Mwanzi1
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 6,000
- 4,586
Kwa imani kubwa nilio nayo, kuna watu ambao walikuwa bado na dukuduku la kuendeleza vuguvugu la uchaguzi mkuu 2015. Maandamano yaliyoshindikana yameweza kuhitimisha siasa za "kiuchaguzi" ili kutoa fusra kwa siasa za "kuendesha". Japo tumechelewa kwa sababu kadhaa ikiwemo baadhi yetu walikataa kuachana mihemko ya kiuchaguzi, lakini watanzania walio wengi kutumia werevu wao, wameonyesha ishara kwamba ni wakati wa kufanya kazi. Siasa hazitaisha ila zina wakati wake, tujaribu kutambuwa nyakati muafaka wa siasa za kiuchaguzi na siasa za kimaendeleo.