Hatima ya Hamad Rashid wa CUF leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatima ya Hamad Rashid wa CUF leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Xuma, Dec 27, 2011.

 1. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  27 December 2011

  Kizitto Noya

  HATIMA ya uanachama ya Mbunge wa Wawi (CUF), Hamad Rashid Mohamed inatarajiwa kujulikana leo atakapojieleza mbele ya Kamati ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho.

  Hatua hiyo inakuja siku chache baada ya Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila kuvuliwa uanachama na chama chake hicho kwa madai ya kukiuka maadili na katiba ya chama ambayo kwa kiasi kikubwa yanafanana na yale yanayomkabili Hamad.

  Hamad hivi karibuni amejikuta katika mgogoro na baadhi ya viongozi wa makao makuu ya CUF baada ya kutangaza kuwania nafasi ya katibu mkuu wa chama inayoshikiliwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Shariff Hamad na kuanza kupita kwenye matawi akigawa misaada, hatua ambayo ilisababisha vurugu katika matawi aliyopita huku tukio katika Tawi la Chechnya lililopo Manzese, likisababisha umwagaji damu baada ya wanachama wanaomuunga mkono kupambana na walinzi wa Blue Guard.

  Baada ya vurugu hizo, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema Hamad angeitwa mbele ya kamati hiyo na jana, taarifa ya CUF ilisema mbunge huyo leo atahojiwa na kamati hiyo kwa tuhuma za kuvunja katiba ya chama hicho.

  Kwa mujibu wa Katiba ya CUF, adhabu ya kosa la kuvunja Katiba ya chama ni kupewa onyo kali, kusimamishwa au kufukuzwa uanachama.Hamad Rashid mwenyewe, alithibitisha kuitwa kwenye kikao hicho na wanachama wenzake 13 wanaomuunga mkono.

  "Ni kweli nimeitwa lakini tuko wengi kidogo. Wameniandikia barua kuniita kwenye Kamati ya Nidhamu na Maadili kesho (leo), ila nasikitika kwamba walianza kunihukumu kabla ya kunisikiliza," alisema Hamad.

  Kuhusu alichoitiwa Hamad alisema: "Wanasema nimevunja Katiba ya chama," huku akirejea adhabu zilizoanishwa kikatiba juu ya kosa hilo.Lakini, akionekana kujua kitakachomtokea kwenye kikao hicho, Hamad alisema kuwa atakata rufaa kupinga uamuzi wa kufukuzwa uanachama.

  "Mimi kuitwa nilitarajia lakini hofu yangu ni kwamba wameshanihukumu kabla ya kunisikiliza. Ila msimamo wangu bado uko palepale, nitakata rufaa kupinga adhabu ya kufukuzwa uanachama," alisema.

  Awali, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Mkuu wa Idara ya Nidhamu na Maadili ya CUF, Abdul Kambaya alisema Hamad na wenzake hao 12 wanaitwa kwenye kikao hicho ili kusomewa tuhuma zinazowakabili na kuwapa fursa ya kujieleza.

  "Tayari tumeshawapa barua za kuwaita kwenye Kamati ya Nidhamu ya Chama kuanzia 27 na 29 kwa mahojiano zaidi," alisema Kambaya na kuongeza kuwa kuhojiwa kwa viongozi hao kuna baraka zote za chama.

  Mbali na Hamad, Kambaya aliwataja watuhumiwa wengine walioitwa kwenye kamati hiyo kuwa ni Juma Saidi Saanan (Mjumbe wa Baraza Kuu Unguja) na Shoka Khamis Juma (Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Pemba).

  Wengine ni Doyo Hassan Doyo (Mjumbe wa Baraza Kuu Tanga), Yasini Mrotwa (Mjumbe wa Baraza Kuu Mbeya), Doni Waziri (Mwenyekiti wa Wilaya ya Ilala) na Mohamedi Massaga (Katibu wa Wilaya ya Ilala).

  Wanachama wengine Albadawi (Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke), Amir Kilungi, Yusufu Mbungilo (Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Wilaya ya Temeke) na Nanjase ambaye ni Mwenyekiti wa Wilaya ya Nachingwea.

  Pia wamo Tamimu Omari (Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkunduge, Kata ya Tandale) na Ahmed Issah kutoka Wilaya ya Morogoro Mjini."Tumeamua kuwaita kwa malengo ya kujadiliana na kuangalia mustakabali wa chama kwa mujibu wa katiba ya chama chetu," imesema taarifa hiyo na kuongeza:

  "Tunawomba wanachama kuendeleza amani na utulivu hasa katika kipindi hiki ambacho chama kinakaa katika vikao vya uamuzi."
  Baadaye Kambaya alisema kwa simu kuwa kamati hiyo, haina mamlaka ya kuwapa adhabu watuhumiwa hao hata kama watabainika kuwa na makosa.

  "Sisi kazi yetu ni kuwasomea tuhuma zao na watapewa muda wa kujieleza kisha tutapendekeza adhabu kwenye vikao vya uamuzi ambavyo ni Kamati ya Utendaji na Baraza Kuu la Uongozi."

  Alipoulizwa vikao hivyo vitakaa lini alisema: "Kamati ya Utendaji itaketi Desemba 30 na Baraza Kuu la Uongozi Desemba 31, mwaka huu."
  Hata hivyo, alieleza kuwa mtuhumiwa asiyekubaliana na uamuzi wa vikao hivyo anaweza kukata rufaa kwenye Mkutano Mkuu wa Taifa ambao katika suala hilo, utapangwa na Baraza la Uongozi.

  Ingawa haijathibitika kama Hamad na wenzake hao watafukuzwa uanachama, CUF ina historia ya kufanya hivyo kwa wanachama wake. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa waliowahi kukumbuwa na masahibu hayo ni pamoja na aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, James Mapalala na aliyekuwa Mbunge, Naila Jidawi na Salum Msabaha.

  Lakini Kambaya alisema katika taarifa hiyo kuwa: "Tunawaahidi wanachama na Watanzania kuwa hatutamuonea yeyote katika uamuzi utakaotolewa na vikao vyote."

  Mgogoro wa Hamad na Maalim Seif ulianza kuibuka baada ya Hamad kutangaza nia yake ya kuwania ukatibu mkuu wa CUF kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika 2014.

  Mgororo huo ulipambana moto mwishoni mwa Novemba katika mkutano wa Hamad uliofanyika Manzese, Dar es Salaam ambako mabaunsa wa chama hicho walivamia mkutano huo na kusababisha mapigano baina yao na wanachama waliokuwa wamehudhuria.

  Tangu hapo, Seif na Hamad wamekuwa wakizunguka kwa nyakati tofauti mikoani mbalimbali nchini na kutoa matamko kadhaa kuhusu ugomvi huo.Mara ya mwisho Seif akiwa Mwanza, alisema mgogoro huo utamalizwa katika vikao vya ndani vya chama hicho.

  Kwa upande wake, Rashid akiwa mkoani Singida alisema hana hofu na vikao hivyo na kwamba anavisubiri kwa hamu ili akaseme kile alichokiita ukweli juu ya hatima ya chama hicho chini ya uongozi wa Maalim Seif.

  Source: MWANANCHI
   
 2. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Magamba bana wanakutumi ukiishiwa thamani wanakupiga teke!!

  Kama mnakumbuka Hamadi Rashidi na David Kafulila si ndio walikuwa mstari wa mbele na kwa kuungwa mkono na wabunge wa magamba mapema mwaka huu walitaka kuunda kambi ndogo ya upinzani bungeni??
   
 3. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #3
  Dec 27, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Niliwahi kumsikia Hamad anasema kuwa ndani ya CUF hakuna kaamati ya nidhamu na maadili. Sasa sijui katiba imebadilika ndani ya siku hizi chache?
   
 4. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #4
  Dec 27, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwa usalama wa CUF wampige chini Hamad Rashid, wakimwacha na tamaa ya madaraka aliyonayo atawasumbua sana baada ya kukosa kuongoza kambi ya upinzani sasa anataka amtoe Maalim ukatibu il awe waziri kiongozi
   
 5. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #5
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Labda wamecopy toka kwa wengine tu!
  Mi kinachonishangaza ni hawa jamaa DK na HR inonekana ni watu wa kupenda madaraka na si vinginevo ndo maana hata bungeni walishadadia kuundwa kwa kambi ndogo ya upinzani!
   
 6. M

  Mwamakula JF-Expert Member

  #6
  Dec 27, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 1,893
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Kamati ya Maadili ipo CCM tu na siyo vyama vya upinzani
   
 7. WAHEED SUDAY

  WAHEED SUDAY JF-Expert Member

  #7
  Dec 27, 2011
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 7,155
  Likes Received: 1,249
  Trophy Points: 280
  huyu HR ni wakupigwa chini tu anatamaa sana ya madaraka kuliko mnavyoamini
   
 8. M

  Molemo JF-Expert Member

  #8
  Dec 27, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Nimefuatilia majina yote nikayasoma mara mbili mbili nikagundua kitu kwamba wanachosema kuhusu hiki chama yana ukweli
   
 9. MAGEUZI KWELI

  MAGEUZI KWELI JF-Expert Member

  #9
  Dec 27, 2011
  Joined: Jul 16, 2011
  Messages: 1,943
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  bismilah rahman rahim......takbirrrrrrrrrrrrrrrr....
   
 10. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #10
  Dec 27, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [h=2]27 DECEMBER 2011[/h][h=3][/h]

  *Kamati ya nidhamu, maadili kumuhoji na wenzake 12
  *Wote watuhumiwa kukiuka utaratibu, katiba ya chama
  *Ripoti ya mahojiano kuwasilishwa Kamati ya Utendaji
  *Mtatiro: Njia aliyotumia haiwezi kukijenga chama chetu


  Na Mwandishi Wetu

  CHAMA cha Wananchi (CUF), kimeanza mchakato wa kumaliza mgogoro unaoendelea ndani ya
  chama hicho ambapo leo, Kamati ya Nidhamu na Maadili itamuhoji Mbunge wa Wawi, Zanzibar, Bw.Hamad Rashid Mohammed, juu ya tuhuma alizozitoa hivi karibuni kupitia vyombo vya habari.

  Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana kwa vyombo vya habari, imesema mbali ya kamati hiyo kumuhoji Bw.Mohammed, pia itawahoji wanachama 12 ambao wote wamepewa barua za kuitwa na kamati hiyo.

  Mkuu wa Idara ya Nidhamu na Maadili ya chama hicho, Bw.Abdul Kambaya, alisema mahojiano hayo yatafanyika kwa siku tatu kuanzia leo hadi Desemba 29, mwaka huu.

  Alisema kamati hiyo ilikutana juzi na kuazimia kuwaita watuhumiwa 13 akiwemo Bw.Mohammed na wanachama wenye nyadhifa mbalimbali katika chama ili wahojiwe kwa kosa la kukiuka utaratibu na katiba ya chama.

  “Kesho (leo), tutaanza kumuhoji Bw.Hamad kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa sita, baada ya hapo tutamuhoji Bw.Juma Saidi Saanan (Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Unguja, Zanzibar), kuanzia saa sita hadi tisa alasiri na mwisho tutamuhoji Bw.Shoka Khamis Juma (Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Pemba, Zanzibar), kuanzia saa tisa hadi 12 jioni,” alisema Bw.Kambaya.

  Aliwataja wanachama wengine ambao watahojiwa kuwa ni Bw.Doyo Hassan Doyo (Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Tanga), Bw.Yasini Mrotwa (Mjumbe wa Baraza Kuu kutoka Mbeya), Bw.Doni Waziri (Mwenyekiti wa Wilaya ya Ilala) na Bw.Mohamedi Massaga (Katibu wa Wilaya ya Ilala).

  Wengine ni Bw.Albadawi (Mwenyekiti wa Wilaya ya Temeke), Bw.Amir Kilungi, Bw.Yusufu Mbungilo (Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi Wilaya ya Temeke), Bw.Nanjase (Mwenyekiti wa Wilaya ya Nachingwea), Bw. Tamimu Omari (Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkunduge, Kata ya Tandale) na Bw.Ahmed Issah kutoka Wilaya ya Morogoro Mjini.

  “Kamati hii imeamua kuwaita kwa lengo la kujadiliana na kuangalia mustakabali wa chama chetu kwa mujibu wa katiba juu ya tuhuma zinazodaiwa na Bw.Mohammed pamoja na wanachama wengine 12 katika kipindi cha miezi miwili sasa,” alisema Bw.Kambaya.

  Alisema baadhi ya wanachama hao wana makosa yanayofanana na wengine yanajitegemea ambapo baada ya mahojiano, kamati itapeleka taarifa kwenye Kamati ya Utendaji Taifa ya chama hicho ambayo ndiyo yenye mamlaka ya kutoa maamuzi.

  Aliongeza kuwa, kama kuna mwanachama ambaye hatakubaliana na maamuzi ya Kamati ya Utendaji, anaruhusiwa kukata rufaa katika Baraza Kuu la chama hicho.

  Bw.Kambaya alisema, hadi sasa Bw.Mohammed hajapeleka tuhuma zozote katika chama kwa maandishi bali madai yake wanayasikia kupitia vyombo vya habari jambo ambalo ni kinyume na taratibu za chama hicho.

  Aliwataka wanachama wa CUF, kuendeleza amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha vikao vya maamuzi ambavyo haviwezi kumuonea mwanachama yeyote.

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Bw.Julius Mtatiro, alisema kitendo cha Bw.Mohammed kutotumia vikao vya chama ni utashi wake mwenyewe.

  “Bw.Mohammed ameshindwa kutumia vikao, ndiyo maana wameamua kumuwahi, CUF inaendeshwa kwa taratibu na kanuni, kuna vikao vya chama ambavyo mwanachama anaweza kutoa hoja yake na wajumbe wakaikubali au kuikataa,” alisema.

  Aliongeza kuwa, njia anazotumia Bw.Mohammed haziwezi kukijenga chama hicho ndiyo maana CUF imeamua kuchukua hatua za kumuita na kumuhoji.

  Majira lilipomtafuta Bw.Mohammed ili kuthibitisha kama alipokea barua hiyo na kushindwa kuwasilisha tuhuma zake kwa uongozi wa chama, simu yake ya mkononi ilikuwa imezimwa.

  Wiki iliyopita, Bw.Mohammed akiwa mkoani Tanga, alikanusha taarifa iliyoandikwa na gazeti moja linalotoka kila siku siyo (Majira) likimnukuu amekwenda kumuomba radhi Katibu Mkuu wa chama hicho ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad ili asifutiwe uanachama na kupoteza ubunge.

  Bw.Mohammed alidai kushangazwa na Maalim Seif kuendeleza malumbano katika vyombo vya habari na kukiuka agizo lake kuwa matatizo yote yanayotokea katika chama yafikishwe kwenye vikao si vinginevyo.

  Alisema dhamira yake ni kupeleka tuhuma nne kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba akimtuhumu Maalim Seif ili aweze kuchukuliwa hatua kwa madai ya kushindwa kusimamia shughuli za chama na kusababisha kipoteze mwelekeo.

  Alizitaja tuhuma hizo kuwa ni pamoja na ofisi yake kushindwa kufanya kazi za chama upande wa bara na kusababisha chama hicho kishindwe vibaya katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2010.

  Tuhuma nyingine ni matumizi mabaya ya fedha na rasilimali za chama na ofisi yake kushindwa kutoa huduma stahiki kwa upande wa Bara na Zanzibar.

  Bw.Mohammed alisema tuhuma ya nne ni chama hicho kushindwa kuutendea haki upande mmoja wa Jamhuri akitolea mfano katika Uchaguzi Mkuu uliopita, Maalim Seif alishindwa kushiriki katika uzinduzi na ufungaji wa kampeni kwa upande wa bara   
Loading...