Hatari!!! Kwa waendesha vyombo vya Moto!

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,931
5,033
Matumizi ya indicator!!!
Hivi unajua matumizi mabaya ya indicator yanasababisha zaidi ya asilimia 20 ya Ajali?
Nakumbusha tena......
Ukiwa mjini Kati, washa indicator angau meta 50 hadi 100 Kabla ya kupinda
Ukiwa nje ya mji - highway washa indictor Walau mita 100 hadi 200 Kabla ya kupinda.
Mwendo wako unavyokuwa wa kasi ndivyo hivyo hivyo unashauriwa kuwasha indicator mapema.

Kumbuka
Kuwasha indicator sio kibali cha kukuruhusu kupinda, ni lazima uangalie side mirror kujihakikishia nyuma na mbele kuko salama Kabla ya kupinda.

kwa wale wasio na uzoefu wa vipimo
meta 50 ni kama nusu ya urefu wa uwanja wa mpira na meta 100 ni kama urefu wa uwanja wa mpira.
 
Safi Sana mleta mada umetoa ushauri mzuri na ni jambo LA kuzingatia!
Licha changamoto ni nyingi maana unaweza wash a endiketa kuashiria unaingia kulia utakuta bodaboda inatokea nyumba yako na kupita hiyo hiyo kuliaaa...
 
Duh,hill suala la indicator madereva wa Dar wanalipuuzia sana, yaani imefikia dereva anapoanza kukata kona ndio anawasha indiketa, yaani inakera sana na ni hatari sana.
 
Hasa madereva wanaotumia bara bara ya sinza wanadharau sana suala la indiketa....hasa kwa sisi madereva wa vipando.....
 
Tatizo mjini humu udereva ni wa kujifunzia viwanja vya mpira, watu ni wapuuzi barabarani hatari.

Mwingine anawasha harafu hazimi,ananyoosha nayo huku inaendelea kuwaka.we uliye nyuma yake ni mwendo wa kuweweseka tu.

Kikubwa mkuu amini barabarani wewe peke yako ndio uko na akili wengine wote wameziacha nyumbani, utapona.
 
boda boda ndio vilaza wa kwanza kwakutokufuata sheria anakuona unaindiketi kukata hata iwe mita mia yeye anapita hivyo kulia bila tahadhari
 
Duh,hill suala la indicator madereva wa Dar wanalipuuzia sana, yaani imefikia dereva anapoanza kukata kona ndio anawasha indiketa, yaani inakera sana na ni hatari sana.
Kuna siku mimi kidgoooo nikagonge ka ist sijui ka vits yn imagine taa imeruhusu halaf km mita mbili hivi kajamaa kakawa kumbe kanaingia kulia mtaani.na kulia kwenyewe hawez pita mpk apishwe na gari ziliko upande wapili...kakawasha indicator ghafla halaf kakasimama kusubiri kapishwe yn nilifunga breki mpk nilihisi zilitaka kufyatuka cz nikisikia saut za ajabu huko chini ya gari...ningemgonga sijui angenilaumu...madereva wa dar wanajifunzia uwani then anatoka kwenda nayo barabaran
 
Back
Top Bottom