Hati ya kusafiria

Hati ya kusafiria

Range rover

Senior Member
Joined
Nov 22, 2016
Posts
186
Reaction score
199
Wadau habari za asubuhi!
Naombeni ushauri kwa anaefahamu ni hivi passport yangu ina majina. manne niliomba kitambulisho cha Taifa kwa majina yote manne ila kilivyotoka kuna majina ma tatu tu,na documents zangu zote zina majina manne,je nichukue hatua gani?isije kuni cost maana uhamiaji siku hizi hawatabiriki.Aasanteni
 
Si urudi huko ulikoanzia mchakato huku watakusaidia kuondoa hilo jina moja!
Wadau habari za asubuhi!
Naombeni ushauri kwa anaefahamu ni hivi passport yangu ina majina. manne niliomba kitambulisho cha Taifa kwa majina yote manne ila kilivyotoka kuna majina ma tatu tu,na documents zangu zote zina majina manne,je nichukue hatua gani?isije kuni cost maana uhamiaji siku hizi hawatabiriki.Aasanteni
 
Tatizo ni kuanza kuondoa jina moja kwenye vyeti vyote vingine ni vya taaluma ndio hapo kichwa kinapo uma
 
Kama kitambulisho kina majina matatu, na Kama ndiyo idadi inayokubalika kwenye kitambulisho wala usipanic. Na wala usiondoe jina lolote kama documents zako zote zina majina hayo kasoro kitambulisho cha taifa tu.
Binafsi nilifanya hivi, Nilienda mahakamani, nikajaza form ya kubadili majina lakini haubadirishi kitu, unaapa mbele ya jaji kwamba hayo ni majina yako kama yalivyoonyeshwa kwenye cheti chako cha kuzaliwa na documents zingine. Hiyo form unakuwa nayo, pamoja na documents zako, popote wakiuliza, unawaeleza NIDA wanachukua majina matatu, na wakihitaji proof utakuwa na court document.
Binafsi nilipata tatizo hilo, huko nje niliwahi kwenda, lakini document yangu ya court ilinisaidia.
 
na kama tarehe zimekosewa kati ya kitambulisho ta taifa na cheti cha kuzaliwa lakini jina ni moja kwenye vyeti vyote hapo inakuwaje?
 
Back
Top Bottom