Mheshimiwa, nashindwa hata nianzie wapi kwasababu rais wetu mpendwa ndiye rafiki yake mmoja wapo wa huyu al bashir na kikwete kwa mdomo wake alilaumu mataifa mengine kutokuwachukulia marais wa africa kihivyo....ni kitu cha ajabu dunia nzima inashangaaa. Turkey ambao ni islamic nation ilimwambia kuwa akitembelea uturuki watamkamata, lakini tz alikuja siku ile kwenye sulivan akakalishwa kwenye kiti pamoja na marais kama kawaida, hakukamatwa.
kwa kufupi, hii warrant ya arrest ni halali kabisa kwasababu al bashir amekuwa indirect perpetrator wa mauaji ya watu weusi kule sudan....na makosa ambayo sina wasiwasi nayo kuwa akikamatwa lazima ataswekwa ndani nayo ni CRIMES AGAINST HUMANITY AND WAR CRIMES....mwanzoni waliweka hadi GENOCIDE kwasababu ilionekana kama wale watu wanaouawa ni wa rangi moja na wengi wao ni kabila moja na kwasababu khartoum ni waarabu waliowengi, prosecutor alitazama kama kutakuwa na genocide..ikashindikana hivyo waka drop charge ya genocide zikabaki izo mbili ya war crimes and crimes against humanity.
kwanini ameshutumiwa na makosa hayo? ni kwasababu al bashir amekuwa akiwatumia kwa mlango wa nyuma (indirectly) janjaweed militias kuua watu halaiki, choma nyumba zao, baka na fanya vitendo vyote vya kiovu,...kuna ushaidi wa kutosha kuthibitisha hilo na yeye amekuwa akiwatumia janjaweek kama silaha ya kuwashambulia adversary wake....
sina uhakika, inawezekana genocide ilisharudishwa mwaka jana au mwaka huu kama sikosei, nitajaribu kusoma iyo doc uliyoweka na material zingine nione...na inawezakana kabisa kuna genocide pale..you know ili kuwe na genocide kunatakiwa kuwe ne proof kuwa the perpetrator intended to terminate/destroy in whole or in part an ethnic,racial, national...etc utasoma hii kwenye ICC STATUTE...ila kinachoangaliwa sana ni "intent to destroy a group" yaani ndo mens rea yake...na kuna ushaidi kuwa al bashir huwa anataka kuteketeza kizazi cha hawa watu weusi sana ili wabaki race ya waarab na machotara kama ilivyo kaskazini mwa sudan.....just kama Turkey walivyofanya kwa armenians, hitler alivyofanya kwa wayahudi, kule cambodia etc....nitakuja na argument za kisheria baadaye...kwasasa nilikuwa naongea kama layman...