Hatari: Kufanya Mapenzi Kwa Njia ya Mdomo

Waongo unatibika na mti shamba unaoitwa " mzinaa" mti huu unapatikana kirahisi tu
 

Shirika la Afya Duniani (WHO) limethahadharisha kuwa, kushiriki mapenzi kwa njia ya mdomo kunasababisha ongezeko la ugonjwa wa kisonono ambao kwa sasa umekuwa mgumu kutibika kutokana na bakteria wanaosababisha kuwa sugu.

Aidha, WHO imeeleza kwamba, kupungua kwa mtumizi ya mipira ya kujamiiana (condoms) kunachochea kwa kiasi kikubwa kusambaa kwa ugonjwa huo wa zinaa.

Ugonjwa wa kisonono kwa sasa umekuwa mgumu kutibika na katika mazingira mengine hautibiki kabisa kutokana na kuendeleza usugu wa dawa (antibiotics) kwa kasi sana.

Ugonjwa wa kisonono husababishwa na bakteria wanaojulikana kitaalamu kwa jina la Neisseria gonorrhoea. Ugonjwa huu husambazwa kufanya ngono isiyo salama kwa njia ya uke, mdomo au njia ya haja kubwa.

Dalili za ugonjwa huu ni pamoja na kutoka maji maji ya njano au kijani katika sehemu za siri, maumivu makali wakati wa kukojoa, pamoja na kutokwa na damu.

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na WHO katika nchi 77, bakteria wanaosababisha kisonono wameonekana kuwa sugu katika dawa zilizokuwa zikitumika kutibu.

Dr Teodora Wi, kutoka WHO amesema kulikuwa kuna kesi tatu kutoka Japan, Ufaransa na Uhispania ambapo ugonjwa huo ulishindikana kabisa kutibika. Alisema kila mara wakianzisha dawa mpya kutibu ugonjwa huo, bakteria huyo aliweza kuihimili dawa hiyo mpya.

Jambao hatarishi zaidi ni kuwa, maambukizi ya ugonjwa huu yapo kwa wingi katika nchi maskini ambapo usugu huo ni mgumu kugundulika.

Ugonjwa wa kisonono unaweza kuathiri uke au uume, njia ya haja kubwa pamoja na koo. Lakini athari za koo ndizo zinazotishia dunia kwa sasa kutokana na watu wengi kujihusisha na mapenzi kwa njia ya mdomo.

Dr Wi alieleza kuwa bakteria hao hukaa sehemu ya nyuma ya koo na mgonjwa anapoanza kupata maumivu na kutibu kwa kutumia dawa za kawaida, hupelekea bakteria hao kujenga usugu dhidi ya dawa hizo na nyingine zitakazotumika mbeleni.
Kwa Wale wamesha patwa na hili Gonjwa la Kisonono la mdomo wanaweza kunitafuta kwa wakati wao ili nipate kuwatibia wapate kupona. Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Herbalist Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe.fewgoodman@hotmail.com What's App +905344508169 Au Ni add Kwa Facebook tumia jina hili mzizimkavu. Au boonyeza hapa.Mzizi Mkavu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom