wa mwakyembe sasa mnajipa promo tu bado issue ya ujenzi wa vip kwenye airport ya dar rais alimwokoa maana ripotiza acg zilikuwa zinakaanga taasisi ziluizo chini yake hembu jiulizeni mpaka anaondoka bandari na atcl taasisi zote walikuweko makaimu, mwakyembe maneno mengi ila ni zero
 
Ufisadi ndani ya serekali ya ccm umetamalaki, simply because wanajua hakuna hatua zozote kali zitakazochukuliwa
 
22nd April 2015

headline_bullet.jpg
Sasa yagundulika aliyeleta mabehewa feki alikuwa na bei ya juu kuliko wote, Aliruhusiwa na kufanyia marekebisho zabuni yake kinyemela

Madudu zaidi yameendelea kuibuka katika sakata la mabehewa feki 274 yaliyonunuliwa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), na sasa imebainika kuwa kampuni iliyopewa zabuni ya kuleta mabehewa hayo ndiyo iliyokuwa ya bei ya juu zaidi kuliko kampuni 10 zilizokuwa zimeomba na haikuweka dhamana yoyote kama sheria ya manunuzi inavyotaka.

Aidha, imebainika pia kuwa ya Hindustan Engineering Ltd ya India, ambayo ilishinda zabuni hiyo, ilibadilishiwa vigezo (specification), vya aina ya mabehewa kinyemela baada ya zabuni kutangazwa na wazabuni kuwasilisha maombi yao.

Kwa mujibu wa taarifa za uhakika ambazo NIPASHE imezipata, kampuni hiyo iliomba kuiuzia TRL mabehewa 174 yenye ‘rubber’ badala ya ‘spring’ kwa dola za Marekani 18,209,317.50 (Sh. bilioni 32.8) wakati kampuni ya Baotou Beifang Chuangye Co. Ltd ya China ilikuwa tayari kuleta idadi hiyo ya mabehewa yenye viwango vinavyokubalika kwa dola za Marekani 13,907,907 (Sh. bilioni 25).

Kampuni hiyo pia ilishinda zabuni hiyo ambayo ilihusisha kuleta mabehewa mengine 100 ya mizigo ambayo ni ya muundo wa matangi (tank wagon) na yasiyofunikwa (flat wagon) kwa dola za Marekani 10,278,182.50 (Sh. bilioni 18.5) wakati kampuni ya Baotou Beifang Chuangye Co. Ltd ya China iliyokuwa ndiyo yenye bei ndogo ilikuwa tayari kuleta idadi hiyo ya mabehewa kwa dola za Marekani 7,272,975 (Sh. bilioni 13.09).

Kampuni hiyo pia ilishinda zabuni ya kuiuzia TRL vipuri kwa thamani ya dola za Marekani 2,561,187.50 (Sh. bilioni 4.4) baada ya kuirekebisha na taarifa ya zabuni inaonyesha kuwa iliwasilisha zabuni iliyorekebishwa na ilikubaliwa.'

Kampuni ya Baotou Beifang Chuangye Co. Ltd iliomba kuleta vipuri hivyo kwa dola za Marekani 2,475,835 (Sh. bilioni 4.46) wakati kampuni nyingine kama Transnet iliomba kwa dola za Marekani 3,108,687 (Sh. bilioni 5.6) wakati Modern Industries iliyoshindwa kwa kutowasilisha dhamana iliomba kwa dola za Marekani 3,344,925 (Sh. bilioni 6.02).

Kwa ujumla taarifa zinaonyesha kuwa kampuni ya Hindustan Engineering ililipwa dola za Marekani 31,048,688 (Sh. bilioni 55.9) wakati kampuni iliyokuwa ya bei ndogo kuliko zote ingeweza kufanyakazi hiyo kwa dola za Marekani 24,368,757 (Sh. bilioni 43.86) hatua ambayo ingeokoa dola za Marekani 6,677,931 (Sh. bilioni 12.02) na kutoitumbukiza nchi kwenye hasara hiyo ya mabehewa feki.

“Mabehewa nyenye rubber hayawezi kabisa kwa namna yoyote ile kupita kwenye reli yetu. Kilichotokea ni kwamba zabuni iliyotangazwa ilitaka wazabuni walete mabehewa yenye spring ambayo ndiyo sahihi, lakini baadaye inaonekana walibadilisha vigezo na kuielekeza kampuni waliyoipa zabuni vigezo vipya ndiyo maana unaona mabehewa yaliyokuja hayafai,” alisema mmoja wa wataalam wa reli ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kampuni ya Hindustan Engineering Ltd haikuweka dhamana yoyote jambo ambalo ni kinyume cha sheria ya manunuzi ya umma na ilitaka ilipwe fedha yote kabla ya kuingiza mabehewa nchini jambo ambalo TRL ilitekeleza.

Wakati mzabuni huyo akiweka masharti hayo, kampuni nyingine zilizoomba ikiwamo iliyokuwa ya bei ndogo zaidi, iliweka dhamana na ilitaka ilipwe kwa awamu hadi itakapokamilisha kazi husika.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa pamoja na kwamba kampuni ya Hindustan Engineering Ltd ilikuwa ya gharama kubwa iliomba kufanya kazi hiyo kwa miaka miwili, wakati kampuni nyingine zilizoshindana kwenye zabuni zingeweza kufanya kazi hiyo kwa miezi tisa hadi mwaka mmoja.

Kampuni ya Hindustan Engineering Ltd haikuweka gharama za matengenezo wakati kampuni nyingine zote ziliweka.

Taarifa zinaonyesha kuwa kampuni nyingine zilikosa sifa za kushinda zabuni kwa kutowasilisha dhamana (bid security), ikiwamo ile ya Modern Industries, DCD rolling stock ambayo pia iliwasilisha bei zilizokuwa na kasoro za kiuandishi pamoja na Lucky Export.

Kampuni nyingine zilizoomba zabuni hiyo ni Caeic Beigin Ltd, CNR Import and Export Corporation Ltd, Hyunan Construction Engineering Ltd, Texmaco Rail and Engineering na Transnet.

Taarifa hizo zimeibuliwa siku sita tu baada ya Alhamisi iliyopita Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, kuwasimamisha kazi vigogo watano wa TRL, akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wake, Kipallo Kisamfu, kutokana tuhuma za kuihujumu serikali katika sakata la ununuzi wa mabehewa feki 274 ya mizigo na kuisababishia hasara ya Sh. bilioni 230.

Wengine waliosimamishwa ni Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles; Mhasibu Mkuu, Mbaraka Mchopa; Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiranga na Meneja Mkuu wa Manunuzi, Ferdinand Soka.

Sitta alisema baada ya kuwasimamisha vigogo hao, utafanyika uchunguzi dhidi yao kwa wiki tatu kuanzia wiki iliyopita.

Kufuatia uamuzi huo, Sitta alimteua aliyekuwa Mhandisi wa TRL, Elias Mshana, kuwa Kaimu Mkurugenzi wa kampuni hiyo, na kumwagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dk. Shaaban Mwinjaka, kusimamia kuundwa kwa kamati ya uchunguzi huo.

Alisema kamati hiyo itaongozwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akishirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi katika Sekta ya Umma (PPRA) pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Sitta alichukua uamuzi huo baada ya kupokea taarifa ya uchunguzi ya kamati iliyoundwa na Waziri aliyemtangulia wizarani hapo, Dk. Harrison Mwakyembe, ambaye alihamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambayo imegundua kuwako kuna hujuma mbalimbali katika kuendesha TRL.

Kabla ya kuchukua uamuzi wa jana, Waziri Sitta aliiagiza bodi ya Wakurugenzi ya Reli kupitia taarifa hiyo na kutoa maelezo kwake juu ya suala ya ununuzi wa mabehewa hayo.

Mabehewa hayo yaliingizwa nchini kupitia kandarasi ya Kampuni ya M/S Hindustan Engineering and Industrial Limited ya India ikishirikiana na kampuni moja nchini inayomilikiwa na mfanyabiashara mmoja ambaye amekuwa akijihusisha na biashara nyingi za kulaghai mashirika ya umma na kujipatia ukwasi wa kupindukia.

Mabehewa hayo yaligundulika kuwa mabovu baada ya kufanyiwa majaribio na baadhi kuanguka kwa kukosa ‘stability’ yakiwa relini na yaliyopokelewa na Dk. Mwakyembe Julai 24, mwaka jana, hayakupitiwa na jopo la mafundi wa TRL ili kuthibitisha ubora wake.

Jana NIPASHE lilimtafuta Waziri Sitta kuzungumzia taarifa hizo bila mafanikio kutokana na simu zake za mkononi kushindwa kupatikana.

Hata hivyo mmoja wa walinzi wake aliliambia NIPASHE kuwa waziri huyo alikuwa kwenye kikao ambacho hata hivyo hakueleza kilikuwa kinafanyikia wapi.

CHANZO: NIPASHE

Back
Top Bottom