Hatimaye Jubilee team Nairobi imekamilika, Sonko ameshinda

MK254

JF-Expert Member
May 11, 2013
32,238
50,410
Sasa mchuano wa uongozi wa Nairobi umeeleweka, upande wa NASA tunaye gavana wa sasa bwana Evans Kidero, nao Jubilee bwana Mike Mbuvi almaarufu kama Sonko ameibuka mshindi. Kuanzia sasa ni kampeini za mbele kwa mbele, ila Sonko kuna uwezekano mkubwa akaibuka na kuwa gavana wetu Nairobi.

3s.jpg

From left: Senator Mike Sonko, Woman Rep Rachel Shebesh and Nominated MP Johnson Sakaja, who are leading in Nairobi Jubilee primaries. PHOTOS | NATION MEDIA GROUP

Nairobi Senator Mike Sonko has won the Nairobi Jubilee gubernatorial nominations.

Senator Sonko got 138, 185 votes against Peter Kenneth's 62, 504 and Bishop Margaret Wanjiru's 7, 654 votes; in 17 constituencies.

In the senatorial race, Mr Johnson Sakaja is leading with 106, 469 in 14 constituencies, Richard Kavemba is second with 10, 729 and Mr Badi Ali third with 9, 079.

In the Nairobi Women Representative nominations, Mrs Rachel Shebesh is also leading with 61,445 followed by Mrs Millicent Omanga with 39,634 while Ms Karen Nyamu has 28,502 votes.

Earlier, Mrs Shebesh stormed Nyayo Indoor Gymnasium at Nyayo Stadium, where the tallying is taking place.

She claimed that her votes in Embakasi North were being stolen and added onto Mrs Omanga's.
"I will stay here and stop this process until you tell me what's going on and why my votes are being stolen," said an agitated Mrs Shebesh who was then escorted to record a statement at Nyayo Stadium Police post.

She later left with her supporters to Jubilee headquarters to lodge a complaint.
Sonko, Sakaja and Shebesh win JP primaries
 
Mimi ni Jubilee lakini Sonko na Shebesh hawaoni Kura yangu kamwe. Governor nitampa Miguna Miguna na Woemen rep sijajua bado.
 
Hebu nishawishi Miguna ana umuhimu gani kuwa gavana wa Nairobi. What's his track record.
Binafsi simpendi Sonko, lakini jamaa ni king'ang'anizi balaa, mpiganaji na mpambanaji, huwa napenda sana sifa za kihivyo maana binafsi najijua kama mpambanaji wa kiaina.

Halafu Sonko amefanya mambo ya kuonekana na kutajika japo ana mapungufu yake. Tukianza kugawa kura, Nairobi itarudi kwa Kidero aendelee kuinyofoa na kuibamiza hadi tuikimbie.
Shebesh ndiye sina hamu naye kabisa, hata ikiwezekana wadhifa wa Women rep ufutwe.
 
Tuhuma za vyeti kwa Sonko.. Zimefikia wapi..!? atakuwa na ushawishi tena kwa wananchi.!
 
Hebu nishawishi Miguna ana umuhimu gani kuwa gavana wa Nairobi. What's his track record.
Binafsi simpendi Sonko, lakini jamaa ni king'ang'anizi balaa, mpiganaji na mpambanaji, huwa napenda sana sifa za kihivyo maana binafsi najijua kama mpambanaji wa kiaina.

Halafu Sonko amefanya mambo ya kuonekana na kutajika japo ana mapungufu yake. Tukianza kugawa kura, Nairobi itarudi kwa Kidero aendelee kuinyofoa na kuibamiza hadi tuikimbie.
Shebesh ndiye sina hamu naye kabisa, hata ikiwezekana wadhifa wa Women rep ufutwe.

Tatizo amablo tuko nalo katika kaunti ya Nairobi ni kupigana na Ufisadi. Badda ya kupigana na ufisadi, tunahitaji mtu ambaye ako methodical na kazi anayofanya. Kidero hawezi Kazi lakini anajibeba kama mtu mwenye akili. Sonko naye, anafanya vitu za kitoto sana. Ashapenda kulia kila mara na propaganda za kiupuuzi. Hivi Juzi, tayari alishakuwa ashaanza kulia eti supporters wake wanafukuzwa kwenye polling station. Hao clerks walijuaje kuwa wanaokuja hapo ni supporters wa sonko?

Tayari alishakuwa kasema Nasa wampe direct ticket. Huyu ni mtu amabye tamaa yake ye uongozi ndio inamwendesha.

La pili, hajui atakachofanya akishika mamlaka. Mtu mwenye akili huwezi kusema kuwa utatengeneza parking lot Uhuru Park ili kuondoa traffic jam. Miguna tu ndiye ako na track record ya kupigana na ufisadi na kutetea haki za wanyonge. He is the only person who has bothered to tell us what he'll do. https://migunamiguna.com/manifesto/
 
Kaka tusipende mambo ya nadharia sana zaidi ya vitendo, ingekua ni nadharia basi Kidero ningempa kura yangu mapema maana jamaa yupo sawa katika kuandaa manifesto na kuitetea. Nakumbuka kabla hajawa gavana, nilikua namskiliza alivyokua anatiririka kuhusu atakachofanya Nairobi hadi nikapata raha kweli. Lakini miaka mitano baadaye tumejonea wenyewe.

Ndio maana nikahoji track record ya Miguna zaidi ya kujaza vijimaneno vya nadharia kwenye blog. Ugomvi wake na Raila ulikua wa kibinafsi na sio kwa sababu za tofauti kwenye itikadi. Kumbuka huyu Miguna bado alikua swahiba wa karibu kipindi tuhuma za ufisadi zikichipuka kwenye ofisi za Raila wakati akiwa waziri mkuu. Hivyo hadi nipate ushawishi wa nini amekifanya cha kuonekana, sina budi kumpa kwaheri.

Sonko alikua na haki za kulalamika wakati wa kura za mchujo, unyang'au ulikua unatendeka pale ambapo hata Kenneth mwenyewe alilalamika pia. Tusijitoe ufahamu, sote tunajua kwenye kura za mchujo, kila mgombea huja na wafuasi wake, hivyo hilo sio la kushangaza. Na zaidi, hamna kiongozi asiyekua na tamaa, siku unaamua kuwa mbunge, seneta, gavana au rais, lazima utakua na tamaa za kichizi, hilo lipo ulimwengu wote na sio sababu za kumpiga chini Sonko.

Viongozi wote hawa wana mapungufu, lakini unachagua yule nafuu.
 
Hivi Sonko, Shebesh na Miguna ni Kabila gani?

Nairobi hatuongozwi na misingi ya ukabila, ni mji mkubwa zaidi ya yote ukanda wa EAC na kati na una watu wa matabaka mbali mbali wakiwemo Watanzania.
Sonko asili yake Ukambani, Miguna ametokea Ujaluoni na Shebesh ana asili ya Kikikuyu.
 
Haki natamani Bashite angekuwa huko kwenu.

Dah! Angekua kwetu hata asingepumua aisei, Wakenya balaa. Waulize Sonko na yule gavana wa Mombasa, walilazimika kuanika vyeti vyao tangu chekechea hadi vyuoni maana walikumbana na mtiti wa kiajabu. Wakenya wakikushuku una vyeti fake, inabidi uchakarike na kurudi ulikosomea ili walimu wajitokeze na kukutetea maana tuna hulka ya kuibua mzuka hadi unakoma.

Bashite angekua Mkenya asingeendelea kupeta, yaani anazomewa kila anakokwenda, akitaka kuhutubia anapigwa chini kwa mayowe, akitembea barabarani anakumbushiwa na halaiki ya watu, akigeuza huku na kule mambo yale yale, akiingia kwenye bar kupata kinywaji anakutana na walevi wajasiri wanaompa makavu.

Huyo abaki huko huko, tena naoa anapeta tu kama kwamba hamna lolote hadi anavamia vyombo vya habari. Hivi wale vijana wa SHILAWADU bado wapo au walisitisha kabisa baada ya jamaa kuwazimia.
 
Wakenya nawaaminia,hamna mchezo ktk masuala ya maslahi ya Taifa ndio maana mmeendelea.

Vijana bado wapo mkuu,wanachapa kazi na maisha yanaendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tanzania hii isikieni tu,ni nchi ya hovyo sana.
 
Nairobi hatuongozwi na misingi ya ukabila, ni mji mkubwa zaidi ya yote ukanda wa EAC na kati na una watu wa matabaka mbali mbali wakiwemo Watanzania.
Sonko asili yake Ukambani, Miguna ametokea Ujaluoni na Shebesh ana asili ya Kikikuyu.
Dar is the largest city in EA sizewise n populationwise! Don't get it twisted
 
Wakenya nawaaminia,hamna mchezo ktk masuala ya maslahi ya Taifa ndio maana mmeendelea.

Vijana bado wapo mkuu,wanachapa kazi na maisha yanaendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.
Tanzania hii isikieni tu,ni nchi ya hovyo sana.

Ingekuwa Kenya imeendelea mbona hamna Mtanzania anayetamani kuzamia huko? Watu wasingejisumbua kwenda Afrika Kusini wakati Kenya ipo karibu.
Amka , achana na hadithi za vijiweni.
 
Nairobi hatuongozwi na misingi ya ukabila, ni mji mkubwa zaidi ya yote ukanda wa EAC na kati na una watu wa matabaka mbali mbali wakiwemo Watanzania.
Sonko asili yake Ukambani, Miguna ametokea Ujaluoni na Shebesh ana asili ya Kikikuyu.

Kaka mbona unajibu hata usichoukizwa?, mi nilitaka kujua makabila ya hao wagombea tu kaka, yupi hapo ni wa NASA?
 
Back
Top Bottom