Hatari na Chang a motor za Boeing 787 Dreamlike...

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,265
2,000
Baadhi ya matatizo yaliyogundulika ya aina hii ya ndege ni pamoja na matatizo ya betri ambayo hutumia "lithium" na kusababisha matatizo ya mfumo wa umeme.Mathalan ndege za All Nippon Airways na Japan Airlines ziliwahi kuwaka moto uliotokana na hitilafu ya umeme.Kadhalika ndege ya United Airlines 787 ya marekani iliwahi kukumbwa na tatizo kama hilo lakini kwa bahati yenyewe haikuwaka moto. Matatizo haya yamesababisha Federal Aviation Administration (FAA ) kuuchunguza muundo wa ndege na kutoa ushauri wa kurekebisha.Katika matukio kadhaa FAA ilizuia kabisa ndege hiyo kuruka.Kadhalika imeelezwa kuwa katika ndege mpya 40 zilizotengenezwa za Dreamliner zilikuwa na tatizo katika uundaji wa mabawa yake...Faida kubwa ya ndege hizi inaelezwa ni gharama za kuzitunza ikiwa chini kwa wastani wa asilimia 30 wakati zile za uendeshaji zukipungua kwa wastani wa asilimia 15.Maoni yangu kwa wazee wa maamuzi ya "mwendokasi" ilikuwa ni bora kufanya utafiti kama wapandaji au wateja watarajiwa wanazichukuliaje ndege hizi ambazo Ethiopia wameshaanza zitumia kwa Africa...kwani faida ya wateja wa nchi za magharibi kuchagua ndege gani apande kwao gharama sio "issue" saana kama nifanyavyo mimi na wewe "wazee wa fastjet" bali kwao usalama ndio "priority"...Tusijepoteza mabilioni arafu tukaishia kumlaumu "Wele Malechela and the likes" kama visingizio kama kawaida yetu kutafuta majawabu kwa njaa ya mkato.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom