Hatari, Soma hapa : Tuwe Makini! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatari, Soma hapa : Tuwe Makini!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BIG Banned, Jun 26, 2012.

 1. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #1
  Jun 26, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Nimepata email kutoka kwa mshikaji, Insikitisha, inatisha sana, nimeona bora niwashirikishe ndugu zangu wa JF.


  Dear friends Leo nimeona ni vyema nika-share nanyi kisa hiki cha kutekwa mfanyakazi mwenzetu ambaye ni cashier siku ya jumatano jioni wiki iliyopita. Ni kama movie lakini ni ukweli, cashier wetu aliomba ruhusa siku hiyo ya tukio aende kwenye mkutano wa wasabato uliokuwa uliendelea viwanja vya biafra. Yeye pia ni msabato aliyeishika dini ya Sabato haswa, kwa hiyo aliondoka saa kumi kamili badala ya saa kumi na moja Baada ya dakika 40 tulianza kupokea sms zinazosema mwenye namba xxx amepata ajali na kufa papo hapo na kwa taarifa zaidi twende muhimbili hospital. Baada ya kutazama hiyo namba xxx ilikuwa ni ya cashier wetu. Tulijaribu kuipiga iliita tu bila kupokelewa, na pia tulipiga namba iliyotutumia sms iliita bila majibu. Ilipofika saa kumi na moja tuliamua kuelekea muhimbili, na baada ya kufika pale emergence tukaambiwa tuelekee chumba cha kuhifadhia maiti. Tulioneshwa mwili wa mtu aliyepata ajali lakini haukuwa wa cashier wetu, tukawatuma wenzetu waende hospitali zote lakini hapakuwa na taarifa zake Baada ya kuzunguka bila mafanikio tulitoa taarifa makao makuu ya usalama barabarani na baada ya dk kumi wakatwambia kuwa hakuna taarifa za ajali mbaya iliyotokea jioni hiyo. Hatua iliyofuata ilikuwa ni kutoa taarifa polisi juu ya tulio hilo na ndipo waliposema kwa kuwa ni mtu mzima tusubiri hadi siku inayofuata. Wakati huo huo ndugu zake pamoja na wafanyakazi wenzetu walikuwa pamoja wakiendelea na jitihada za kumtafuta hadi saa sita usiku. Kilichokuwa
  kinatia wasiwasi zaidi ile namba iliendelea kutumia sms namba takribani zote zilizokuwa kwenye phonebook yake na ndugu zake hawakuwahi kuona ndugu yao akichelewa kiasi hicho. Ilipotimu mida kama ya saa sita na nusu walisikia mtu akigonga mlango, alikuwa kaumizwa na amejaa matope, hakuwa na uwezo wa kuzungumza sana, ilibidi wampeleke kituo cha polisi na baada ya muda hospitali ya mwananyamala. Alipopata nguvu alianza kuwasimulia nduguze kilichotokea. Alipotoka ofisini alikwenda moja kwa moja kwenye kituo cha daladala cha karakana, pale kituoni walikuwa abiria wawili yaani yeye na mama mmoja. Baada ya dk chache ilikuja coaster iliyoandikwa mbele Kawe na ilikuwa na tinted nyeusi, yule mama hakupanda sababu alikuwa anaelekea posta ila yeye alipanda. Ndani ya gari kulikuwa na watu watatu pamoja na dereva, wawili wakiwa wamekaa nyuma na mmoja akiwa amekaa karibu na driver. Gari hiyo
  hiyo ilikuwa ni mpya, mmoja wa abiria alimumba simu cashier apige simu moja kwa jamaa yake maana alidai kuwa simu yake illiishiwa charge na walikuwa wametoka mtwara kupeleka maiti, alimuuliza cashier umri wake na kama ameoa na anafanya kazi wapi, cashier akamjibu hajaoa na hana kazi pia ana miaka 32. Walipofika Tazara hawakutaka kupakia abiria yoyote na walikuwa wote wamevaa miwani myeusi, na ndipo akaanza kuingiwa na mashaka akaomba ashuke, wao wakamwambia watapita biafra na hawana mpango wa kusanya kwa kuwa hata yeye walimpa lifti tu. Gari ilipokaribia taa za buguruni akainuka ili ashuke, jamaa wale wa nyuma wakamkalisha chini kwa nguvu, na sio kwenye viti yaani chini kabisa. Mmoja wao akafunga kitambaa cheusi kwenye macho na mikono ikafungwa kwa nyuma na mipira, baada ya muda akasikia kama wamempulizia perfume. Akihisi fahamu kumtoka polepole na neno lamwisho analokumbuka alisikia kuwa waelekee misitu ya Kibaha wakamalize kazi. Kilichomwamsha ni kofi zito alilopigwa na kusukumwa hadi nje ya gari. Alianza kulia na kuwasihi wasimdhuru, wakaanza kumrusha kichurachura huku wakimkanyaga. Walikuwa wameshamfungua kitambaa machoni na waliacha gari umbali kama wa dk kumi na lilikuwa ni pori zito na giza, wao walivaa vitu usoni na walikuwa wamevaa gloves. Wakamwekea simu yake mfukoni wakiwa wametoa simcard, walichomwambia wanachohitaji ni sehemu zake za siri na sio kitu kingine. Mmoja wao akaambiwa alete kisu kikali wanachokitumia, na walipompigia boss wao akawasisitiza nyeti zinazotakiwa lazma ziwe za mtu
  wa miaka 40 na kuendelea. Mwenzao mmoja akasema cashier alisema alikuwa na miaka 32, baada ya kumkagua wakakuta card yake inaonyesha kazaliwa mwaka 1979. Kulingana na yeye asemavyo ndicho kilichomwokoa ila
  waliendelea kumkung'uta kwa hasira. Wakamrudisha kwenye gari na baada ya mwendo wakampakia kwenye gari nyingine ndogo iliyokuwa na watu wawili ambao walimchukua na kumtelekeza maeneo ya sayansi. Hawakuchukua kitu hata kimoja wala kumwambia lolote, siku iliyofuata alipelekwa agakhan kwa uchunguzi zaidi na kwa sasa anaendelea
  vzr. Kwa ufupi ni hayo, ukweli mwenyezi Mungu atulinde na tumwombe pia abadilishe mioyo ya watu ambayo imekuwa migumu mno kwa ajili ya kupatavyeo na utajiri wa haraka.

  Amen.
   
 2. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #2
  Jun 26, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Alinacha!!
   
 3. s

  sawabho JF-Expert Member

  #3
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Mwone Shigongo akufundishe kuandika story ya kusisimua mbayo haijichanganyi na kuonyesha wazi kuwa ni story ya kubuni. Ni Watekaji wa aina gani ambao watazunguka na mateka namna hiyo kutoka Karakana, Buguruni, Msitu wa Kibaha na kuja kumwaacha Sayansi. Ni lazima wangemwacha huko huko Kibaha kama wangeona kuwa sio chaguo lao, yaani watumie mafuta yao kumpeleka mpaka sayansi kwa faida ya nani ?
   
 4. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #4
  Jun 26, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Labda hawajafikia huo uwezo wako!.
   
 5. s

  sawabho JF-Expert Member

  #5
  Jun 26, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Hapana Big Banned, wezi na watekaji wote wanafanya shughuli zao kwa faida na sio kwa hasara, hawataki kupoteza muda. Basi hawa wa kwako wanajifunza, ndio maana hata walikuwa hawafahamu kuwa mtu anayetakiwa ni wa miaka 40+, wakazunguka na huyo ndugu yako kutwa nzima na hatimaye kumrudisha Sayansi salama salmini; kwa maana kwamba hawakuumtoa sehemu za siri walizotumwa na Bosi wao ambaye hakuelekeza anachokitaka mapema.
   
 6. atubariki

  atubariki JF-Expert Member

  #6
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 26, 2011
  Messages: 225
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Poleni xana na ahsante ndugu kwa kutujuza hakika nitakuwa makini
   
 7. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #7
  Jun 26, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Ukiwaona waambie nina umri wa miaka 40 waje wachukue nyeti zangu za kiume kama wanashida nazo.
   
 8. 1

  19don JF-Expert Member

  #8
  Jun 26, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 572
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  pole na asante kwa taarifa
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jun 26, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Jana nimesoma stori hiihii,ndo maana kabla ya kusoma nimeangaliwa imeletwa lini????sasa hata sitak kuamin abt this,,,,,
   
 10. BIG Banned

  BIG Banned JF-Expert Member

  #10
  Jun 26, 2012
  Joined: May 4, 2012
  Messages: 263
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Uamini usiamini sidhani kama msaada kwako. cha msingi jihadhari, kuwa makini, tunakupenda.
   
 11. Mama Yeyoo

  Mama Yeyoo Senior Member

  #11
  Jun 26, 2012
  Joined: Mar 25, 2012
  Messages: 101
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nataka kudharau lakini nikakumbuka wiki uliyopita huku Moshi katika radio Kili FM walitangaza kuhusu kisa cha ukweli cha mama mmoja alipanda hizi Noah zinazoenda Mpakani Tarakea,ilikuwa giza limeanza kuingia so alipoona Noah imesimama akachupa ndani,yule mama kuingia akakuta vijana watatu na dereva,gari ilipoanza mwendo mara paka akatokea paka wakamwambia yule mama kuwa amnyonyeshe yule paka..in short wakamlzamisha hadi walipoona inatosha wakasimamisha gari wakamtupa nje ndio yule mama kumpigia mumewe na kumsimulia kisa chote,pale alipotupwa palikuwa na watu,so baada ya muda yule mama akapoteza nguvu akaanguka wakamuwahisha Mawenzi,by the time wanafika huko akawa amepoteza maisha,daktari akasema kuwa yule mama alikuwa amekaukiwa damu so asingeweZa kuishi....kwa mujibu wa mtangazaji wa hiyo radio hizo facts wamezifuatilia hadi hospitali na kukuta ilikuwa kweli....Kwa mtazamo wangu inaweza kuwa ni kweli
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Jun 26, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Nimeipenda hii Kamanda!
   
 13. G

  Godwishes JF-Expert Member

  #13
  Jun 26, 2012
  Joined: Aug 26, 2011
  Messages: 575
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Aiseee!
   
 14. s

  sawabho JF-Expert Member

  #14
  Jun 27, 2012
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Asante Mkuu, kwa kuipenda. Lakini chukua tahadhari, lisemalo lipo kama halipo laja, hata kama sio hilo la kutaka nyeti za mtu mwenye miaka 40+, lakini la kufanana nalo kama vile kuchukuliwa mkwanja wako na hiyo Blackberry yako.
   
 15. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #15
  Jun 27, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 739
  Trophy Points: 280
  It looks like a well costructed and polished story to share.
   
Loading...