MeinKempf
JF-Expert Member
- Jun 11, 2013
- 11,094
- 7,225
Katika kuonesha kwamba yuko serious na ishu ya mauaji na uvunjifu Wa amani unaoendelea mkoa wa pwani katika maeneo Hasa ya kibiti, mkuranga, jaribu, na maeneo mengineyo.
Leo 06 /06/2017 Amekwenda mwenyewe eneo la tukio kuonana na wazee Wa maeneo hayo na kuzungumza nao ili kupata maoni yao ambayo wakichanganya na mbinu zao watawashinda hao wadharimu wanaokosesha raha na amani RAIA wasio na hatia.
Hatimaye mkuu Mpya Wa Jeshi la polisi Tanzania Afande IGP umeamua kuingia front line mwenyewe kama kamanda mkuu baada ya hiki leo Jumanne 06 June 2017 kuibukia pande za kibiti na mkuranga yeye mwenyewe ili kujaribu kupata Picha halisi ya kinachoendelea eneo Hilo.
Hakika kitendo hicho ni cha kishujaa na kimewatia moyo wapambanaji Wetu walioko humo wakijitahidi kupambana kuweka hali ya hewa iwe shwari .
Maana mkuu IGP sirro katoka humo jioni (wale Wa barabara ya kilwa road na Mandela road mpaka pande za tazara mtakuwa mlipishana na msafara wake jioni ya leo mida ya kumi na mbili akirudi). Hongera kamanda mpambanaji.
Hakika huyu ndiye kiongozi tuliyemtaka, kwani ana uthubutu Wa kwenda mstari Wa mbele na kuongea na vijana wake katika kujua Nini kinatakiwa kufanyika.
Hongera mkuu IGP Sirro kwa kuanza kazi yako vizuri. Naanza kuona kauli ya hapa kazi tu unaweza vaa viatu vyake.
Video ya ziara yake kibiti na mkuranga hiki hapa.
Hongera IGP sirro, kwani hii imeanza nikumbusha enzi za kamanda mstaafu Venance Tossy, aliyekuwa Mkuu Wa mafunzo na operation wa zamani Wa polisi Tanzania.
Je Nini maoni na kushauri wako kwa Afande IGP ili kutatua changamoto ya pwani Hasa mauaji ya kibiti, mkuranga, jaribu, n.k