KikulachoChako
JF-Expert Member
- Jul 21, 2013
- 19,880
- 40,040
habari wakuu...jana mwanajamii mwenzenu ilibaki kidogo tu ni rest in peace kutoka kwa wananchi wenye hasira kali...ilikuwa kwenye daladala...kama mnavyojua wana jf usafiri wa umma tabu zake hasa nyakati za asubuhi...basi baada ya daladala kuingia kituoni watu tukaanza kugombania..hatimaye nikafanikiwa kuingia..lakini sikufanikiwa kupata siti....nilisimama na mdada fulani hivi pembeni yangu huku akiwa amening'iniza mkoba wake upande wangu..wakati tunaendelea na safari na hizi barabara zetu zilizo kwenye marekebisho.
ule mkoba ukawa unaning'inia kuniegemea mimi....sasa kuna mtu alikuwa anashuka kituo kinachofuata ikanilazimu kusogea mbele kidogo ili kumpisha mshukaji..kwa bahati mbaya wakati nampisha yule mshukaji mabega yetu yakawa kama yanauvuta ule mkoba wa yule dada..kasheshe likaanzia hapo baada kunihisi mimi ndiye niliyekuwa nauvuta ule mkoba kwa makusudio ya kuiba.
akaanza kunipigia makelele ya wizi..jambo ambalo liliwwapa hamaki abiria wengine wakaanza kunishambulia hadi konda alipoanza kunitetea kwa kuwa alilishuhudia...na ukijumlisha na personality ...abiria wakaanza kunielewa kwamba sikuwa mwizi...ikanibidi nishukie kituo kinachofuata ili kuondoa nuksi...duh..kweli si kila anayekufa kwa wizi basi kaiba kweli..wengine wanasingiziwa tu...tuweni tunaposhambulia wezi....
poleni sana! Naomba kuwaleteeni hiki kisa cha kusikitisha; ilikuwa mwaka jana jamaa yangu na rafiki yangu tulisoma naye o'level huko mara katika harakati za maisha alikuja dsm sasa huo mwaka jana alikuwa na biashara ya butcher na kijana mmoja katika kukosa uaminifu wakadhurumiana na mdhumiwa akiwa rafiku yangu anaitwa frenk warioba. Sasa mkakati ukaundwa na huyo mshirika wake akaitwa na rafiki yake maeneo ya ving'ung'uti kuwa akamlipe pesa yake aliondoka tabata akamuaga mke wake ambaye ana mtoto mmoja. Kumbe mdaiwa wake alikuwa ameandaa raia kuwa kuna jambazi sugu anakuja kufanya uharifu kwa hiyo atamuita na wasifanye kosa zaidi ya kumuua. Mara akapigiwa simu akaenda mara kufika tu maeneo aliyoelekezwa akavamiwa na watu kuanza kumpiga huku wakimwitia jambazi!jambazi! Alipigwa mpaka akawa ameishiwa nguvu. Mwisho akapewa simu aongee na ndugu yeyote ndo akampigia simu mama yake aliye kuwepo musoma mara akamwambia mama nauliwa mimi mwanao nimepaziwa mwizi...! Mama yake huku akisikia makelele mara wakamnyanganya simu jamaa wakamfunga mataili ya magari wakamwagia petroli wakamchoma moto akiwa hai. Nasimulia kama hadithi but it happened hapa dsm mwaka jana. Kibaya zaidi yeye alikuwa mtoto peke yake kwa mama yake ambaye ni mjane. Na kingine mjane huyo akufanya lolote maana ana uwezo wa kufuatilia kifo cha mtoto wake mmoja ili haki itendeke... Kiukweli nilipoambiwa maswaubu ya kifo cha rafiki yangu iliniuma sana na nikamuhurumia na mama mjane na mzee aliyempoteza mtoto wake mmoja na pekee. Kama ugushwa na mkasa huu sema amina kwa marehemu na mama huyu mjane mwenye uchungu mkubwa moyoni mwaje.
Mkuu kisa chako kinasikitisha huu n mkasa ambao huwezi kuuepuka, je huyo jamaa unamfaham aliefanya hayo? Kma c ww je mke wake?
Najarb kuona jinsi ambavyo dunia ilivyo katili