Hatima ya Mkapa bungeni wiki ijayo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatima ya Mkapa bungeni wiki ijayo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 1, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Hatima yake bungeni wiki ijayo

  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

  JINAMIZI la shutuma limeendelea kumwandama Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, kudai kiongozi huyo alipoteza dira na kuifanya nchi ielekee kusikojulikana.

  Aidha, Lipumba alisema kiongozi huyo hakuwa na mtazamo wa muda mrefu, jambo ambalo hata viongozi wengi wa sasa wameangukia katika mkumbo huo.

  Anatoa sababu za viongozi hao kuingia huko kwa kushiriki kwa kasi kubwa katika vitendo vya ufisadi bila kujali masilahi ya taifa.

  Kauli hiyo ya Lipumba dhidi ya Mkapa imekuja huku kukiwa shinikizo kubwa kutoka kwa baadhi ya wananchi na wabunge kutaka kiongozi huyo aondolewe kinga ili aweze kupelekwa mahakamani kwa tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka.

  Profesa Lipumba alitoa kauli hiyo juzi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uchaguzi mdogo wa ubunge katika Jimbo la Mbeya Vijijini uliomalizika hivi karibuni na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuibuka na ushindi.

  Alisema kiongozi anapokosa dira ya kuona mbali humfanya ajione ana uwezo wa kufanya kila kitu kwa muda huo, bila ya kufikiri kuwa jambo analolifanya litakuwa na madhara kwa taifa au litakuja kumletea matatizo pindi aondokapo madarakani.

  “Mkapa hakuwa na dira ya mbali, ndiyo maana yeye na viongozi wenzake walijihusisha katika mambo ya kifisadi na hivi sasa baadhi yao ndio wanaanza kuumbuka kwa kupelekwa mahakamani,” alisema Profesa Lipumba.

  Alisema sifa kubwa ya kiongozi ni kujenga misingi imara ya maendeleo ya muda mrefu, lakini si kufikiri namna ya kutapanya rasilimali za taifa kama inavyoonekana hivi sasa.

  “Tupo njia panda, hatujui tuendako, kwani viongozi wamejisahau kiasi cha kujikuta wanabomoa misingi ya maendeleo badala ya kuijenga nchi kama wengi tulivyotarajia,” alisema Profesa Lipumba ambaye kitaaluma ni mchumi.


  Wakati Lipumba akimchambua Mkapa, hatima ya kuondolewa au kutokuondolewa kinga kwa kiongozi huyo wa awamu ya tatu inatarajiwa kujulikana kuanzia kesho katika vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini Dodoma iwapo hoja ya kufanya hivyo itawasilishwa.

  Habari ambazo Tanzania Daima Jumapili imezipata zinadai kuwa kuna mgawanyiko mkubwa miongoni mwa wabunge kuhusu suala hilo, huku idadi kubwa ikionekana kumkingia kifua.

  Baadhi ya wabunge wanaodaiwa kumkingia kifua, wakiwemo wa kambi ya upinzani, inadaiwa wanafanya hivyo ili kumnusuru kiongozi huyo na wengine wanaoshiriki kwa namna moja au nyingine kwa matumizi mabaya ya madaraka.

  Tayari Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo ‘Ndesa Pesa’ (CHADEMA), alionyesha nia ya kutaka kuwasilisha hoja binafsi bungeni akitaka kinga ya Mkapa iondolewe, lakini katika siku za hivi karibuni amenukuliwa akisema hataiwasilisha hoja hiyo katika kikao kinachoendelea hivi sasa.

  Pamoja na Ndesamburo kuripotiwa kutoiwasilisha, bado mbunge yeyote anaweza kujitokeza kuwasilisha hoja hiyo ambayo ili ipite itahitaji uungwaji mkono wa wabunge wasiopungua theluthi mbili.

  Jambo kubwa lililopo hivi sasa ni kuelekeza macho bungeni kuona kama kuna mbunge atajitokeza kuwasilisha hoja hiyo inayosubiriwa kwa hamu kubwa na baadhi ya watu.

  Wakati kukiwa na joto hilo, wiki iliyopita Mkapa aliwaonya viongozi kuacha siasa za majungu, fitina, chuki, ukabila na udini, kwani wasipofanya hivyo Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 utakuwa mgumu na kuna hatari taifa likaingia katika machafuko.

  Onyo hilo alilitoa mkoani Iringa alipokuwa kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

  Alisema katika kipindi cha miaka mitatu aliyo nje ya uongozi, ameshuhudia mambo hayo kwa kiwango kinachomtia woga.

  Wakati Mkapa akitoa onyo hilo, baadhi ya viongozi wa kidini wakitumia majukwaa mbalimbali ya kidini, wamejitokeza hadharani wakimtetea, kwa kudai ni kiongozi anayestahili heshima kubwa, kwa kuwa amelifanyia taifa mambo mengi mazuri, ikiwemo kukuza uchumi wa taifa.

  Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya siasa wanabashiri kuwa kujiingiza kwa viongozi hao kunalifanya sula hilo kuchukua mkondo wa kidini zaidi kuliko kisiasa kama ilivyokuwa hapo awali.

  Wachambuzi hao wanadai kuwa, suala la Mkapa kufanywa kuwa la kidini, kuna kila dalili la kuligawa taifa kwa misingi ya kidini, hasa kuhusu utawala wa sasa unaoongozwa na Rais Jakaya Kikwete.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Saafi sana ingawa mimi huwa sio mpenzi mkubwa wa Lipumba, lakini kwenye hili tupo ukurasa mmoja.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Alipokuwa anafanya ufisadi alipokuwa Ikulu Mkapa hakukumbuka kama yeye ni mcha mungu na ufisadi mkubwa aliokuwa anaoufanya dhidi ya Watanzania tuliomchagua kutuongoza ni dhambi kubwa. Leo anaona maji yanamfika shingoni ndiyo anakumbuka makanisa na kutoa vijisenti vyake vya ufisadi ili makanisa yamtetee katika dhambi zake za kifisadi alizozifanya dhidi ya Watanzania ikiwemo kujiuzia Kiwira kwa bei ya bure katika mazingira ya kutatanisha, kuwaleta Net Group, kuuza nyumba kwa bei ya bure na kuliingiza Taifa hasara ya mabilioni, kununua ndege mkweche ya Rais, ununuzi wa Rada uliogubikwa na ufisadi, kufanya biashara akiwa Ikulu.

  Wabunge wanaomtetea wengi hawana mapenzi ya kweli na nchi yetu, wapo radhi kumtetea Mkapa kwa nguvu zao zote badala ya kuwatetea Watanzania ili kuhakikisha Kiwira inarudishwa chini ya umiliki wa Watanzania na nyumba za serikali zilizouzwa na Mkapa nazo kurudishwa chini ya miliki ya Watanzania.

  Swala la aliyayotenda Mkapa akiwa madarakani si la Uislamu na Ukristo bali ni kudharau kwake kwa maadili ya uongozi na kuamua kutuibia Watanzania tena kwa kificho pamoja na kuwa tulimuamini na kumpa dhamana kubwa ya kutuongoza. Kuyajadili mabaya aliyofayafanya Mkapa alipokuwa madarakani hakuonyeshi chuki dhidi ya Mkapa au fitina wala majungu bali ni kutaka kujua yote yaliyojiri alipkuwa madarakani kwa kuchunguzwa na kama akionekana ana hatia basi apandishwe kizimbani kujibu tuhuma dhidi yake

  Wabunge wote watakaomtetea Mkapa hawastahili kuwa wawakilishi wa Watanzania maana badala ya kuweka mbele maslahi ya Watanzania bungeni wameamua kuweka mbele maslahi ya mafisadi akiwemo Mkapa.

  Kwa Wabunge wote mtakaomtetea Mkapa, Shame on you! Wakati nchi ikiendelea kutokuwa na maendeleo yoyote miaka nenda miaka rudi lakini hamuoni haya wala aibu kuwatetea wale wezi waliokupua mabilioni ambayo yanasababisha nchi yetu isipige hatua yoyote ile ya maendeleo. Halafu mnajifanya ni wawakilishi wa Watanzania bungeni, kumbe mnawakilisha mafisadi :(
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Feb 1, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkulu Bubu maneno mazito sana na tupo pamoja hapa.
   
 5. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #5
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Muungwana FMES, lazima tuhakikishe Viongozi tunaowapa dhamana kubwa ya kutuongoza basi wanafuata miiko na maadili ya viongozi, vinginevyo tutaendelea kuwa na viongozi mafisadi ambao wanajua hata wakitufisadi Watanzania hawatafanywa chochote maana wataenda kutoa vijisenti vyao makanisani na misikitini ili watetewe na viongozi wa dini hizo na kisha kukingiwa vifua na 'wawakilishi wa Watanzania" Bungeni. Katiba ya Tanzania kamwe isitumike kuwatetea mafisadi, haikutungwa kwa ajili hiyo.
   
 6. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #6
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  BABU,
  Jambo hili limejaa siasa sana.
  Ni vigumu kujua ukweli.
   
 7. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #7
  Feb 1, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135

  Mkuu siamini kama na wewe ni mwanachama wa JF na unafuatilia ushahidi unaowekwa hapa kuhusu issues za ufisadi. Naweza kukuuliza umewahi kusikia Mkapa akikanusha tuhuma zozote za ufisai mbali na kusema niwivu, chuki na fitna? Umewahi kusikia aktoa ushahidi kuhusu kujiuzia mgodi wa Kiwira? Umemsikia akiongea lolote kuhusu EPA? Au unataka kuamini kuwa wawakilishi wetu wote na wanasiasa wanaotaka kujadili hili swala wamekuwa waongo?? au na wewe unadhani wanamuonea wivu Mkapa!!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  Feb 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,206
  Trophy Points: 280
  Mkapa anapokumbuka shuka kumekucha

  Kulwa Karedia
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu​

  WIKI iliyopita alipokuwa kwenye warsha ya siku tatu ya Umoja wa Vijana (UVCCM) Rais mstaafu, Benjamin Mkapa aliibua tena jambo ambalo Watanzania hawakutegemea kama angethubutu kusema ama kuiambia jamii ya Kitanzania.

  Alibainisha kuwa anajutia uamuzi wake wa kubinafsisha rasilimali nyingi za taifa kwa wageni huku wazawa wakibaki mikono mitupu.

  Hatua ya Mkapa kusema maneno haya naamini imetoka moyoni mwake kwa dhati baada ya kuona uamuzi aliochukuwa akiwa kwenye utawala uliwaacha wananchi wake "wakipigika" kwa maisha magumu.


  Miongoni mwetu tunajua jinsi utawala wake ulivyojikita zaidi katika ubinafsishaji mashirika, kampuni, migodi, hifadhi za wanyamapori vyote hivi vinakwenda mikononi mwa wawekezaji.

  Sio siri, leo hii mwananchi yeyote ambaye anaishi karibu na maeneo yanayozunguka mbunga za wanyama amegeuka kuwa mtumwa ndani ya taifa lake kwani amepigwa marufuku hata kukusanya kuni kwa ajili ya mahitaji yake.

  Mwananchi yeyote akikamatwa ndani ya eneo la hifadhi huyo kwanza atapokea kipigo kikali kutoka kwa askari walioajiriwa na wawekezaji, na hatimaye kufungwa jela kati ya miezi sita hadi mwaka mmoja!

  Huu ni utumwa wa utawala wa Mkapa, leo wananchi wamekuwa na wakati mgumu kupata kitoweo cha nyama pori, kimeadimika kama almasi tunasema sawa lakini nani wa kubeba lawama hizi kama siyo Mkapa na timu yake ya viongozi wa Ukweli na Uwazi!

  Kama kweli serikali yake ilikuwa ni ya ukweli na uwazi Watanzania tumeuona jamani… tumeshuhudia jinsi kauli mbiu hii ilivyowaneemesha watawala wa serikali yake na leo tunaona baadhi yao wanatinga katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kujibu tuhuma za kuingizia serikali hasara ya mabilioni ya fedha.

  Mkapa huyo huyo ndiye aliyeidhinisha kuuzwa kwa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa "Makaburu" kutoka Afrika Kusini kwa kiasi cha sh. bilioni 20 kiasi ambacho ni kidogo ukilinganisha na unyeti wa benki husika.

  Kama kweli Mkapa anajuta anapaswa kutueleza tangu NBC iende mikononi mwa "Makaburu" wamevuna faida kiasi gani? Pamoja na rasilimali zetu tulizowapatia bila ya kujua kizazi kijacho kitahitaji kutumia majengo hayo.

  Nani asiyejua serikali ya Mkapa jinsi ilivyotumia uwezo wake kuwaruhusu wawekezaji kutoka nje kufungua viwanda vingi vya samaki katika mikoa ya Mwanza, Mara, Shinyanga na Kagera.

  Baada ya kuhakikisha wawekezaji wamepata nafasi hiyo, mamilioni ya Watanzania sasa wamekuwa na wakati mgumu kupata mboga kwani wavuvi sasa wanaambulia kupata vitoto vya samaki tu tofauti na zamani.

  Lakini kibaya zaidi, wananchi wameendelea kuambulia mabaki ya samaki maarufu kwa jina la "Mapanki" licha ya serikali kukataa kuwepo kwa hali hiyo.

  Si jambo la kubisha kwamba mapanki yanaliwa na mtu yeyote; atakayebisha naomba atembelee vijiiji vya Butuguri, Butiama, Busegwe, Kiabakari, Bisarye, Bumangi, Nyakanga na Bisumwe, vyote viko mkoani Mara ili ujionee kila siku ya gulio jinsi watu wanavyonunua mapanki.

  Sasa kwa nini Mkapa ajute? Wakati alifanya hivi akitambua wazi kwamba wananchi wake wengi wana kipato cha chini ambacho hakiwezi kukidhi mahitaji yao, lakini wawekezaji walionekana bora zaidi.

  Sikubaliani na kauli yake kwamba, angelipata nafasi angelirekebisha makosa yake ! Kwanza napenda kumwambia kwamba hivi sasa milango imefungwa, tumekwishajifunza ama kwa maneno ya waswahili yasemayo "Angalia ulipojikwaa siyo ulipoangukia".

  Sasa hivi Watanzania wamebadilika siyo tena wale wa mwaka 47, sidhani kama watampigia kura za ndiyo kama zile alizopata mwaka 1995 na mwaka 2000 licha ya kuwepo upinzani mkali.

  Ya Mkapa yamekuwa funzo kwetu; kwamba tunapowapa viongozi wetu dhamana ya kuongoza taifa halafu wakashindwa kujali maslahi ya taifa na badala yake kuangalia zaidi manufaa yao, umefika muda wa kuwakataa.

  Nani asiyekumbuka jinsi Mkapa alivyosakamwa kwa tuhuma za kufanya biashara akiwa Ikulu katika utawala wake kinyume na utaratibu, lakini ameshindwa kukanusha suala hili.


  Kiongozi ambaye anawapenda wananchi wake lazima katika moja ya hotuba zake angesimama siku moja na kuwambia katika utawala wake amefanya mambo mengi lakini kuna makosa aliyofanya na kuomba msamaha kwa yaliyotokea.

  Katika moja ya hotuba za Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema, maneno haya, "Katika utawala wangu nimefanya mengi lakini yapo niliyokosea, mimi sikuwa malaika!" Huu ndiyo uungwana kwa kiongozi anayewapenda wananchi wake.

  Kwa hali hiyo ndiyo maana nasema kujuta kwa Mkapa kunanitia shaka hasa ikizingatiwa kwamba wakati anaingia madarakani aliweka bayana mali alizokuwa anamiliki, jiulize sasa wakati anaondoka madarakani mbona hakuthubutu kufungua kinywa chake juu ya anavyovimiliki.

  Naamini kwamba havisemeki na hata vikisemeka, kwa aliyesikia mali zake za awali, angepata mshtuko na kutamani kuwa rais. Je na hili pia alilijutia?

  Leo hii tukisema tuanze kazi ya kukagua mali anazomiliki Mkapa lazima tutaibua utitiri wa mali kinyume na matarajio ya wengi. Bila shaka tutakuta maghorofa, mashamba, magari, majengo yaliyopangishwa watu mbalimbali na miradi mingine ambayo ni mikubwa katika taifa hili.

  Napenda kumalizia kwa kusema, Mkapa kama kweli una uchungu wa Watanzania wenzako, weka wazi sakata la Mgodi wa Makaa ya Mawe wa Kiwira ili uendelee kujijengea heshima mbele ya umma. Japokuwa viongozi wa dini wamekuwa wakiuelezea umma juu ya usafi wako, nao pia hufikia pahala pa kuwaambia waumini wao wakiri kwa vinywa vyao.

  Mkapa kama muumini, ni zamu yako sasa kufanya hivyo, ili Watanzania waamini kuwa unaumia uonapo rasilimali za Watanzania zikimilikiwa na wageni huku zaidi ya asilimia 75, wasijue wale nini, wanywe nini. Ndiyo maana nasema Mkapa amekumbuka shuka wakati kumekucha.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 9. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #9
  Feb 1, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  BABU,
  Tatizo si Mkapa kukanusha au kutokanusha.
  Nia yangu ni kuona hoja zisizo za kisiasa zikiendeshwa bila siasa.
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Feb 1, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,324
  Likes Received: 1,791
  Trophy Points: 280
  The way nionavyo..hata kama itahukua muda mrefu kiasi gani, Mkapa na jamaa zake watasimama kuzijibu hoja za watanzania tuu.Suala la kujinufaisha kwa mali ya umma sio rahisi kulitupia chini ya kapeti hata kama ni mahiri kiasi gani.He should face the truth by humbly addressing the allegations...kuna sauti hapa inalia ikiita kjua ukweli. Si busara kuendelea kudharau
   
Loading...