Hatimaye! CCM yafikiia tamati ya utawala wake

mavumbi

JF-Expert Member
Joined
Feb 8, 2013
Posts
596
Reaction score
328
Hayawi Hayawi Yamekuwa!

Akina Karl Marx huko nyuma waliyasema - na sio kwa kutabiri bali kwa kutafakari michakato na mwelekeo wa mabadiliko ya kiuchumi na Kijamii - Kwamba utafika wakati mfumo fulani utajichokea wenyewe kwa sababu za michakato inayopitwa na wakati, misuguano, mivurugano ya ndani ambayo itawafanya wadau wake kuchokana wenyewe kwa wenyewe, na wanaosubiri kupata riziki kupitia mfumo huo uliopo kukata tamaa.

Hayati Nyerere alianza na falsafa ya kugawana riziki kupitia sera za udhibiti wa rasilimali za taifa ili kuondoa tofauti za kipato miongoni mwa wananchi na wote tuwe sawa.
Ustaadhi Mwinyi akaja na sera za soko huria ili kuwainua wananchi katika kutafuta riziki na kuupiga vita ukabwela usio wa lazima.
Mkapa akaja na sera za ubinafsishaji na juhudi za kubana mianya ya ukwepaji ukusanyaji wa mapato ili serikali iwe na nguvu ya kiuchumi kwa maslahi ya wananachi wake.
Bwana Kikiwete amefanya kazi kubwa sana ya uendelezaji wa miundo mbinu ya kitaifa ili kufungua milango ya kifursa za kibiashara na uzalishaji, na uwekezaji wa nguvu sekta zote.

Yote haya yaliyofanikiwa na yasiyofanikiwa yamefanyika chini ya uongozi wa Chama Tawala, ambacho sasa kinaelekea kuishiwa sera na hatimaye kubakiwa na dhana ya kutafuta "mtu ama watu" wa kuwatwisha mzigo wa udereva wa nchi hii, badala ya sera na mikakati inayoonekana itawahakikishia WaTz nafuu na maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii.

Na ndio sababu tunaona kina Membe, Makufuli, Sita, Ngoyayi, na wengine wakihamasishwa kujitokeza, na kupigiwa debe huku na huko, ili watafute fursa ya uongozi, bila kujali mustakabali wala muktadha wa sera za Chama hiki na ahadi zake kwa Wananchi.

Ni wazi kabisa hiki Chama kikongwe kimefikia hatua ya uzee, kuchoka, na hatimaye kuchokwa na Watz walio wengi.
Mivutano iliyomo ndani ya chama endapo itafikia hatua ya kuteuliwa mtu kugombea uongozi ati kwa kuwa kuna dhana ya "anapendwa na Wengi" ambayo haina mashiko zaidi ya hisia na sababu za kimaslahi za wapiga debe wake, ndipo maneno ya kina Marx yatakapo dhihirika kwa kuwa siku zote JAMII SIO MGANDO, BALI HUBADILIKA KWA KUWA NDIO MAUMBILE YAKE.

Na hiki Chama kikongwe kitajikuta kikihifadhiwa kwenye dampo la taka taka za historia.

Ni suala la muda tu......Just a matter of Time.

Hili swala ni dhahiri....yaaan CCM wangejua jinsi ambavyo siwapendi na nimewachoka , wangeondoka tu madarakani kabla ya uchaguzi....Muda ukifika hata uibe kura inashindikana...

Ukawa Tusiposhinda mwaka huu kwa utawala wa kikwete basi tusahau IKULU...
 
Mkuu nikweli,naliona anguko kubwa la Chama kikongwe na hii ni fursa pekee kwetu mana wenzetu wameelekea kibra
 
Wakoloni Weupe Walivyoona Watanganyika Wako Silias Wanaitaka Nchi Yao, Wakaachia Wenyewe Bila Kusubili Kumwaga Dam Lakini Bahat Mbaya, Ikaende Kinyume Na Matalajio Ya Wengi Na Hatamie Ikaangukia Kwa Mkoloni Mweus Ccm, Sasa Tuko Silias Tunaitaka Nchi Yetu, Tunataka Tujitawale Wenyewe, Tunaiomba Ccm Iachie Madaraka Bila Kusubili Kumwaga Dam.
 
Kuna kila dalili chama kongwe kilichobakia madarakani Kwa muda mrefu kinakwenda kuzikwa rasmi Oct 15. kwani hata wenyewe Kwa wenyewe wamechokana achilia mbali wale wapenda mabadilio ambao ndio wengi nikiwamo na mimi , ni muda tu.
 
Hayawi Hayawi Yamekuwa!

Akina Karl Marx huko nyuma waliyasema - na sio kwa kutabiri bali kwa kutafakari michakato na mwelekeo wa mabadiliko ya kiuchumi na Kijamii - Kwamba utafika wakati mfumo fulani utajichokea wenyewe kwa sababu za michakato inayopitwa na wakati, misuguano, mivurugano ya ndani ambayo itawafanya wadau wake kuchokana wenyewe kwa wenyewe, na wanaosubiri kupata riziki kupitia mfumo huo uliopo kukata tamaa.

Kasi ya maendeleo haiendani kabisa na kodi pamoja na mikopo wanayokopa ambayo mwisho mlipaji ni mwananchi, sababu wao hata PAYEE nasikia wamejisamehe.
 
Wakoloni Weupe Walivyoona Watanganyika Wako Silias Wanaitaka Nchi Yao, Wakaachia Wenyewe Bila Kusubili Kumwaga Dam Lakini Bahat Mbaya, Ikaende Kinyume Na Matalajio Ya Wengi Na Hatamie Ikaangukia Kwa Mkoloni Mweus Ccm, Sasa Tuko Silias Tunaitaka Nchi Yetu, Tunataka Tujitawale Wenyewe, Tunaiomba Ccm Iachie Madaraka Bila Kusubili Kumwaga Dam.

Mkuu, Chama kongwe ni chama cha waoga.....cowards. Tegemeo lao kuu ni Majeshi ya ulinzi na usalama, ambayo nayo hivi sasa yamechoshwa na ufisadi na umasikini wa wazi kabisa. Kazi iliyopo ni kuwatoa woga Watz wa kawaida ili kuleta mabadiliko.
 
Hayawi Hayawi Yamekuwa!
Hayati Nyerere alianza na falsafa ya kugawana riziki kupitia sera za udhibiti wa rasilimali za taifa ili kuondoa tofauti za kipato miongoni mwa wananchi na wote tuwe sawa.
Ustaadhi Mwinyi akaja na sera za soko huria ili kuwainua wananchi katika kutafuta riziki na kuupiga vita ukabwela usio wa lazima.
Mkapa akaja na sera za ubinafsishaji na juhudi za kubana mianya ya ukwepaji ukusanyaji wa mapato ili serikali iwe na nguvu ya kiuchumi kwa maslahi ya wananachi wake.
Bwana Kikiwete amefanya kazi kubwa sana ya uendelezaji wa miundo mbinu ya kitaifa ili kufungua milango ya kifursa za kibiashara na uzalishaji, na uwekezaji wa nguvu sekta zote.

Na ndio sababu tunaona kina Membe, Makufuli, Sita, Ngoyayi, na wengine wakihamasishwa kujitokeza, na kupigiwa debe huku na huko, ili watafute fursa ya uongozi, bila kujali mustakabali wala muktadha wa sera za Chama hiki na ahadi zake kwa Wananchi.

Mivutano iliyomo ndani ya chama endapo itafikia hatua ya kuteuliwa mtu kugombea uongozi ati kwa kuwa kuna dhana ya "anapendwa na Wengi" ambayo haina mashiko zaidi ya hisia na sababu za kimaslahi za wapiga debe wake, ndipo maneno ya kina Marx yatakapo dhihirika kwa kuwa siku zote JAMII SIO MGANDO, BALI HUBADILIKA KWA KUWA NDIO MAUMBILE YAKE.

Mkuu Mavumbi umenena! Ila katika wote hao wanne waliongoza huyu tuliye naye ndiye aliyejaribu kuleta mabadiliko ya nguvu kwa kutambua na kuzisoma alama za nyakati....
1. Amefungua milango ya fursa za elimu kwa vijana wengi zaidi haijapata kutokea...changamoto yake ajira
2. Ametoa uhuru mkubw sana kwa mawasilinao nahabari kupitia vyombo na media mbalimbali
3. Ameshiriki moja kwa moja katika kuinua michezo na burudani...changamoto yake viwango dhaifu vya washidani wetu
4. Kubwa kuliko yote...ameanzisha mchakato wa kupatikana kwa Katiba Mpya.

Acha Chama Kongwe kife lakini historia itawakumbuka viongozi waliotuinua
 
Vimebaki visiku vichache tu kuuzika utawala dhalimu
 
Back
Top Bottom