hatimae ivo mapunda aitwa taifa star

hatimae ivo mapunda aitwa taifa star

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,077
Reaction score
64,247
Ivo mapunda ameitwa katika kikosi cha taifa star na vilevile wameitwa wachezaji wanne wa mbeya city. Amesema kaita wachezaji wengi ambao atawafanyia mchujo baade. Mia
 
Sidhani kama unafahamu mpira vizuri, Mwombeki ni straka mzuri sana anaejua kutumia akili awapo uwanjani.

Kafanya nini hadi sasa? Hilo ndio swali langu la msingi...

Huwezi kuwaacha watu wenye takwimu nzuri halafu uingize watu kisa wana majina marahisi mdomoni.

Ukimtetea Mwombeki, kuna mwingine atakuja kukuambia Tegete ni straika mzuri na anajua sana kutumia akili...
 
Hivi kumbe bado kuna timu ya taifa ya mpira wa miguu? hahahaha mi nilijua wameidisolve!
 
mkuu mombeki kiwango bado ni mvivu hakabi na mzito kwenye maamuzi alaf ata takwimu zinamuangusha, ana goli 2 mechi 9

Kuna bwana mdogo hapo juu naona anatokwa povu tu...halafu sikujua kumbe ana posts mbili tu tokea mwezi wa tatu
 
mbeya city........ wamechukuliwa wanne...... habari njema hizi.....viva mbeya city nafikiri inaweza ikawa ndo timu ya kwanza ya mkoani kutoa wachezaji wengi
 
Wachezaji 16 wa kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Novemba 12 mwaka huu kinaundwa na Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).



Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).



Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.
 
Kuna jambo moja watu wanashindwa kulielewa...Kim Poulsen ameita vikosi viwili tofauti:

1. Kikosi cha kwanza amekipachika jina ya 'Future Young Taifa Stars'.... Huku ndio 'babu' Ivo Mapunda kaitwa na kikosi hiki kitatumika kunyofoa wachezaji kwa ajili ya timu kubwa ya Taifa Stars.

2. Kikosi cha pili ndio Senior timu ambayo ni 'Taifa Stars'...Huku 'babu' Ivo Mapunda hayupo kabisa.

Hicho kikosi cha kwanza baada ya mchujo, kitatoa wachezaji 10 watakaojumuishwa katika timu ya Kilimanjaro Stars kwa ajili ya mashindano Chalenji huko Kenya.

Mchujo wa kuwapata hao wachezaji 10 utafanyika wakati "Future Young Taifa Stars" itakapokabiliana na "Taifa Stars" uwanja mkuu wa Taifa mnamo Novemba 13.

Wachezaji 16 wa Taifa Stars:

Ally Mustafa (Yanga), Mwadini Ali (Azam), Aggrey Morris (Azam), Kelvin Yondani (Yanga), Shomari Kapombe (AC Cannes, Ufaransa) na Nadir Haroub (Yanga).

Erasto Nyoni (Azam), Vincent Barnabas (Mtibwa Sugar), Salum Abubakar (Azam), Mwinyi Kazimoto (Markhiya, Qatar), Frank Domayo (Yanga), Athuman Idd (Yanga), Mrisho Ngasa (Yanga), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), Mbwana Samata (TP Mazembe, DRC) na John Bocco (Azam).

Wachezaji 30 wa Future Young Taifa Stars:

Makipa Aishi Manula (Azam), Hussein Shariff (Mtibwa Sugar) na Ivo Mapunda (Gor Mahia, Kenya).

Mabeki ni David Luhende (Yanga), Hassan Mwasapili (Mbeya City), Himid Mao (Azam), Issa Rashid (Simba), Ismail Gambo (Azam), John Kabanda (Mbeya City), Kessy Khamis (Mtibwa Sugar), Michael Pius (Ruvu Shooting), Miraji Adam (Simba), Mohamed Hussein (Kagera Sugar), Said Moradi (Azam) na Waziri Salum (Azam).

Viungo ni Amri Kiemba (Simba), Farid Mussa (Azam), Haruni Chanongo (Simba), Hassan Dilunga (Ruvu Shooting), Jonas Mkude (Simba), Khamis Mcha (Azam), Ramadhan Singano (Simba), Simon Msuva (Yanga), William Lucian (Simba).

Washambuliaji ni Elias Maguli (Ruvu Shooting), Hussein Javu (Yanga), Joseph Kimwaga (Azam), Juma Liuzio (Mtibwa Sugar), Mwagane Yeya (Mbeya City) na Paul Nonga (Mbeya City).

Nukuu:

Kim amesema kikosi cha Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager chenyewe kitaingia kambini Novemba 12 jijini Dar es Salaam ambapo siku inayofuata ndipo kitakapocheza mechi na Future Young Taifa Stars.

Baada ya mechi hiyo, kambi ya Future Young Taifa Stars itavunjwa wakati Taifa Stars itaondoka Novemba 14 mwaka huu kwenda Arusha ambapo itaweka kambi na kucheza mechi ya kirafiki ya kimataifa kabla ya kwenda Nairobi, Kenya kwenye michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika kuanzia Novemba 27 hadi Desemba 12 mwaka huu.

Wachezaji wengine kumi kutoka Future Young Taifa Stars baadaye wataongezwa katika kikosi kitakachounda timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars) kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji.
 
Back
Top Bottom