Hatimaye J.K Kafanikiwa kunywa maji na kuchafua kisima | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye J.K Kafanikiwa kunywa maji na kuchafua kisima

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dawa ya Maralia, Jul 17, 2011.

 1. D

  Dawa ya Maralia Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niwape wadau wa JF kwa kazi nzuri mnayoielimisha jamii kupitia mtandao huu, salute kwenu.

  Nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa CCM toka wameanzisha operesheni hii vua gamba, ukiafuatilia kwa makini kabisa(jaribu kufikiri angalau kwa dk 5) ndugu zanguni, unajiuliza hivi gamba ni lipi ndani ya CCM wao wanadai eti ni wenzao wa 3 (EL,RA,AC) nimewafuatilia kwa makini hawa jamaa kwa mujibu wa kashfa na tuhuma ambazo wanazo tukianza na AC yeye ana kashfa ya RADA, RA yeye ana tuhuma za Kagoda,EL yeye Richmond sasa je walichukua imprest za hela hizo peke yao bila Ikulu, Wizara au mamlaka husika bila kubaliki mchakato huu, nikitu kisichowezeka kabisa hata ndani ya familia tu Mama au Baba afanye manunuzi makubwa bila hata mwenzake kujulishwa wakati mwingine hata watoto wanajulishwa sembuse serikalini. Wana JF huu ni usanii wa kupindukia tatizo sisi Watz ni mambumbu wa kupindukia hatuchambui mambo kwa umakini matokeo yake tuna ushabiki wa kupindukia na hili ni tatizo kwa taifa, Pesa ya serikali haitolewi na mtu yeyote hata Rais ha uwezo huo bila kuwashirikisha watu wa karibu yake sasa haikupaswa kuwalaumu hawa jamaa especially lawama tunazozitoa sisi wananchi moja kwa moja kwao ni kosa kubwa na tunatenda dhambi kubwa wanaJF.

  Kwa hili ilipaswa watu wailaumu moja kwa moja, Kilichotokea hapa watu walitafuta hela ya kuwasidia kutawala na hawa jamaa walikuwa ni migongo ya kupitishia fedha kutokana na mamlaka yao au uwezo wao, kwa wale wanaokumbuka mwaka 2005 hawa jamaa walipewa jukumu la kutafuta fedha usiku na mchana hawalali ili mwenzao apate sasa kilichotokea baadhi yetu JF tunajua kabisa mwenzao amewageuka (kwa lugha nyingine kama kichwa cha habari kinavyozungumza), Unajua ukiwa mswahili ni mswahili tu jamaa kawatosa wenzake kwa ambae angekuwepo Mbeya kwenye maandamano yao ya juzi ilishangaza wamechukua watu toka vijijini huko wanashindia maji aibu, Agenda za kuzungumza hawana Sendeka,Sitta,Mwakyembe,Nape wanaongea vitu havina mpangilio kabisa,inaonyesha dhahiri wametumwa na Chairman kuwaponda hawa jamaa hii ni dharau kabisa kwa wananchi Sitta anasema tatizo la umeme ni mikataba wanaiangalia, wanaingalia miaka mingapi? eti Sendeka anasema Uamuzi mgumu hata machizi wanaweza kuuchukua Serikali inachukua uamuzi makini, Jamani Serikali hii ya awamu ya 4 uamuzi upi makini wameuchukua mpaka sasa kuleta ahueni ya maisha ya mtanzania wa kawaida hebu yeyote aorodheshe. Sasa hivi ukiwa nchi za wenzetu ukisema mimi mtanzania unaona aibu nchi ipo gizani,Rais hana speech itakoyoweza kumvuta hata mtu wa kawaida kumsikiliza kwa sasa alishatoa kauli taifa kuwa gizani itakuwa ndoto matokeo yake imekuwa vise versa hivi nani anamshauri Rais kwa sasa Watanzania ifike mahali tuwatafute washauri wa Rais tuwajue na kama wapo kwa kweli wanastahili laana ya kutupwa haiwezekana Mhe. Rais anafanya vitu vya ajabu mpaka watu ambao hawajaenda shule wanashangaa ameita Mawaziri,Makatibu na Manaibu wao Dodoma wanakaa kuwasuta eti ni semina elekezi hivi kweli Mwananchi wakawaida anapaswa kujua mawaziri na manaibu mwaziri hawaelewani au waziri anashindwa kutoa taarifa mpaka ampigie yeye. WanaJF gamba lipo moja tu likitoka hilo Tanzania Bora tutaiona tuendelee kuomba Mungu haya yatimie siku zote malipo ya dhambi zote yapo hapahapa duniani tuendelee kuomba mungu atujalie moyo wa uvumilivu lakini ukweli utakuja kuonekena no matter itachukua muda gani.

  Mungu Ibariki Afrika,Mungu Ibariki. Tanzania.

  Ahsanteni.
   
 2. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Jk mtoto wa mjini!
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  na hao anaowatumia sasa atawtema tu ka anavyowafanyia maswaiba wake wa 2005
   
 4. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #4
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tatizo la Nape ni limbukeni, hajifunzi kutokana na yale yaliyowakuta wenzake. Anajiona yeye ndo kaukata sana. Namuonea huruma kwakuwa bado ni kijana. Akiharibu CV yake leo ndo basi tena.
   
 5. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #5
  Jul 17, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mkuu kawatumia jamaa na kawatosa, hivi sasa hakuna kitu kitu kitakachowasafisha!
   
 6. K

  Kilongayena Member

  #6
  Jul 17, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tatizo la serikali yetu ya CCM mzaha na usanii mwingi, nina uhakika EL,AC Hawatajiuzuru kwa sababu ya utoto aliokuwa nao Nape na wenzake kina Sitta na hapo ndo tutakapoiona picha kamili shauri yao bwana.
   
 7. H

  Handsome Member

  #7
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 87
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ila siku ikifika Nape ataikimbia Nchi,am sure,tatizo lake hajui What goes arround is what comes arround,
   
 8. Nzowa Godat

  Nzowa Godat JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 15, 2011
  Messages: 2,630
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Mjini bwaga moyo au mla ndisi au chali nzi.
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hahahaaa,tena k'ko0o
   
 10. s

  seniorita JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 674
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukitafuna muwa na kumeza maji yake yenye sukari si mwisho utatema tu makapi? Habari ndio hiyo
   
 11. D

  Dawa ya Maralia Member

  #11
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nape ushauri wangu wa bure tu hebu achana nasiasa za kihuni hizo wewe bado mtoto sana, hivi unashindwa kufikiria wazee wazima kama msekwa wametulia tu,hao jamaa unaowasema hivyo wanaijua serikali mwanzo mwisho J.K mwenyewe ana wajua hao bila wao Urais angeusikia
   
 12. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  JK ni born town. Kama hadithi za sungura vile.
   
 13. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  bwagamoyo palikuwa mjini kabla ya Dar!
   
 14. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #14
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mkuu mimi ni malizie gamba ni ccm yenyewe. Nadhani tunahitaji nchi ijivue gamba yaani kuiondoa ccm.

  CDM njooni na kauli mbiu ya kuivua gamba Tanzania ambalo ni ccm.
   
 15. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #15
  Jul 17, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mimi nadhani kujivua gamba kwa R.A ni move iliyoandaliwa kwa ajili ya kumvunja nguvu Lowasa. Ionekane kuwa watuhumia wengine wanajiondoa lakini yeye ni mkaidi.

  Tujikumbushe sababu kuu ya R.A kuachia ngazi, akisema kuwa ameamua kufanya hivyo kwa maslahi ya biashara zake. Rostam ni mfanya biashara wa kimataifa kama alivyosema yeye, uamuzi umelenga katika kuokoa reputation ya biashara zake.
  Chenge na Lowasa ni wanasiasa pure, hususani Lowasa,leo hii umtoe Lowasa kwenye siasa halafu akafanye nini? Kila mtu hutamani kupiga hatua ya mbele kwa kila anachofanya, Lowasa hatua yake ya mbele ni Ikulu, na si siri utendaji wake hata raia wa kawaida wanaukubali.

  Hili ni tishio sana kwa mtandao ambao unaongozwa na akina Sitta, kama jamaa akichaguliwa kuwa mgombea basi chama kitagawanyika na ndiyo mwisho wa ccm. Itakuwa ngumu sana kumuondoa jamaa katika nafasi yake na kufifisha ndoto zake za ikulu, maana anao utetezi kuhusu Richmond,na anapewa support kubwa ndani ya chama. Sipati picha siku akiitisha mkutano na waandishi wa habari au akaitisha mkutano wa hadhara kufight back. Jamaa ananguvu, naamini si ndani ya ccm tu bali hata nje kwa wananchi.
   
 16. D

  Dawa ya Maralia Member

  #16
  Jul 17, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na ndio hatari inayokuja Joss
   
Loading...