Hatari ya Rais kuangushwa kwa maslahi ya mafisadi

RingaRinga

JF-Expert Member
Jul 10, 2015
1,041
510
Unaweza kudhani tuko salama mikononi mwa rais Magufuli lakini ni salama kiasi gani hakuna aliye na hakika.

Mafisadi na waliolewa uongozi wanaweza kufanya chochote, hata kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye pia usishangae hii ikafanywa na wabunge toka vyama vyote hasa kwa kuwa rais amekuwa akigusa pia masilahi ya wabunge kuanzia mikopo ya magari ya wabunge hadi juzi bilioni 6 zilivyoondolewa ktk mfuko wa bunge na Magdalena Sakaya akalalamikia kitendo hicho, kuna possibility kwamba linapokuja swala la maslahi ya wabunge uzalendo na vyama huwekwa pembeni.

Rai yangu kwa wabunge wazalendo kutoka vyama vyote utakapofika wakati wa 'masia' kutundikwa msalabani chondechonde nawaomba sana msimame nyuma ya rais wetu mpendwa mkombozi wa wanyonge nnahakika 90%+ ya wananchi watamsupport ili kuhakikisha ukombozi kamili wa nchi hii unapatikana.

Kuna ukweli usiopingika kuwa asilimia kubwa ya wabunge wetu ni wale wanaojua kuwa tumewapa ubunge kama zawadi na si wao kutuongoza kututoa katika umaskini na shida za sampuli mbalimbali zilizokithiri.

Kama ikitokea bunge likavunjwa nna imani baragumu litakalopigwa na Magufuli kutafuta kuungwa mkono, watakaokuwa nyuma yake ni wabunge ambao wao watakuwa wamejitathmini na kuona kuwa wataendana na kariba ya rais wetu ya kujitoa sadaka kwa ajili ya wananchi na si kwa masilahi ya chama kwanza.

Naomba kunukuu maneno ya busara kwamba;-
"Don't run after happiness but make other people happy and you will find happiness is running after you" kwamba, tusitafute kujifurahisha wenyewe badala yake tuwafurahishe wengine kisha furaha yenyewe itakuja ikitukimbilia.

Hivi kuna propaganda gani yenye nguvu ya kujenga chama badala ya hii ya kutumikia wananchi kizalendo kama anavyofanya Rais wetu Ndugu John Pombe Joseph Magufuli?
 
Wabunge maslahi ni wengi sana nao wanatoka chama cha mafisadi (ccm)
 
Sina cha kusema sana, uko sahihi na usemacho ni kweli. lets pray for our JPM
 
kiujumla wabunge wetu wengi ni wachumia tumbo na sio wa kutumikia wananchi. ukienda vijijini muda huu wa mvua barabara nyingi hazipitiki. lakini wabunge wako dar wanakula raha. tuendelee kumuombee maghufuli ili aendelee kutumbua majipu..
 
tatizo lililopo ni kuwa asilimia kubwa ya wabunge wetu wametumia rushwa kwenye uchaguzi, kuanzia ngazi ya vyama hadi kwenye uchaguzi mkuu.wengine waliuza mali au kuingia kwenye madeni makubwa.usitarajie wabunge hao wawe na utashi wa kuwawakilisha wapiga kura wao bali akili zao ziko kimaslahi zaidi.ndio haya tunayoyashuhudia sasa.
 
Watakao mdondosha Magufuli ni watu kutoka chama chake (Lugumi na washirika wake) kwani ndio wanaongoza kwa vitendo vya kifisadi. Tangu Magufuli ashike dola, kashfa zote za ufisadi zilizopata kuibuka zimehusisha wanachama wa CCM. Licha ya hii ya Lugumi, kuna kashfa ya wabunge kuchukua rushwa toka kwa wakurugenzi wa mashirika ya umma kwa mgongo wa Kamati za Bunge. Hata akiunda mahakama ya majizi itasheheni wana CCM watupu.
 
Nadhani uwajui ccm vizuri ila huu mchezo awatauweza huyu jamaa Ni mtu wa kitengo na anawaamini Sana hasa linapokuja suala la sabotage. Mswahili anapambana Sana kumuaribia huyu jamaa but now is just like a toothless dog.
 
Muhimili wa bunge auache ufanye shughuli zake hapo tutakuwa wote nyuma yake lakini ya kutaka bunge liwe chini yake, mahakama pia iwe chini yake hiyo hapana haiwezi kutufikisha popote kimaendeleo.
 
Wapiga deal chadema safari marekani na dubai msimu huu. Hakuna

Mkuu hii vita ya ufisadi haina chama, tukisema tuangalie vyama hadi sasa hivi chama gani viongozi wake wameghubikwa na kashfa za rushwa? Tuweke mambo ya uchama pembeni, na wote tuseme kila ajihusishaye na rushwa/ufisadi apate stahiki yake bila kujali anatoka chama gani.
 
Kama alivyopinga Dar kung'ang'ania Meya kuwa CCM, Ukwawa wanamuelewa vizuri jinsi anavyotekereza sera zao hawatamwangusha ila ni wachache. Kura zikipigwa utashangaa kijani zitatoka kiduchu hasa wale wapiga vigeregere na kucheza mchiriku juu ya wenzao.
 
sasa chadema ndiyo wameshika dola mdau ebu toa ufafanuzi aise
Mwaka jana Joyce Mukya alikuwa kikazi za bunge marekani lakini kiongozi wa KUB akiwa Dubai alimuita akatize ziala amfuate Dubai kwa gharama za bunge
 
tatizo lililopo ni kuwa asilimia kubwa ya wabunge wetu wametumia rushwa kwenye uchaguzi, kuanzia ngazi ya vyama hadi kwenye uchaguzi mkuu.wengine waliuza mali au kuingia kwenye madeni makubwa.usitarajie wabunge hao wawe na utashi wa kuwawakilisha wapiga kura wao bali akili zao ziko kimaslahi zaidi.ndio haya tunayoyashuhudia sasa.
Tunafanyaje kuondokana na hali hii?
 
Back
Top Bottom