Hatimae ngalangala (Noah Voxy) nimeliuza

wakati mwingine kumiliki gari ni sawa ni kujibebesha gunia la misumari
Kuna mama mmoja analo jeusi anafanya catering service alikuwa anapeleka msosi kwenye sherehe ya send off.Lilimzimikia ghafla mataa ya magomeni alipatwa na pressure akalazwa.

Kilikuu yake nayo spana mkononi.Anasema hataki kuyasikia tena.Hana hamu na Noah voxy.
 
Baada ya kuhangaika na Noah voxy ambalo kwa muonekano wa nje linaonekana jipya(pamba) au wanasemaga in mint condition ila ilitaka kunifirisi...
Umelaumu sifa za Brevis,lakini Voxy tatizo lake ni ulaji mkubwa wa mafuta na body laini sana,shuda ulizozisema ni ulikua hutengenezi gari ikazaa matatizo mengi kupita kiasi
 
Inaonekana ulinunua kimeo mkuu. Hizo gari sio mbovu kiasi hicho. Inaonekana ilishapata shuruba za kutosha kabla ya kutua mikononi mwako.

Wakati mwingine bodi za gari na maileji zinatudanganya sana kuhusu ubora wa gari
 
Kuna mama mmoja analo jeusi anafanya catering service alikuwa anapeleka msosi kwenye sherehe ya send off.Lilimzimikia ghafla mataa ya magomeni alipatwa na pressure akalazwa.

Kilikuu yake nayo spana mkononi.Anasema hataki kuyasikia tena.Hana hamu na Noah voxy.
Kuna siku tulikuwa na safari alfajiri
Asubuhi tumepakiza mizigo kwenye kirikuu chetu tuwahi stendi si kikagoma kuwaka kabisa.. ....
Kirikuu navyo majanga tupu
 
Afu ukimiliki gari kimeo yaani unakua mtu wa mizinga tu kila mtu unampiga kizinga yaani mtu wa kudaiwadaiwa tu. Mpaka washkaji wanakukataa. Speaking from experience.
 
Niliwahi kununua Noah new model kutoka Japan, injin ilikuja vipande vipande... Clearing agent naye akapoteza document.. Gari ilikaa bandarini miezi mitano.. Nilipofanikiwa kulitoa, nikaliuza faster!
Bandarini miezi mitano? kwa charge ya bandari hii yetu, au ulihamishia bond warehouse?
 
Back
Top Bottom