Hatimaye Jerry Muro ' ajilipua ' kwa kuwatolea Uvivu Viongozi wa Yanga SC, Kocha Mwinyi Zahera na Msemaji Dismas Ten

Ni haki yake kutoa maoni yake. Lakini atambue si kila anachosema kinapata uungwaji mkono na watu wote...Mimi ni mmoja wapo ninayemwona kama mtoa post na aliyemnukuu wote wamekengeuka!.

Wanashindwaje kufahamu jinsi Yanga inavyopigwa vita kutoka kila kona, lakini kwa jitihada adimu inachechemea kwenda mbele, jambo ambalo linapaswa kupongezwa na si kubezwa km afanyavyo jamaa yetu huyo mpenda misifa asiyostahili, na tarumbeta lake linalojishadidisha eti mikia ni timu ya Mungu....labda alimaanisha Bwawa la Mungu!

Shime wanajangwani na wapenda soccer wasiache kuichangia timu ya wananchi ambayo inapitia fitna, na vikwazo lukuki vinavyolenga kuidhoofisha timu ya wananchi...Walishindwa, Wameshindwa na Watashindwa...Daima mbele!!!!
 
Well said mkuu,Nina uhakika Yanga itapitia wakati mgumu sana pia kama huyu kocha akitikiswa .. to be honest, kinachoibeba yanga kwa sasa ni spirit ya Zahera ila kiuchumi wako dhooful hali.

Serikali ikaebali na soka!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Maisha Kupokezana mbona hata Sisi Simba SC tuliumia na kuteseka mno wakati wa awamu ya JK na Serikali yake? Watu wa Simba SC tulikuwa ' hatupumui ' na tulinyanyasika sana hadi wengine tukapoteza ' Nuru ' zetu Usoni. Asante Serikali ya Awamu ya Gwala / Tano chini yake Jemedari, Mwanamume na Shujaa Rais Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ( ambaye ni Mnazi Kindakindaki na LiaLia ) wa Simba Sports Club bila kumsahau Waziri Mkuu wake, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, 75% ya Baraza lake la Mawaziri ni ' Mnyama Mnyamani ' tupu achilia mbali ' Watendaji ' wake wengine.

Yanga SC watulie tu na ' tutawatesa ' hadi 2025 na sasa hivi tunataka Kuhakikisha hata Rais atakayekuja ' Kumrithi ' JPM nae lazima awe ni mwana Msimbazi mwanzo mwisho. Yaani tunataka ' tuwanyanyase ' na ' tuwatese ' Yanga hadi watuombe radhi / msamaha huku wakitunyooshea mikono. Awamu ya Nne ya Rais Mstaafu Kikwete ' ilitutesa ' mno na sana wana Simba SC hivyo sasa na Sisi ' tunenepe ' na Awamu hii ya JPM wetu.

Watuvumilie tu kwakweli hakuna namna!
 
Wakati akizungumza hayo alikuwa tayari ameshakunywa mbege, hivyo tunamsamehe ila aendelee na kazi yake kama mkuu wa wilaya na atuachie na yanga mbovu ambayo ni ya wananchi.
 
Ok, ila kumbuka kwa sokala bongo hakuna SIMBA imara bila YANGA imara!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Serikali inafanya kila sehem ni siasa za kutukuzana, nimemuona waziri juzi kavaa mshati wenye bendera mbili, ila kiukweli ule ni unafiki wa hali ya juu maana watu wanamfahamu yuko chama lipi na pia zengwe analowapiga wana jangwani!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimdharau sana kuvaa ile shirt, kiukweli taifa linapitia kipindi kigumu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yanga ilivyokuwa bora haikufungwa 5 na Al Ahly Misri Mechi mbili...
 
Nukuu ya mwinyi Zahera na hiyo no 6 ni ya kijinga sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilitegemea mkuu wa wilaya na mpenzi kindakindaki wa Yanga anafahamu vizuri timu inavyopita katika kipindi kigumu, na nilitegemea Shabiki huyu angalau angemshukuru Kocha kwa kuwafanya wachezaji wawe na morari ya kucheza katika mazingira magumu.

Yaani kwa mtazamo wangu Jerry kachemsha kwa kumsema vibaya kocha, kama kweli hivi ndivyo alivyosema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…