Hatimaye Kamati ya Mwakyembe yaanika ufisadi TRL

Smart mwananchi

Senior Member
Joined
Jul 17, 2014
Posts
102
Reaction score
50
Taarifa za uwakika pasipo shaka yoyote kutoka kwa mmoja wa wajumbe wa tume ya uchunguzi wa ununuzi wa mabehewa ya TRL iliyoundwa na aliyekuwa Waziri wa uchukuzi ambao wamekabidhi ripoti yake kwa Mhe. Sita Waziri wa sasa wa uchukuzi imeweka wazi jinsi wataalam wa TRL walivyofisadi

Nchi kwenye ununuzi wa haya mabehewa.

Mojawapo ya maajabu ya Musa kama siyo ya firahuni ni pale hawa wataalam walipobadilisha specification s na baadhi ya vipengele vya mkataba baada ya ukaguzi nchini India ili mkataba ukidhi walichokuta huko na siyo mtengenezaji atengeneze kwa mahitaji
yetu... Bila huruma wala weledi wakaweka matumbo yao Mbeleeee.

Tumwombe Mhe. Waziri awachukulie hatua stahili na wapelekwe Kmahakamani kwa kuhujumu uchumi na siyo kuwahamishaa.

Tegemea report kamili hapa.

 
breaking halafu porojo tu...
 
Kazi za Mwakyembe zina weledi sana,kwa madudu hayo tunamuomba waziri sita achukue maamuzi ya kuwafuta kazi na kuwapeleka mahakamani
 
Tunataka uchunguzi mwingne ufanyike juu ya ununuzi BVR.
 
Mwakyembe unawakatisha tamaa mafisadi, wanatamani kweli na wanaomba usiku na mchana wakuweke kweny kundi lao lakini wameshindwa, Now nimeanimi kuwa ulikufa na wemefufuka tena kaza but na endelea kutuwakilsha vyema africa mashariki:rockon:
 
Nimepitaa mtanikuta Ubungo October jam a wanapiga utafikiri niniii kama nchi ni ndege basi kuna mijitu inafikiri nchi IPO kwenye auto pilot.....
 

Sitta atachukua maamuzi magumu kutaka sifa na uzee wake wa 71, si anajinasibu kutaka nafasi magogoni! Huu mwaka vyura vitageuka kenge,mae
 
Kaka vipi nazo unazitili shaka BVR????, basi iundwe tume lakini sijamuona mwingine mtamu kama mcharu wa kuunda tume inayo leta mjibu mazuri na yasiyo na longolo kama mh mwakyembe, ana tisha kwenye kuunda tume, nazani ana digirii sita nayo ni kuunda tume.:yo:
 
Hua najiulizaga ninini kilicho mfanya rais kumuhamisha mwakiembe kwenye wizara hii alafu hua sipati majibu,
 
Mkuu, nani wa kuchukua hatua??? Umeamia lini Tanzania?
Unamfahamu vizuri Bw. Sita na Mwakyembe?

Angekuwa Mwakyembe bado yupo uchukuzi maamuzi magumu yagekuwepo,huu ndio muda wa kuona kama mzee sita anaweza kutoa maamuzi au atawalinda wezi
 
Mwongo mkubwa wewe. Hili dili la Mwakiembe mwenyewe na ndio maana aliondolewa wizara ya uchukuzi.

Alipiga dili la mabehewa na kule bandarini akapata bilioni ya kununua kiwanja kule Bahari Beach zingine alitaka ziwe za uchaguzi kule kwao Kiela ambako watu hawamtaki.

Hii ripoti alikabidhiwa tokea tarehe 01/12/2014 lakini hakuitangaza mpaka Sitta alivyokuja na kuwaambia kamati wamkabidhi yeye.

Hili ndilo lilifanya Mwakiembe aondolewe Ikulu. Kama mnabisha mwambie aipeleke mahakamani gazeti la Jamhuri lililoandika kuhusu ufisadi wake. Taarifa zote wanazo na hata alivyolipa pesa kule Yono Auction Mart kununua kiwanja kutoka kwa mzungu wa Kijerumani.

 

Jenifa naona unaugua ugojwa usioeleweka
. Umeng'ang'ana wewee Ohhh Mwakyembe kanunua kiwanja bahari beach. Tunachotaka kutoka kwako ni ushahidi wa docs na sio maneno ya Kariakoo shimoni.
Tuwekee vithibitisho. Nenda kwa huyo Yono wako akupe ushahidi. Usituletee maneno ya kwenye taarabu ya mzee Yusuf, tunataka ushahidi.
Kama huna ushahidi Nenda kwenye kazi yako ya kucheza baikoko au kanga moko, huku sio kwako hakukufai.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…