Hatima ya Maisha yetu

Mla Bata

JF-Expert Member
Jan 24, 2013
6,764
13,815
Wasalaam!

It’s been a while, i definitely miss the good old days here.

RIP Warumi , kizzo Gunz, Regia Mtema na wanafamilia wenzetu wote waliotutangulia mbele za haki.

Wangari Maathai, where are you boss? i I miss you buddy.

Well, turudi kwenye mada yetu ya leo, “hatima ya maisha yetu”

Naandika uzi huu ukiwa inspired na maisha yangu na baadhi ya vijana wengi wa kizazi hiki, zipo nyuzi nyingi zimekuwa zikianzishwa na watu wengi humu wakiwa na sintofahamu na hatima ya maisha yao kwenye nyanja tofauti tofauti, either maisha kwa ujumla, mapenzi, masomo biashara na kadhalika.

Binafsi katika makuzi yangu na kujitafuta kwenye maisha, nimeshapitia mapito haya kwa namna moja au nyingine. Lipo swali kubwa lililokuwa linazunguka kila uchwao kwenye akili yangu.

Hatima ya maisha ya binadamu, ni fate (predestined), ama ni freewill??
Binadamu kwa fikra na upeo tuliopewa na Mungu maisha yetu na hatima zetu, zimeshaandikwa na hatuwezi kuzibadilisha (hatupo responsible na mustakabali na hatima zetu, sababu zilishaandikwa) ama hatima zetu zipo mikononi mwetu na sisi ndio tupo responsible na destiny zetu? Are we creating our own destiny?

Imagine unaamka asubuhi, jua la Dar es salaam linakumalizikia mwilini kutwa, jasho mpaka kwenye nyayo za miguu lakini ikifika jioni huna cha maana ulichoingiza na siku, wiki, mwezi na mwaka vinakatika, huku ukiwitness baadhi ya rafiki zako wakiachive ndoto zao za maisha, wapo wanaoolewa, wapo wanao pata appointment mpya makazini ama kupandishwa vyeo na kadhalika, lakini mambo ni tofauti kwenye maisha yako.

Kuna ndoto unaiamini kwenye maisha yako, kuna sehemu unatamani kufika kwenye maisha yako, lakini kupitia challlenges unazopitia kuna muda maswali yafuatayo yanakuja kichwani mwako.

-May be I never meant to be in these huge positions in my life, sijapangiwa kupata kitu fulani, haikuwa riziki yangu n.k

-Labda muda wangu bado
-Labda hiki ninachokifanya kazi/biashara/masomo/mahusiano siyo kitu kilichoandikwa kwaajili yangu n.k

Wakati haya yote yanatokea bado unaendelea kuwitness your fellas wakiupgrade kimaisha kila uchwao, then kuna mawazo yanakuambia, komaa tu hicho hicho unachofanya (kazi/biashara/mapenzi) labda siku moja utatoboa.

Then siku zinakatika, umri unaenda you don’t see any big changes in your life, and still you don’t know HATIMA YA MAISHA YAKO, confussion zinatawala kichwani mwako mpaka kuna muda unainamisha kichwa chini na hisia za kukata tamaa zinakuingia, you feel like you’re dying inside, Yes you are.

Inafikirisha, na inatia simanzi lakini kuna kitu kimoja hakijawahi kubadilika maana toka huu ulimwengu uwepo, Maisha ni kitu kigumu sana kukielewa, hayajawahi kuwa marahisi.

Katika kupambana na maisha na kutafuta kujua hatima ya maisha yetu kama binadamu kuna vitu tunatakiwa kuvifahamu na kuvielewa vizuri.

Fate, karma, Destiny, Freewill

Hapa naomba tuelewane kitu kimoja either wewe unaamini kwenye Mungu, ama laa, unaabudu mizimu, mawe ama Ng’ombe, hivi vitu vipo constant.

Fate

Hatima, licha ya tofauti ya imani tulizo nazo but we both believe, kiumbe kinachoitwa binadamu kimeumbwa na hatima yake, hii huwezi kuicontrol, and sometimes it will take you, all your life kujua hatma ya maisha yako, kwa imani tofauti toufauti tunaamini kila binadamu kuna mahali anatakiwa afike kwenye maisha yake, au ndio purpose kubwa ya yeye kuwa duniani ili jambo fulani litimie. “Everything happen for a reason”

Destiny

Hii ni mambo yote yanayotokea kwenye maisha ya binadamu mpaka kufa kwake, kwa kiasi kikubwa binadamu tunaweza kucontrol destiny zetu (nitaeleza).

Karma

Huu ni mjumuisho wa matukio mazuri na mabaya yanayotokea kwenye maisha yako, yakichagizwa na matendo yako yaliyopita, what goes around comes around .
Wanasema the more unafanya matendo mazuri kwenye maisha yako, nature inaattract yale matendo so tegemea kupata likely results mbeleni and vice versa is true. Hii inafanana na “Law of attractions”

Freewill

Hapa sasa, binadamu tumeumbwa na fikra na utashi, maamuzi yako ya kila siku kwenye maisha yako thats freewill, matendo unayoyafanya kila siku, we’re responsible for what we do in our lives, kuna mambo ambayo hakuna mtu anakutuma ufanye, unafanya for your own will, that will determine your destiny.

Mambo yote manne niliyojaribu kuyagusia hapo juu yana mchango mkubwa sana kudetermine hatma ya maisha yako, tuzungumze…..

Fate is always there for you, it is just waiting for your actions, fate haiji kujitambulisha kwako ili uichukue, wala haikai mlangoni ili ugongane nayo hapana, but your fate is always there for you to do a right decisions in your life.

Fate brings you opportunities but your freewill determines whether or not you take them. Wanasema you can’t change your fate but your freewill can postpone it, kwa maana hatma yako ipo pale ila matendo yako na maamuzi yako ndio yatakayoamua kujichelewesha kuifikia hatma yako.

Destiny inaamuliwa na maamuzi yako ya kila siku kwenye maisha yako either maamuzi makubwa au madogo, choices na decisions zako zitakupeleka kwenye destiny yako una mwanamke wa muonekano wa kawaida na mwenye mapenzi ya dhati kwako asiyejali unacho au huna lakini umeamua kuoa yule mwanamke anaekuvutia machoni kwa urembo na shape nzuri aliyonayo, na anafanya ufurahi hata akikuudhi, hapo unatengeneza destiny yako buddy.

Wanasema “Every small decisions that we make is responsible for creating the journey ahead of us” ikitokea yule slay queen uliemchagua akaanza vitimbi na vituko who is responsible? Now you understand? That is destiny.

Lessons fupi zitakazo kufanya upate jicho la tatu la kuona fate yako na kuwa destiny nzuri kwenye maisha yako.

-Maamuzi yako ya kila siku kwenye maisha yako, jaribu kujipa muda na kuwa makini kufanya maamuzi kwenye maisha yako, either maamuzi makubwa au madogo sababu kuna maamuzi utayafanya yatakwenda kugharimu ama kukutengenezea path nzuri kufikia hatma yako, kuwa makini na maamuzi yako.

-Pay attentions in your life, kuna kitu maisha yako yanakwambia, kuna kazi au biashara unatumia nguvu kubwa sana lakini siku zote huoni maslahi, lakini kuna kitu ukigusa tu hakijawahi kukupa matokeo mabaya, lakini ni vile hujapata jicho la kung’amua kuwa hiyo ndio njia yako ya kutoboa. Kuna mwanamke au mwanaume upo nae kwenye mahusiano lakini kila kukicha drama na maugomvi hayaishi, ila unajidanganga ngoja nikomae ivo ivo, amka bongolala.

Kuna muda kuna vitu maisha yetu yanatuambia lakini kwa sababu hatupay attention, tunashindwa kung’amua baraka tunazopishana nazo.

-Don’t lie to yourself, Sema na nafsi yako, jiambie ukweli utakuweka huru, unapata stress kuona watu wana majumba na magari ya kifahari, wakati huo ndio kwanza unasubiri mahafali yako ya chuo kikuu November/December, bro unaakili wewee? Hakuna kitu kinakuja kirahisi, there is always a price to pay, sema na nafsi yako.

-Find yourself & things you love and capable to do, kuna muda vijana tunajipa pressure wenyewe tu, jiulize unataka kuwa mtu fulani, lakini jiulize una uwezo wa kufanya jambo hilo, are you talented au are you capable to learn the knowledge needed? Ni vema ukatumia muda wako kujiuliza wewe ni nani, unaweza kufanya nini au ni mzuri wa kitu gani then go for badala ya kuota ndoto za mchana kuna kitu real unaweza kufanya na kikaexist.

-Always be GRATEFUL and THANKFUL kuna muda tunashindwa kunotice baraka zinazotuzunguka au tulizonazo kwenye maisha yetu kwa kuendelea kuwaza vikubwa tunavyovihitaji kwenye maisha yetu, ebu chukua muda wako angalia safari ya maisha yako kuna vingapi vya thamani unavyo au umepitia kwenye maisha yako na wengine hawana?

When the last time umelazwa hospital kwa ugonjwa mahututi? Unaamka salama kila uchwao badala ya kushukuru hata kwa afya ya mwili uliyo nayo unaanza kucomplain kwanini huna pesa ya kununu iphone 14, sad! Hata kiimani tunaambiwa kabla hujaomba vikubwa shukuru vile vidogo ulivyobarikiwa.

All in all, let’s be positive and aim higher, the Universe listens and Everything is possible for who believes.

Let’s meet at the top, cheers

Mla bata.
 
Mzee umenigusa hapo kwenye watu niliosoma nao wanaupgrade lakini ndo maisha ndg yangu.Kama wanangu kibao washakuwa maboss ila mimi naamini kama bado navuta pumzi bado the game is still on..ipo siku nisipopata atapata mtoto wangu.
Amen for that brother. ✊🏾
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom